Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  8 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 21
M.  Jumapili, 31 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watu wa Al-Fashir Baina ya Nyundo ya Vita na Kinoo cha Njaa, na Hawana Wokovu isipokuwa kwa Dola ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Mji wa Al-Fashir, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, unashuhudia janga halisi la kibinadamu, huku kukiwa na vita kati ya pande zinazopigana, ambapo makumi ya raia waliuawa katika siku chache zilizopita, huku wakaazi wakiteseka kutokana na kuzingirwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, na njaa ya makusudi, katika kivuli cha kimya cha kituliwa shaka cha kimataifa, huku Umoja wa Mataifa ukithibitisha mauaji ya angalau watu 89 katika mapigano ya siku zilizopita.

Kinachowatokea watu wetu mjini Al-Fashir, cha mauaji, kuhangaishwa, na kufa njaa, hakika ni jambo lililoharamishwa katika sheria ya Uislamu, na ni jinai isiyosameheka. Na ikiwa Vikosi vya Misaada wa Haraka (RSF) vitabeba madhambi hayo, kwa vile wao ndio wanaowazingira raia, wakiwapiga makombora kwa silaha zao, na kuwazuilia chakula na maji, basi jukumu la dola ni kubwa zaidi, kwani inawajibikia raia wake, kwa kauli ya Mtume (saw):

«وَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam (mtawala) ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake.” Pia ina jukumu la kutoa chakula, makaazi na usalama. Akasema (saw): «مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِنًا فِي سِرْبِهِ، مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا» “Mwenye kuamka katika nyinyi akiwa salama katika boma lake, mwenye afya njema katika mwili wake, na ana chakula chake cha siku, ni kana kwamba dunia nzima imeletwa kwake.

Hata hivyo serikali imetelekeza jukumu lake na kuendelea kuomba Umoja wa Mataifa na mashirika yake. Waziri Mkuu Kamil Idris alisema almeliomba Baraza la Usalama kutumia mamlaka yake ya kisheria kukomesha mzingiro unaoendelea dhidi ya mji wa Al-Fashir kwa zaidi ya siku 500, huku akijua kuwa jukumu hilo ni lake. Zaidi ya hayo, Umoja wa Mataifa ulikuwa umetoa, kupitia Baraza lake la Usalama, Azimio nambari 2736 mnamo Juni 13, 2024, kwa kuungwa mkono na wanachama 14 na Urusi kujiepusha, ambapo Baraza hili lilipitisha azimio la kutaka RSF isitishe kuzingira kwao mji wa Al-Fashir, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, na kutoa wito wa kusitisha mapigano na machafuko mara moja mjini Al-Fashir na viunga vyake, na kuondolewa kwa wapiganaji wote wanaotishia usalama na amani ya raia. Azimio hili halijatekelezwa licha ya zaidi ya mwaka mmoja kupita tangu kutolewa kwake! Jambo linalothibitisha kwamba upande unaosimamia vita hautaki mzingiro huu umalizike isipokuwa kwa kuanguka kwa Al-Fashir, ili Darfur iwe yote mikononi mwa RSF na kujiandaa kwa ajili ya kujitenga, kulingana na Amerika inavyotaka, kwani inapanga kuichana Sudan katika vijidola vitano vidogo, ikianza na Sudan Kusini.

Serikali lazima isukume mara moja majeshi yake yote kuvunja mzingiro wa Al-Fashir, ikifuatiwa na misafara ya chakula na dawa. Hili ndilo linalolazimishwa na haki ya uchungaji katika Sharia, na pia ndilo linalohitajika kuzuia mpango wa Marekani wa kutenganisha Darfur.

Enyi Watu wetu wa Sudan: Tiba msingi ya majanga yetu yote katika kila sehemu ya ardhi yetu, kwa hakika tiba inayong'oa mizizi ya Magharibi kafiri kutoka katika ardhi zetu, na kuzima njama za Marekani na dola za kikoloni zinazotaka kuichana Sudan, ni mfumo wa Uislamu, unaotekelezwa na Dola yake, Khilafah kwa njia ya Utume.

Kwa hivyo, fanyeni kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, faradhi ya Mola wenu na chimbuko la utukufu wenu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.