Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 19 Rajab 1447 | Na: HTS 1447 / 77 |
| M. Alhamisi, 08 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkutano na Hotuba katika Mji wa El Obeid
(Imetafsiriwa)
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, wanachama wa Hizb ut Tahrir walifanya mkutano na hotuba ya hadhara katika mji la El Obeid, mji mkuu wa Kordofan Kaskazini, mnamo Jumatano, 18 Rajab 1447 H, sambamba na 7 Januari 2026 M, katika uwanja wa Msikiti wa Soko la Al-Salihin.
Ustadh Muhammad Al-Qouni, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza katika amali hiyo, akielezea kwamba Waislamu hawatakuwa na heshima, usalama, au amani isipokuwa chini ya utawala wa Dola ya Khilafah.
Kisha akatuma ujumbe kwa wale walio katika nafasi za madaraka na ushawishi, wanazuoni, wanasiasa, na wanahabari, akiwahimiza kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Mashababu walibeba mabango yanayoelezea amali hiyo.
Wahudhuriaji waliitikia maandamano na hotuba hizo kwa kuisifu Hizb na Mashababu wake.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
in katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |