Kongamano la Sharm El-Sheikh Ni Kutangaza Ushindi Juu ya Ummah, Kumakinisha Utiifu, na Kuimarisha Ukaliaji wa Kimabavu
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya Trump kutangaza ushindi yeye na mfuasi wake, umbile la Kiyahudi, walioupata katika hotuba yake mbele ya Knesset. Ushindi huu ulipatikana dhidi ya raia wasio na silaha, wakiwemo wanawake, watoto, na wazee, pamoja na miti na mawe, Muuaji wa Gaza alielekea kwenye kongamano hilo liliopangwa na kibaraka wake nchini Misri, Sisi, ambapo aliwaalika wale wote waliokula njama dhidi ya ardhi iliyobarikiwa.