Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 14 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: HTS 1447 / 123 |
| M. Jumapili, 31 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vikosi vya Msaada wa Haraka Vinafanya Mauaji Dhidi ya Watu Wasio na Silaha, na Serikali Haiwezi Kuwalinda!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Alhamisi na Ijumaa, Mei 28 na 29, 2026, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilizindua mashambulizi kwenye vijiji vilivyo magharibi mwa mji wa Bara katika Jimbo la Kordofan Kaskazini, na kusababisha vifo vya raia kadhaa wasio na silaha. Mtandao wa Madaktari wa Sudan ulithibitisha katika taarifa mnamo Ijumaa, Mei 29, 2026, kwamba RSF ilifanya mauaji makubwa katika mji wa Al-Marra na vijiji vinavyozunguka, na kuwaua raia 27. Katika ripoti yake ya hivi karibuni mnamo Jumamosi, Mei 30, 2026, Al-Arabiya TV ilisema: “Idadi ya vifo kutokana na mauaji ya Vikosi vya Msaada wa Haraka katika eneo la Al-Marra huko Kordofan Kaskazini imeongezeka hadi 58.” Wakati Vikosi vya Msaada wa Haraka vinafanya mauaji haya katika vijiji vya Kordofan, serikali inalaani tu na kuhesabu waliokufa, bila kuchukua hatua zozote kali kuzuia mauaji haya kutokea. Sudan Tribune iliripoti mnamo Jumamosi, Mei 30, 2026, kwamba serikali ya Jimbo la Kordofan Kaskazini ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikilaani uhalifu na ukiukaji mkubwa uliofanywa na wanamgambo wa waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka dhidi ya raia wasio na silaha huko la Al-Marra katika eneo la Bara Magharibi.
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunawakumbusha viongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka na wanajeshi wao kwamba kuwaua watu wasio na hatia, wasio na silaha ni dhambi kubwa na uhalifu usiosameheka. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[مَن قَتَلَ نَفْساً بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعاً] “aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote.” [Al-Ma'idah 5:32]. Na Anasema (swt) kuhusiana na Nafsi ya Muumini:
[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً] “Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisa 4:93]. Hata mkiepuka adhabu ya dunia hii, adhabu ya Mwenyezi Mungu inawangojeeni Akhera, kwani Mwenyezi Mungu hutoa muda lakini hapuuzi.
Ama nyinyi watawala wa Sudan, jukumu lenu ni kubwa zaidi. Uzembe wenu katika kulinda maisha na heshima ya watu utahojiwa Siku ya Kiyama; siku ambayo hadhi, utajiri, wala mamlaka hayatawafaa. Kwa kuwa mumekabidhiwa mambo ya watu, ima timizeni wajibu wenu wa kuwalinda, au waachieni wale wenye uwezo zaidi yenu. Kwani Mtume (saw) amesema:
«أَلَا كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Hakika kila mmoja wenu ni mchungaji na anawajibika kwa anavyochunga: Imam (mtawala) wa watu ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake.” Makhalifa na watawala wa Kiislamu waliweka mifano bora zaidi katika kulinda maisha ya watu, heshima, na mali zao, kwani huu ulikuwa wajibu na faradhi yao, sio ihsani waliyopewa. Kwa mfano, Umar al-Faruq, khalifa rashid (Mwenyezi Mungu awe radhi naye), alisema: “Wallahi, kama nyumbu angejikwaa kwenye kingo za Mto Furati, ningeogopa kwamba Mwenyezi Mungu angeniuliza kwa nini sikuitengeneza njia, ewe Umar!” Kwa hivyo vipi kuhusu nyinyi, wakati wale wanaouawa kinyama Waislamu waumini, raia wenu ambao mutawajibika kwao Siku ya Kiyama?!
Rambirambi zetu kwa watu wetu katika eneo la Dar Hamid. Tunawasihi kufanya kazi pamoja na wale wanaojitahidi kusimamisha dola ya ulinzi na utunzaji; Dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida ya pili, kwa njia ya Utume, ndiyo pekee inayoweza kulinda maisha na heshima ya watu, na kuwapa maisha yenye hadhi katika radhi ya Mola wao Mlezi.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24].
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |