Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  5 Jumada II 1447 Na: 1447 / 04
M.  Jumatano, 26 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

GHASIA ZA TANZANIA ZA BAADA YA UCHAGUZI WA 2025

(Imetafsiriwa)

Wapendwa Waandishi wa Habari,

Tanzania imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa tangu siku ya uchaguzi ya tarehe 29 Oktoba 2025 na baadaye kwa siku kadhaa, na kusababisha vifo na uharibifu wa mali na miundombinu. Kufuatia tukio hili, sisi, Hizb ut Tahrir / Tanzania, tungependa kuelezea yafuatayo:

Kama tulivyosema kila mara kwamba demokrasia pamoja na mfumo wake wa vyama vingi ni mfumo wa kisiasa wa ubepari ambao ulianzishwa na wakoloni wa Magharibi kwa maslahi yao wenyewe, si kwa ajili ya matamanio, maslahi, au maendeleo ya nchi zetu kama wengi wanavyoamini hadi kufikia hatua kwamba baadhi ya watu huchanganyikiwa na matumaini ya uongo, kupoteza muda mwingi, rasilimali, na hata kuhatarisha maisha yao kwa kutarajia mabadiliko.

Mfumo huu wa demokrasia ya vyama vingi ulianzishwa na wakoloni kupitia uhadaifu na udanganyifu kwa lengo la kubadilisha sura ya utawala, kwani waligundua kuwa watu wamechoka na kulikuwa na kutoridhika kunakoongezeka kutokana na ukatili wa mfumo wa chama kimoja ambao ulilindwa nao (Magharibi) baada ya kutoa uhuru bandia. Kwa mfumo huu, wamagharibi pia wanalenga kuwadanganya watu kwamba wao pia wana dori ya kufanya maamuzi, jambo ambalo si kweli, kwani hata nchini Marekani raia hawachagui rais wao moja kwa moja.

Kwa hivyo, mfumo huu wa vyama vingi ulianzishwa kama mkakati mwingine wa kuimarisha ukoloni mamboleo baada ya ukoloni wa zamani na uhuru bandia (uhuru wa bendera), ili kuwazuia watu kufikiria kwa usahihi dhidi ya mfumo wa kibepari. Ikawa sasa, badala ya watu kufanya kazi ya kung'oa mfumo mbovu wa kibepari uliotawala na kunyonya duniani kote, haswa katika nchi zinazoendelea, watu walibaki wamemezwa na nguvu zao katika suluhisho la uongo la kubadilisha sura za watawala huku tatizo msingi, ambalo ni mfumo wa kibepari, likibakia.

Hata hivyo, ikiwa mtawala atalinda maslahi yao vizuri, pande zinazopingana zitaendelea kubaki kama watazamaji. Kwa hivyo, ni wazi kwamba nchi za kikoloni za Magharibi pia zimekuwa zikitumia sera ya mifumo ya vyama vingi na visingizio vyengine kuchochea mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, migawanyiko, na vurugu kwa njia ya ujanja ili kufikia kwa urahisi unyonyaji wao wa rasilimali katika nchi zinazoendelea. Mifano ni pamoja na Sudan, Congo, Yemen, Somalia, na kwengineko.

Bila kusahau kwamba uchaguzi wa vyama vingi ni mkakati wa kikoloni wa kurefusha muda wa uhai wa mfumo wao wa kibepari, na kufanya vyama vya upinzani kuwa silaha ya vyama tawala vya ulimwengu wa tatu, iwapo havitalinda maslahi ya wakoloni, katika hali hiyo vyama vinavyopingana vitapewa mamlaka ya kuondoa chama tawala kutoka kwenye kiti cha enzi.

Kuhusu kuibuka kwa kauli zinazochochea mgawanyiko na kuchochea mvutano wa kidini kati ya Waislamu na Wakristo na baadhi ya viongozi Wakristo na Waislamu, hii ni matokeo ya fikra ya kikoloni ya ‘gawanya utawale.’

Ikumbukwe kwamba wakoloni, kwa kuendeleza kwa makusudi utawala wao katika koloni zao, huacha au kuunda mipasuko mbalimbali ya mgawanyiko kwa msingi wa kikabila, kikanda, kidini nk, mambo ya kuwatumia kwa urahisi kwa manufaa yao wenyewe inapohitajika.

Wito Wazi kwa Wote

Baada ya maelezo haya, tungependa kutoa wito wazi kwa umma mzima katika yafuatayo:

Kila mtu anapaswa kufahamu kwamba tatizo kubwa na la msingi duniani leo ni mfumo wa kibepari, ambao unatawala kila mahali, umeimarishwa na kuongozwa na dola kubwa. Hivyo, kubadilisha sura ya mtawala hakubadilishi chochote isipokuwa uchovu na upotevu wa rasilimali.

Kuna nchi nyingi zinazoendelea zinazotekeleza demokrasia ya vyama vingi, lakini rasilimali zao bado zinamilikiwa na mataifa ya Magharibi, raia bado wanapambana katika umaskini, na nchi zao zinabaki kuwa watumwa wa mataifa ya Magharibi. Kwa hivyo, suluhisho halisi si kuwa na mifumo ya vyama vingi, bali ni kung'oa mfumo wa kibepari kutoka kwenye uso wa ardhi.

Zaidi ya hayo, tunaonya baadhi ya taasisi, wafuasi, na viongozi wa dini miongoni mwa Waislamu na Wakristo wasianguke katika mtego wa wakoloni wanaotumia hisia za uchochezi na mvutano wa kidini kwa ajili ya siasa za kidemokrasia.

Inatarajiwa kwamba viongozi wa kidini wanapaswa kujitokeza kwa umma na masuluhisho yao ya kidini katika siasa, uchumi na jamii, badala ya kuchochea mzozo wa kidini kwa kudandia siasa za kidemokrasia, ambazo haziwahusu na zisizo na maadili ya kiroho.

Matumizi ya uchochezi wa kidini kwa ajili ya siasa za kisekula yana matokeo mabaya, majanga na hayaishii vizuri, kama ilivyoonekana huko Bosnia Herzegovina kuanzia 1992 hadi 1995, Afrika ya Kati mwaka 2013 kupitia magenge ya Anti Balaka na Seleka, na mwendelezo wa mizozo kama hiyo ndani ya Nigeria, Sudan, nk.

Natanguliza Asante.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.