Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 554
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Muungano kati ya Pakistan, Uturuki na Azerbaijan umekuwa ukichukua umbo kwa utaratibu uliopangwa, tangu viongozi wa nchi hizo tatu walipokutana kwenye mkutano wa kilele katika msimu wa kiangazi wa 2024. Mkutano huo uliwaleta pamoja Rais wa Uturuki Erdogan, Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, na Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev. Uliangazia mahusiano ya kisiasa kati ya dola hizo tatu, na kushughulikia masuala ya kikanda na kimataifa kama vile Gaza, Cyprus, Kashmir, na suala la chuki dhidi ya Uislamu.
Mnamo tarehe 16 Juni 2025, Mbunge wa Misri Diaa El-Din Dawood alipinga rasimu ya bajeti kuu ya mwaka wa fedha wa 2025/2026, akionyesha kuwa serikali inadai kupunguza deni la umma, wakati takwimu zinaonyesha kinyume chake. Alibainisha kuwa deni la ndani na nje limeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2018, na kufikia jumla ya pauni trilioni 11.5 za Misri mwezi Juni 2024. Alieleza kuwa mikataba iliyotangazwa na serikali haitafsiri matokeo yanayoonekana kwa wananchi, akikosoa kuendelea kwa matumizi ya sera hizo hizo za kiuchumi. Pia alieleza kuwa mapato ya deni na malipo ya awamu pekee katika bajeti mpya yanafikia karibu pauni bilioni 4,382.6 za Misri.
Maumbile ya mahusiano kati ya Uingereza na Urusi yamekuwa makali na yenye taharuki tangu karne ya 18, na uadui wa wazi na dhahiri kati yao. Kwa mfano, Dmitry Medvedev, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi, alisema mnamo Aprili 21, 2023, "Uingereza daima imekuwa, na sasa, na itakuwa adui yetu wa milele. Angalau hadi wakati ambapo kisiwa chao chenye majivuno kitazama ndani ya shimo la bahari kutokana na wimbi lililochochewa na mfumo wa kivita wa Urusi."
Huku kukiwa na mikutano tasa na makongamano ya uhadaifu, msafara maarufu unaojiita "Msafara wa Uthabiti" ulitoka Tunisia, Algeria, na Morocco, kuelekea Gaza kupitia Libya na Misri, kwa lengo la kuvunja mzingiro na kusaidia watu wa Ukanda wa Gaza, ambao wamekuwa chini ya vikwazo kwa zaidi ya miezi kumi na nane. Msafara huo uliwabeba wanaume na wanawake wa rika zote, waliounganishwa kwa lengo moja: kuvunja mzingiro huu uliowekwa na umbile la Kiyahudi kwa watu wa Gaza, kwa ushirika na ushiriki wa moja kwa moja wa tawala zilizo jirani, hasa unaoshikilia bendera kati yao utawala wa Misri.
Habari muhimu kwa uchambuzi kwa jumla ndio msingi wa tafakari ya kisiasa. Kwa hakika, ndio riziki ya kila siku ya wanasiasa. Bila hivyo, siasa haziwezi kueleweka, uchambuzi wa kisiasa hauwezi kuwepo, matukio hayawezi kutambuliwa, na madhumuni yake husalia kutojulikani.