Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  15 Muharram 1444 Na: 1444/02
M.  Jumamosi, 13 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pindi Serikali Inapotekeleza Unyanyasaji dhidi ya Wanawake
(Imetafsiriwa)

Wizara ya Wanawake, Familia na Wazee inazindua kampeni ya kinidhamu ambayo kwayo ilichagua kauli mbiu ya “Kupinga Unyanyasaji dhidi ya Wanawake” ambapo kupitia kwayo inapigia debe utekelezaji wa Sheria Msingi nambari 58 ya tarehe 11/8/2017, iwe ndio mdhamini pekee wa kuweka hatua za kutokomeza aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Wizara hiyo ya Wanawake inazingatia, kwa mtazamo dhahiri wa ajenda ya kijinsia, kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake unatokana na ubaguzi wa kijinsia, na inalenga kufikia usawa kamili baina ya jinsia, hata kama hili linapingana na hukmu za Uislamu kwa misingi kwamba zinagongana heshima kwa hadhi ya binadamu.

Sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Tunisia tunafanya kila juhudi kufichua sumu hizo ambazo serikali ya Tunisia imekuwa ikieneza miongoni mwa wanajamii, haswa wale wa wenye kutunga sheria, kwa sababu ya hatari yake kwa wanawake haswa na Familia ya Kiislamu na jamii kwa jumla. Maoni yetu ni kwamba unyanyasaji wanaopitia wanawake ni ule ambao serikali inawafanyia kupitia sheria mseto na mtindo wa maisha wa Kimagharibi ambayo inataka kuwalazimishia kwa nguvu. Ima kupitia kuweka sheria zilizotokana na mikataba ya kimataifa ya Kimagharibi kama vile CEDAW na Mkataba wa Istanbul, au kulazimisha fikra za Kimagharibi ambazo ni ngeni kwa imani yetu, kama vile ushoga, ukaaji uchi, uasherati na uzinzi, na mashambulizi dhidi ya ghariza ya kimaumbile ya mwanamke.

Katika kuendeleza unyanyasaji dhidi ya wanawake wa Kiislamu, utawala na taasisi zake zinataka kuwanyima uangalizi wa baba, kaka na waume zao kwa jina la usawa, uhuru kutoka kwa mamlaka ya baba au ya kiume, kupoteza kwao malezi bora, uhusiano mzuri na ulinzi, na kuwalazimisha kutoa nafaqa (masurufu) sawa na wanaume. Serikali pia haikukosa kutafuta kuwafukarisha na kuwanyonya kama vibarua nafuu kwa mitaji ya kimataifa na ya ndani kwa kisingizio cha kuwawezesha kiuchumi, ambapo ni unyanyasaji ule ule wa kiuchumi wanaouzungumzia! Mbali na kufuja haki zao kwa utajiri mkubwa unaomilikiwa na Tunisia na kuukabidhi ndani ya sahani ya dhahabu kwa makampuni ya uporaji ya Kimagharibi.

Baada ya unyanyasaji wote huu unaofanywa na serikali dhidi ya wanawake wa Kiislamu, inatuhutubia kuhusu kuwalinda kutokana na familia zao. Uhalisia ni kwamba sheria za mfumo huu na mtindo wa maisha unaoulazimisha ndio chanzo cha mizozo inayosambaratisha familia na kuwafanya wanawake kuwa wanyonge.

Tunaona kwamba kile wanachokiita sheria dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake si chochote ila ni kuwanyonya wanawake na kufanya biashara na masuala yao, ili kukidhi matamanio ya Magharibi, na kutabikisha makubaliano ambayo Tunisia imeyatia saini tangu enzi ya Bourguiba, katika muktadha wa kutaka kuunda jamii yenye kuonekana kuwa na itikadi kali inayozaa muundo wa kijamii wa Kimagharibi, pamoja na maradhi yake yote ya kijamii na kimaadili ambao ni ngeni kwa hadhara yetu ya Kiislamu ndani ya mfumo wa uvunjaji sheria ya Kiislamu iliyounganisha familia ya Kiislamu na kuhakikisha furaha yake na kufafanua majukumu ya wanaume pamoja na wanawake kama Mwenyezi Mungu alivyoumba na kutaka.

Hivyo basi, tunatoa wito kwa Waislamu katika ardhi ya Al-Zaytuonah kuzikataa sheria hizi, zinazoitishia familia ya Kiislamu, msingi wa jamii, nguzo yake na msingi wa mwamko wake, kwani zinalenga kuleta mizozo baina ya wanafamilia moja, ambayo kwayo Uislamu umeifanya msingi wa uhusiano wao mwema, mapenzi na huruma.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجاً لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ]

“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.” [Ar-Rum: 21].

Ustadha Hanan Al-Khamiri
Msemaji Rasmi wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.