Jumatano, 08 Sha'aban 1441 | 2020/04/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Dhoruba Inayokuja: Kutoka kwa Uingereza Katika EU

Uingereza imetoka rasmi katika Muungano wa Ulaya katika siku ya mwisho ya Januari lakini utokaji umezusha changamoto nyingine nyingi, ambazo zitaharakisha kuvunjika kwa Umoja wa Ulaya. Kwa sasa kuna kipindi cha mpito ambapo Uingereza na EU zitakuwa zikijadiliana mipangilio ya ziada, hata hivyo, masuala kadhaa yanajitokeza kuhusiana na mpango mpya wa biashara baina ya Uingereza na EU.

Soma zaidi...

Mbinu ya Amerika na Kupunguza Kisiasa Wanajeshi ndani ya Afghanistan

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amesema katika jukwaa la kiulimwengu la kiuchumi lililofanyoka Davos, kwamba serikali ya Afghan haitapata matatizo baada ya vikosi vya kigeni kujiondoa kutoka nchini humo; hata hivyo, kama mazungumzo yataendelea na Taliban badala ya serikali yake, vita vitachukua awamu nyingine.

Soma zaidi...

Kwa Nini Xinjiang ni Muhimu kwa Uchina

Ukandamizaji wa Uchina wa kupita mipaka dhidi ya Waislamu haujawahi kushuhudiwa duniani kote. Mwaka uliopita umeshuhudia matukio ya ripoti na video zikionesha Waislamu wa Uyghur wakijazwa ndani ya kambi zilizotapakaa ndani ya magharibi ya Uchina. Huku shinikizo zikizidi kutoka katika vyombo vya habari vya Magharibi, ambavyo vina ajenda yao, sasa utawala wa Uchina umekubali kuwa inatekeleza unyama huo: kisiwa cha kambi kimejengwa. Shirika la habari linaloendeshwa na serikali ya Uchina la Xinhua siku ya Jumamosi 13 Oktoba 2018 lilimnukuu afisaa rasmi kuwa lazima dini zipitie "mchakato wa kuzifanya mujtamaa zisizokuwa za Kichina kuwa chini ya athari ya thaqafa ya Kichina."

Soma zaidi...

Ziara ya Haraka ya Trump ya Ulaya, Uingereza na Urusi

Ziara ya haraka ya Trump ya Ulaya, Uingereza na Urusi imeuacha ulimwengu ukishangaa ikiwa Amerika iko makini kuhifadhi mfumo wa uhuru ulioko kwa sasa. Trump kumsifu Merkel kuwa mateka wa Urusi na kushutumu wazi wazi mipango ya May ya kuiondoa Uingereza katika Muungano wa Ulaya (Brexit) inaashiria zaidi ya sintofahamu nyepesi katika kitovu cha muungano wa nchi zilizopakana na bahari ya Atlantiki. Kuongeza chumvi kwenye kidonda, Trump alisonga mbele na kuuita Muungano wa Ulaya adui huku akitarajia mkutano usiokuwa wa kawaida wa kirafiki na Putin mjini Helsinki.

Soma zaidi...

Nigeria Yakabiliana na Mustakbali Usiothabiti

Tangu uhuru mwaka wa 1960, historia ya kisiasa ya Nigeria imekuwa ya kuzongwa na matatizo kadhaa - vita vya kikabila, vita vya kidini, vita vya mafuta, mapinduzi ya kijeshi nk. Takribani asilimia 75 ya miaka baada ya uhuru ilitumiwa chini ya utawala wa kijeshi na udikteta. Hata hivyo, ghasia za Nigeria hazijawahi kufikia kiwango cha wenzao wa Afrika kama Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu