Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Rabi' II 1447 Na: 10 / 1447
M.  Jumatatu, 13 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuongezeka kwa Umwagaji damu kwenye Mpaka wa Pakistan na Afghanistan na Kushindwa kwa Pande zote mbili Kushikamana na Hukmu ya Mwenyezi Mungu

(Imetafsiriwa)

Mbali na sera ya “kujizuia” iliyotabanniwa na serikali za sasa za Pakistan na Afghanistan kwa maadui wa Umma – Mayahudi, Mabaniani, na Waamerika – Pakistan pamoja na Afghanistan zilitangaza kwamba makumi ya wanajeshi kutoka kila upande walikuwa wameuawa katika mapigano ambayo yalizuka kwenye mpaka wao wa pamoja. Makabiliano hayo yalianza mnamo Jumamosi jioni kwa operesheni iliyoanzishwa na vikosi vya Taliban, na kusababisha Islamabad kuapa kutoa jibu kali. Kabul, kwa upande wake, ilitangaza kuwa vikosi vyake vilifanya operesheni dhidi ya vikosi vya usalama vya Pakistan ili kulipiza kisasi kwa ukiukaji wa mara kwa mara na uvamizi wa anga unaofanywa na jeshi la Pakistan katika eneo la Afghanistan.

Katikati ya matukio haya, India inasimama kwa furaha, ikitazama damu ya Waislamu ikimwagwa kwa mikono ya ndugu zao wenyewe. Haya yanajiri baada ya serikali ya Afghanistan kuchagua kusonga karibu na India – matokeo ya sera za kizembe zilizotabanniwa na uongozi wa Pakistan, ambao uliitenganisha serikali ya Afghanistan na kuwafukuza “wakimbizi” wa Afghanistan kutoka Pakistan. Kwa hiyo, Afghanistan iligeukia India, adui mkuu wa Pakistan. Ukaribu huu usio wa kawaida kati ya Kabul na New Delhi umeikasirisha Pakistan na kuisukuma kuchukua hatua. Kama sehemu ya ukaribu huu, India mnamo Ijumaa ilimkaribisha waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan kwa mara ya kwanza tangu 2021 na kutangaza kwamba misheni yake ya kidiplomasia jijini Kabul itapandishwa hadhi na kuwa ubalozi kamili.

Iwe kuzorota kwa mahusiano kati ya Islamabad na Kabul kunatokana na kuongezeka kwa mafungamano ya dhati ya Afghanistan na India au kwa madai ya kuunga mkono Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), lawama kuu ni kwa serikali zote mbili kwa kushindwa kutatua mizozo yao kwa uhuru – mbali na uingiliaji wa India na kimataifa – na kwa kukataa kuregesha mizozo yao kwa Qur'an na Sunnah, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ]

Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.” [Al-Hujurat: 10]. Badala yake, kila upande ulianza kumtaja mwengine kuwa ni adui au mchokozi wa kigeni. Msemaji wa serikali ya Afghanistan Zabihullah Mujahid alisema katika mkutano na waandishi wa habari wa Jumapili kwamba “wanajeshi 58 wa Pakistan waliuawa katika operesheni hii.” Wakati huo huo, jeshi la Pakistan liliripoti kwamba “wanajeshi 23 wa Pakistan waliuawa shahidi wakitetea hadhi ya eneo la taifa letu dhidi ya uchokozi huu wa wazi,” na kuongeza kwamba “wamewaua au kuwajeruhi zaidi ya wapiganaji 200 wa Taliban na magaidi washirika kupitia mashambulizi sahihi na mabomu.”

Kinyume kabisa na sauti ya kidiplomasia na sera ya “kujizuia” ambayo serikali ya Pakistan inatabanni dhidi ya adui yake wa milele, India, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif aliitishia Afghanistan katika taarifa yake: “Hakutakuwa na kulegeza msimamo katika kutetea Pakistan; kila uchochezi utakabiliwa na jibu kali na la ufanisi.” Kabul ilijibu kwa njia hiyo hiyo, ikionyesha ukosefu huo huo wa ufahamu wa kanuni msingi za Kiislamu na hukmu za lazima. Mujahid alitangaza mnamo Jumapili: “Pakistan imeshambulia asubuhi ya leo, na tuko tayari kujibu kwa nguvu.”

Waislamu wanatamani kiasi gani kuona nguvu na azma kama hiyo ikielekezwa badala yake kwa maadui wa kweli wa Mwenyezi Mungu – wale ambao wameendelea kuushambulia Umma huko Kashmir, Gaza, na Turkestan Mashariki! Hata hivyo watawala hawa ni vibaraka wa wakoloni makafiri, wanaotumikia tu maslahi ya mabwana zao. Miongoni mwa maslahi hayo ni kupandikiza uadui, mgawanyiko, na mfarakano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe. Hali yao inalingana kikamilifu na usemi wa zamani kuhusu waoga: “Simba dhidi ya yake mwenyewe, lakini mbuni vitani.”

Huku Shehbaz Sharif akiwatishia ndugu zake wa Afghanistan, wakati huo huo anajiandaa kuhudhuria kile kinachojulikana kama “Kongamano la Kuvumiliana” (Mkutano wa Amani wa Gaza) huko Sharm El-Sheikh – jukwaa ambalo linatafuta kuficha uhalifu wa Mayahudi – chini ya uenyekiti wa si mwengine ila adui aliyeapishwa wa Ummah, Donald Trump.

Enyi Waislamu wa Pakistan, Enyi wenye ikhlasi katika jeshi la Pakistan!

Watawala na makamanda wenu ni ndio adui zenu halisi, basi jihadharini nao

[هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ] “Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Al-Munafiqun: 4]. Ingehitaji juhudi kidogo sana za kijeshi, kujitolea mhanga, na mauaji ya kishahidi kuikomboa Kashmir au kuwanusuru wanaodhulumiwa katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kuliko yale yaliyotumika kuimarisha udhibiti wa Marekani nchini Afghanistan na kupigana na Waislamu huko. Na watawala wenu na majemedari wenu wanazitumia rasilimali za umma na majeshi yenu katika njia ya Shetani badala ya njia ya Mwenyezi Mungu – kama mnavyotaka na kama Anavyoamrisha.

Inaelekea kwamba damu hii, iliyomwagika kutoka pande zote mbili, itatumiwa vibaya na serikali ya Kabul kama kisingizio cha kukubali kukabidhi Kambi ya Anga ya Bagram kwa Marekani, na kuruhusu Amerika kuitumia kwa mara nyengine tena kama nukta kianzilishi cha mashambulizi dhidi ya hasimu yeyote wa kieneo – hasa wana wenye ik wa Umma.

Hivyo basi, ni wajibu kwa Umma kufanya kazi pamoja na wanachama waaminifu wa Hizb ut Tahrir ili kujiondoa wenyewe kutoka kwa walaghai hawa wanaokiuka matukufu ya Uislamu. Maafisa wanyoofu ndani ya jeshi la Pakistan lazima watoe nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume – kumteua Khalifah ambaye anatawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, kuunganisha Pakistan na Afghanistan na nchi zengine za Kiislamu.

Hii ndiyo dola iliyoahidiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) baada ya zama za sasa za utawala dhalimu, kama alivyosema (saw):

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثم سكت»

“...Kisha utakuwemo utawala wa kutenza nguvu, na utakuweko kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uweko kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” (Imesimuliwa na Ahmad).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.