Afisi ya Habari
Wilayah Syria
| H. 21 Shawwal 1447 | Na: 12 / 1447 H |
| M. Jumatano, 08 Aprili 2026 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Omar Abdel Rahim Khatib (Abu Abdo Khatib)
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)
Kwa kuamini qadhaa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria inamuomboleza kwa Waislamu jumla, na kwa wabebaji dawah haswa, Ndugu Omar Abdul Rahim Khatib (Abu Abdo Khatib), mmoja wa wanachama wake, kutoka kijiji cha Arhab katika vijiji vya magharibi mwa Aleppo, na ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 50, ambayo aliitumia kwa utiifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Alijulikana, Mwenyezi Mungu amrehemu, kwa tabia yake safi na tabia yake ya upole. Alikuwa na matarajio makubwa, azma isiyoyumba, na bidii kubwa kwa Dini ya Mwenyezi Mungu, akifanya kazi bila kuchoka kutekeleza Sheria Yake Takatifu chini ya Khilafah. Alibeba ulinganizi wa Uislamu kwa ikhlasi, uvumilivu, na uthabiti, akivumilia shida, mateso, kifungo, na hali ngumu ya maisha. Alikamatwa wakati wa enzi ya utawala wa zamani mnamo 2006 na kuachiliwa huru mnamo 2011, akiendelea na dhamira yake ya kueneza ujumbe pamoja na Hizb ut Tahrir, kwa uvumilivu na matumaini ya thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Alishiriki katika mapinduzi ya Syria tangu mwanzo wake hadi Mwenyezi Mungu alipotupatia ukombozi, hadi Mwenyezi Mungu alipoamuru kwamba atuondoke leo hadi kwenye makao ya milele na rehema ya Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu amrehemu, aliishi akibeba ujumbe wa Uislamu na mradi wa Khilafah, akiwa imara katika agano lake na Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo tunavyomwona, na hatufikirii kumhukumu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu amkubali miongoni mwa watu wema, amkumbatie katika rehema Yake isiyo na mipaka, na ampe Pepo ya juu zaidi akiwa pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, na wema—na ni kundi bora lilioje hilo! Pia tunamwomba Yeye, Aliyetukuka, atupe sisi na familia yake subira na faraja.
Ni cha Mwenyezi Mungu kile anachotoa na anachochukua, na kila kitu kwake kina wakati wake uliowekwa. Hatusemi ila yanayomridhisha Mola wetu Mlezi, Aliyetukuka: [إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutaregea”.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Kalima ya Ustadh Ali Abdul Rahman katika Kikao cha Rambirambi
cha Ustadh Omar Abdul Rahim Khatib (Abu Abdo Khatib), Mungu amrehemu.
Jumatano, 21 Shawwal 1447 H, sawia na 8 Aprili 2026 M

| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Syria |
Address & Website Tel: |