Ni lini Tutakomesha Uingiliaji wa Kafiri Magharibi na Mashirika yake ya Kikoloni katika Maisha Yetu, na Kuelekeza Nyuso Zetu Kwa Al-Waahid, Al-Haakim?
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Chini ya ufadhili wa shirika la Ufaransa la Promediation, vyama vya kisiasa vya Sudan vilifanya warsha jijini Port Sudan, kama ilivyoripotiwa kwenye tovuti ya Sudan Tribune mnamo tarehe 5 Oktoba 2025: “Warsha inalenga kufafanua vigezo vya mazungumzo ya mustakbali yatakayoongozwa na Sudan, ikiwemo washiriki wake, eneo, na dori ya upatanishi wa kimataifa, kulingana na msemaji wa kambi hiyo Mohammed Zakaria. Viongozi wa muungano huo walisisitiza haja ya muungano wa ndani ulioshikamana. Minni Arko Minnawi, mkuu wa kamati ya kisiasa ya umoja huo, alisema hatua ya pamoja kati ya viongozi wa kiraia na kijeshi ni muhimu kwa ajili ya utulivu.