Makubaliano ya Aibu ya Kuhalalisha Usalama na Mayahudi na Miradi ya Ugawaji ni Hatari Kubwa Inayolenga Kuvunja Utashi wa Kiota na Ushindi Uliopata
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika taarifa ambazo, kusema kwa uchache, ni hatari, zilizotolewa na mkuu wa awamu ya mpito, Ahmed al-Sharaa, vipengee vya hali ya sasa ya Syria vilifichuliwa. Alionyesha kwamba “Syria inajua jinsi ya kupigana, lakini haitaki tena vita,” na kwamba “haina chaguo ila kufikia makubaliano ya usalama na Israel,” wakati “kujitolea kwa Israel kwa makubaliano haya ni suala tofauti.” Pia alieleza kuwa matukio ya Sweida yalikuwa tu “mtego uliotayarishwa makhsusi kuzuia makubaliano ya awali juu ya utaratibu wa usalama,” na kwamba “baadhi ya mirengo ndani ya SDF na PKK ilivuruga makubaliano ya Machi na kupunguza kasi ya mchakato huo.” Amesisitiza kuwa “hali ya kaskazini mashariki mwa Syria inatishia usalama wa kitaifa wa Uturuki pamoja na Iraq,” na akadokeza kuwa “ikiwa uwiano hautafikiwa ifikapo Disemba, Uturuki inaweza kuchukua hatua za kijeshi.”