Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mamlaka ya Palestina Yafuata Mbinu za Mashetani Kuhalalisha Uhalifu wake katika Kambi ya Jenin!

Mamlaka ya Palestina (PA) ilikusanya vyombo vyake vya habari na vipaza sauti vya wasemaji na nzi wa kielektroniki (wanyanyasaji wa mtandaoni wanaounga mkono serikali) ili kuchafulia jina kambi ya Jenin na watu wake na kuhalalisha umwagaji wa damu yao. Kisha, ilikusanya vyombo vyake na majambazi katika mji wa Khalil al-Rahman, na wachache wa wale walioitwa watu mashuhuri waliojiuza kwa PA kwa manufaa maovu, na wale ambao iliwatishia kutoka kwa wafanyikazi na walimu. Ilitumia wizara, shule zilizofungwa, na kukodi mabasi ili Jimbo la Khalil al-Rahman, mji na wilaya, ionekane kuwa pamoja nayo katika kumwaga damu ya watu wa kambi ya Jenin. Hii ijapokuwa inajua na wale walio nyuma ya kwamba Khalil al-Rahman, pamoja na watu wake na koo zake, hawawezi kukubali kwamba itoa nusu ya neno kumwaga tone la damu ya Waislamu. Kwa kitendo hiki kiovu, inataka kuleta mgawanyiko kati ya watu wa Palestina (kaskazini na kusini) chini ya pazia la uongo la uhalifu wake.

Soma zaidi...

Tubas ni Shahidi wa Upendeleo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina dhidi ya Maadui wa Palestina na Watu wake

Ni zaidi ya uhaini, kwamba Mamlaka ya Ndani ya Palestina inatangaza uadui wake kwa watu wa Palestina, kama inavyotokea kwa kuwasaka Mujahidina wa Tubas, kuwakamata na kuwapiga risasi, kuwatawanya watu huko kwa gesi ya machozi, kuwaua Mujahidina na kuwatia nguvuni kama wafanyavyo Mayahudi, sawa kwa sawa, na kutenda kwa niaba yake kwa kujaza pengo wakati inashughulika na uvamizi wake dhidi ya Gaza na Lebanon.

Soma zaidi...

Mamlaka ya Palestina Iliyofungamana na Maadui wa Mwenyezi Mungu Yakamilisha Dori ya Ghadhabu katika Kuwatesa Watu wa Palestina na Kuwakamata Watetezi wa Haki

Siku chache zilizopita, vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) viliwakamata Sheikh Aws Abu Arqoub na Sheikh Muhammad Manasrah, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kwa kuwakamata wale wanaosema ukweli, PA na vikosi vyake vinasisitiza kuwa kiongozi wa Mayahudi, wakidunga visu watu wote wa Palestina.

Soma zaidi...

Umbile la Halifu la Mayahudi Kukiuka Nafasi za Ummah na Kuua Watu wake katika Miji Mikuu ni Uhalifu wa Tawala za Kioga mbele ya Umbile la Kiyahudi

Katika shambulizi la kiuhaini na lisilo na aibu, umbile halifu la Kiyahudi lilimuua mkuu wa afisi ya kisiasa ya Hamas jijiniTehran, ambapo Ndugu Ismail Haniyeh aliuawa shahidi alfajiri ya leo na adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Umma. Tunamuomba Mwenyezi Mungu rehema na msamaha wake na amjaalie miongoni mwa mashahidi. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutaregea.

Soma zaidi...

Mkono wa Umbile Halifu Wavamia nchi Yetu ya Yemen na ash-Sham chini ya Njama za Tawala na Kukosekana kwa Uzuiaji

Ndege za umbile halifu la Kiyahudi zilianzisha msururu wa mashambulizi ya kichokozi dhidi ya Yemen. Wakati wa mkutano wake jana, Baraza la Mawaziri la umbile hilo linalohusika na masuala ya usalama liliidhinisha shambulizi hilo dhidi ya Yemen, kwani uvamizi huo ulilenga vituo vya kuhifadhi mafuta na kituo cha umeme katika bandari ya Hodeidah.

Soma zaidi...

Mauaji ya Kikatili dhidi ya Watu Wetu mjini Gaza Bila Uwajibikaji! Lini Tutayaona Majeshi ya Waislamu Yakiinuka?!

Wizara ya Afya mjini Gaza imetangaza kuwa mashahidi 79 na majeruhi zaidi ya 289, baadhi yao wakiwa katika hali mahututi, wamewasili katika hospitali ya Nasser Medical Complex kufuatia mashambulizi ya mabomu kwa kambi za watu waliokimbia makaazi yao huko Mawasi Khan Yunis. Mauaji haya yanajiri baada ya uvamizi huo kufanya mauaji ya kutisha katika eneo la viwandani la kitongoji cha Tel al-Hawa, katika vitongoji vya Mji wa Gaza, na katika kambi za eneo la kati, na kusababisha zaidi ya mashahidi 100, na kuongeza kwa kasi idadi ya majeruhi.

Soma zaidi...

Serikali Vibaraka Zinalipa Uhai Umbile la Mayahudi. Usaliti wa Siri sasa Umekuwa wa Dhahiri!

Chini ya kichwa, "Kuendesha daraja la ardhini kati ya bandari za Haifa na Dubai, kupita Saudi Arabia na Jordan, kuvipita vitisho vya Mahouthi," wavuti ya arabi21.com uliripoti, ukitoa mfano wa Vyombo vya habari vya Kiebrania, kwamba, "Imarati (UAE ) na dola inayokalia kimabavu zilitia saini makubaliano ya kuendesha daraja la ardhini, kati ya bandari za Dubai na Haifa, likipitia katika eneo la Saudia na Jordan, kwa lengo la kuvipita vitisho vya Mahouthi vya kufunga njia za kupitia meli.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu