Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  7 Rabi' I 1447 Na: BN/S 1447 / 03
M.  Jumamosi, 30 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

[وَمَنْ يُهِنِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ مُكْرِمٍ]

Na anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumhishimu. [Al-Hajj: 18]

(Imetafsiriwa)

Baada ya maafikiano yote yaliyofanywa na PLO, ambayo yalifikia uhaini mkubwa kwa kuitoa sehemu kubwa ya Palestina. Na baada ya kukubalika kwake kuwa chombo cha usalama (katika muundo wa mamlaka) kinachowapiga vita watu wa Palestina, kupokonya silaha kambi za ndani ya Palestina kwa kuua, kuzingira na kukamata, na nje ya Palestina kwa uratibu na serikali za Syria na Lebanon, ili kuzuia tishio lolote, kubwa au dogo, kwa usalama wa Mayahudi ndani au karibu na Palestina. Na baada ya kulaaniwa kwake Oktoba 7, 2023, na matakwa yake kupitia kwa mkuu wa Mamlaka hiyo ya kuwaachilia huru wafungwa wa uvamizi huo. Na baada ya kubainishwa kwake na matakwa ya Wamarekani na Mayahudi kwa kutoa wito wa kusalimisha silaha mjini Gaza na utayari wake wa kuwa upande unaotekeleza kile ambacho mashini ya mauaji huko Gaza ulishindwa kufanya.

Baada ya hayo yote na mengine mengi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza katika taarifa yake mnamo Ijumaa tarehe 29/8/2025 kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio anakataa na kubatilisha visa za wanachama wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) na Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kabla ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. (Al Jazeera)

Licha ya upendeleo, makubaliano, na usaliti, na utayari wa PLO kufanya zaidi, utawala wa Trump umeona kuwa ni kwa maslahi ya usalama wa kitaifa wa Amerika “kuwajibisha PLO na PA kwa kutozingatia ahadi zao, na kwa kuhujumu matarajio ya amani.” (US State Dept; Al Jazeera), kana kwamba ilivyofanya PA katika kupigana na watu wa Palestina na kusalimisha nchi haitoshi.

Kwa hivyo, jinai zote za Shirika na Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utayari wao wa kucheza kila dori duni haikuwapa kinga, si kwa Waamerika wala kwa Mayahudi. Bali, kila wakati wanang'ang'ania kuwadhalilisha na kuongeza kile kinachotakiwa kwao. Marekani sasa inashutumu kile ilichokiita “utambuzi wa upande mmoja wa taifa dhahania la Palestina,” (AlJazeera.net) baada ya Mayahudi kuondoa kila uwezekano au upeo wa kuwepo kwake kupitia miradi ya makaazi na kuvunjwa kwa Ukingo wa Magharibi. Hata kama Mamlaka ya Palestina ingewapa Mayahudi Palestina yote, na hata kama ingewasaidia kumuua mtoto wa mwisho huko Gaza, hali yake na walinzi wake ingekuwa kama ya mtu anayekimbilia kwenye utandu wa buibui.

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنْكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتاً وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua. [Al-‘Ankabut: 41].

Au

[كَمَثَلِ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ قَرِيباً ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ * كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنْسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِنْكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ]

Ni kama mfano wa walio kuwa kabla yao hivi karibuni. Walionja uovu wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu * Ni kama mfano wa Shetani anapo mwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.” [Al-Hashr: 15-16].

Wasaliti hawazingatii wala hawana akili. Kurasa za historia, za kale na za kisasa, zimejaa ujumbe kwamba msaliti hana msimamo na watu wake na taifa lake, na kwamba bwana wake hatahifadhi hadhi yake anapojiweka katika hali ya udhalilifu. Atamtupa kando ya barabara au kumwacha kwa taifa lake kumkanyaga siku moja chini ya miguu yao. Tumeshuhudia tawala zilizokufa na wasaliti wakishirikiana na maadui mara nyingi katika zama zote, lakini msaliti hajifunzi somo kutoka kwa wale waliomtangulia!

Usaliti wa Palestina haukuanza siku ambayo PLO iliitelekeza, lakini hata kabla ya hapo, tawala za wahaini zilipotangaza makubaliano ya amani mnamo 1949 na kutoa ulinzi kwa Mayahudi kujenga dola yao. Tangu wakati huo, wametoa ulinzi wake, wakizuia Ummah kufanya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa.

Usaliti wa Palestina ulidhihirika pale tawala za wahaini katika nchi za Kiislamu zilipoitelekeza, na kuibadilisha kutoka kuwa kadhia ya Umma na Dini hadi kuwa kadhia ya kitaifa. Kisha, Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina ikaanzishwa kama mwakilishi pekee wa watu wa Palestina, wakifanya uhaini na makubaliano kwa jina lao. Uhaini huu dhidi ya Palestina na watu wake unaendelea hadi leo.

Kama vile Palestina ilivyoregea jana kutoka kwa Makruseda hadi kukumbatiwa na Ummah mikononi mwa askari waliokusanyika kuikomboa kutoka Mashariki na Magharibi ya ardhi za Kiislamu, itaregea tena, Mwenyezi Mungu akipenda, kwa mikono safi ya wana wa Ummah, ili Palestina iwe lulu ya Ash-Sham na kitovu cha ardhi za Waislamu.

[فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]

“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra: 7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

in katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.