Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  23 Jumada I 1447 Na: 1447 / 03
M.  Ijumaa, 14 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Demokrasia Haitukuzi Uhai Wala Mali

(Imetafsiriwa)

Kwa mara nyengine tena Tanzania imekumbwa na vurugu za baada ya uchaguzi kwa siku kadhaa kuanzia 29 Oktoba 2025 na kusababisha vifo vya watu wengi na uharibifu mkubwa kwa mali binafsi na miundombinu ya umma.

Tangu uchaguzi wa kwanza wa rais wa vyama vingi uliofanyika Tanzania mwaka wa 1995, kuibuka tena kwa vurugu za baada ya uchaguzi kumekuwa mfululizo na jambo lisilokwisha katika kila baada ya miaka mitano. Hata hivyo, vurugu za mwaka huu ni kubwa na zimeenea hata zaidi ya zile za kuhuzunisha za mwaka wa 2000 ambapo zaidi ya wafuasi 40 wa upinzani (CUF) huko Zanzibar (visiwa vyenye uhuru nusu) walipigwa risasi na kuuawa, zaidi ya 600 walijeruhiwa na inakadiriwa kuwa 2,000 walikimbilia nchi jirani ya Kenya.

Ghasia ndio asili ya demokrasia na chaguzi kuanzia kwenye msingi wake kama ifuatavyo:

1. Demokrasia ambayo ni mfumo tawala wa ubepari uliojengwa tu juu ya kipimo kimoja katika vitendo, ambacho ni ‘maslahi’. Yaani, mtu hutenda au kujizuia ili kupata maslahi. Haishangazi kwa mfuasi wa demokrasia iwe serikalini au upinzani kutenda au kuwashajiisha wengine kutenda kwa njia ambayo ingelinda maslahi. Kwa msingi wa kanuni hii, vyama vyote vya kidemokrasia havipo ili kuhudumia ustawi wa watu, lakini ni njia ya kiuchumi kwa wanasiasa, ima kwa kula ruzuku ambazo ni za umma, kutarajia uteuzi, kula misaada kutoka kwa wakoloni, kujihusisha na michango kutoka kwa wafadhili, nk.

2. Mfumo wa kidemokrasia unaunga mkono fikra ovu na ya kishetani ya Machiavelli, ambayo huhubiri: ‘Njia huhalalisha lengo, na lengo huhalalisha njia’. Hii ina maana kwamba katika demokrasia chochote kinaweza kufanywa, kama vile kuua, kuunda ugomvi kwa msingi wa hisia za kidini na rangi, kusema uongo au kitu chengine chochote bila kujali madhara yake, maadamu malengo yanayohitajika yatafikiwa. Kimsingi katika demokrasia hawana dhana ya halali au haramu, jambo muhimu ni chochote kinachopelekea kufikia malengo yao.

3. Demokrasia ya vyama vingi ilianzishwa na Magharibi kwa maslahi yao wenyewe, na si kwa maslahi wala maendeleo ya nchi zetu kama inavyoonekana na wengi kwa kiasi kwamba baadhi ya watu walichanganyikiwa na matumaini makubwa yaliyopotea, muda mwingi uliopotea, kutokwa na jasho jingi – hata kupoteza maisha wakitarajia mabadiliko. Badala yake ililetwa na magharibi kama njama na udanganyifu kwa kubadilisha sura ya utawala, walipogundua kuwa watu wamechoka na kulikuwa na ongezeko la kutoridhika kutokana na ukatili wa mfumo wa chama kimoja uliolindwa nao (Magharibi). Uliletwa kama chombo chengine cha kuimarisha ukoloni mamboleo kwa kuwavuruga watu wasione mambo kwa mtazamo wa kimfumo. Badala ya kupambana na mfumo muovu wa kibepari, hutumia nguvu zao katika suluhisho la uwongo la kubadilisha nyuso za watawala. Zaidi ya hayo, katika visa vingi mataifa ya magharibi kupitia hilo na visingizio vyengine huchochea mizozo ya kiraia na vurugu ili kurahisisha njia ya unyonyaji wa rasilimali zao. Mifano mizuri: Sudan, Congo, Yemen, Somalia, nk.

Ni dhahiri kwamba mfumo kama huo hauwezi kuepuka mizozo ya mara kwa mara, migogoro, na vurugu zisizokwisha, udhaifu, lakini zaidi ya yote unakabiliwa na kutoweza kuwatumikia wanadamu kwa uadilifu.

Wakati umefika kwa kila mtu mwenye bidii na uangavu anayetafuta mabadiliko halisi ya kimfumo kujiepusha kushiriki au kuunga mkono ukandamizaji fisadi wa kidemokrasia. Kwa Waislamu, ni faradhi kushikamana na njia sahihi ya Kiislamu ya mabadiliko kama ilivyofundishwa na Mtume (saw) ili kusimamisha tena Dola ya Khilafah, kuanzia katika ulimwengu wa Kiislamu.

Ama kwa wasiokuwa Waislamu, wakati umefika kwao kuchunguza mfumo badali wa Kiislamu na mwelekeo wake wa mabadiliko, kisha kuukumbatia na kujitenga na ufisadi na udanganyifu wa demokrasia.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.