Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  23 Rabi' II 1443 Na: BN/S 1443 / 01
M.  Jumapili, 28 Novemba 2021

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka katika Kizazi cha Kwanza cha Hizb ut Tahrir

﴿مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ

وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzab: 23]

(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inaomboleza, mmoja wa wanaume wa Hizb ut Tahrir, mbebaji da'wah kutoka safu zake za kizazi cha kwanza, Marehemu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Al-Hajj Hatem Misbah Nasser al-Din (Abu Ahed)

Ambaye alikwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu asubuhi ya leo Jumapili 11/28/2021 M, na Hajj, Mwenyezi Mungu amrehemu, alitumia maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, popote alipokwenda na kusafiri. Na alikuwa Mwenyezi Mungu amrehemu mshale miongoni mwa mishale ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu, ikiwakilisha daw'ah pale inapofuma basi akavumilia kwa utiifu na ikhlasi, ndani ya jela za tawala za vibaraka na madhalimu.

Al-Hajj, Mwenyezi Mungu amrehemu, inashuhudiwa uchu wake wa kuhudhuria na kushiriki katika amali nyingi za da'wah katika ardhi iliyobarikiwa, na kushuhudiwa katika medani za kuamrisha mema na kukataza maovu, kutabanni maslahi ya watu na kupigania mambo yao. Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, hakuwa na chaneli ya kutetea msimamo wa sahaba Tamim al-Dari, ambaye alikuwepo kwenye vikao vya mahakama na visimamo licha ya umri wake mkubwa. Ungemuona akishiriki katika kupinga kanuni ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii na upingaji wa Mkataba wa CEDAW, wakidai haki mbele ya kila njama dhidi ya watu wa Palestina, akizunguka baina ya miji ya Palestina akishindana na mashababu wa Hizb ut Tahrir katika kuitikia wito wa ulinganizi.

Mwenyezi Mungu amrehemu mtu wetu tuliyempoteza kwa rehema pana na amuweke katika mabustani yake makubwa, na hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutaregea, na Mwenyezi Mungu atawalipa familia na jamaa zake ujira mkubwa na kuwapa subira na faraja, na wala hatusemi isipokuwa yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, ni cha Mwenyezi Mungu alichokitoa na ni cha Mwenyezi Mungu alichokichukua na kila kitu mbele Yake kina kipimo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Ardhi Iliyobarikiwa Palestina

- Tanzia ya Al-Hajj Hatim Misbah Nasser Aldeen wakati wa Mazishi Yake -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.