Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  11 Muharram 1442 Na: Afg. 1442 H / 01
M.  Jumapili, 30 Agosti 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wafuasi wa Machiavelli Hawawezi Kuondoa Ufisadi
(Imetafsiriwa)

Serikali ya Afghanistan imewaelekeza maafisa kadhaa wa serikali, wakiwemo mawaziri, manaibu, magavana na washauri, kwa afisi ya Mkuu wa Sheria kwa tuhuma za ufisadi. Pia iliwakamata maafisa wengine wa zamani ambao walitiwa hatiani kwa uhalifu anuwai.

Maswala mawili yafuatayo ni muhimu sana na yanapaswa kuzingatiwa kuhusu hali kuu ya ujanja kama huu:

Kwanza, katika mfumo wa kirasilimali, msingi wa taratibu na sera unategemea faida na manufaa. Kwa hivyo, mizani inaonekana wazi kati ya watu binafsi na dola ambazo zinatawalisha mfumo huu fisidifu. Katika serikali kama hizo, rais, wasaidizi wake wa karibu na taasisi za serikali binafsi ni wafuasi wa Machiavelli, anayejulikana kama baba wa siasa katika nidhamu ya kijamhuri. Ili kuakisi maoni yake ya kisiasa, Machiavelli anatolea mfano wa mtawala aliyewauwa watu kadhaa mikononi mwa majenerali wake, na hivyo kuwaondoa kutoka kwake. Kisha mtawala huyo anageuka, lakini wakati watu wanapokosoa kitendo cha kikatili cha majenerali, mtawala huyo hukata vichwa vya majenerali wake. Kwa maoni ya Machiavelli, mtawala huyu aliyetajwa hapo ndiye mwanasiasa bora kwa sababu kwa upande mmoja, aliwanyonya majenerali wake, na kwa upande mwingine aliiweka mbali nafsi yake kwa kuwaua, na akajitambulisha kama mtu maarufu na mpiganaji wa ufisadi baina ya watu.

Watawala wa Afghanistan wanafuata sera hiyo hiyo ili kulinda mamlaka yao ya kisiasa na maslahi ya kibinafsi. Kwa upande mmoja, wanaweka njia ya ufisadi kwa kuteua wasaidizi wao wafisadi kwenye nyadhifa kuu za serikali; Kwa upande mwingine, muda mfupi baadaye, wanawatuhumu watu hawa kwa ufisadi, na kujionyesha kama viongozi wa kupambana na ufisadi. Kwa kweli, wamejifunza jinsi ya kutumia siasa za watu wengi na za mkumbo kuficha ufisadi wao, na hata kuchafua taswira ya jamii.

Pili: Watawala wa nchi za Kiislamu, pamoja na Afghanistan, wanajiona wana deni kwa wale ambao wamewaunga mkono kila wakati kuchukua madaraka. Kwa kweli, wao ni vibaraka na watafanya chochote kuiridhisha Amerika na NATO. Kwa kweli, watawala wa Afghanistan wamepanga kuwasilisha ripoti juu ya matendo yao kwa mabwana zao kwenye kongamano la Geneva utakaofanyika mwishoni mwa mwaka wa 2020; Kwa hivyo, walianza hatua za kupambana na ufisadi ili kuwa na kitu cha kuwasilisha kwenye kongamano hilo na pia kuvutia ridhaa ya mabwana zao wa Magharibi.

Watu wa Kiislamu wa Afghanistan hawapaswi kudanganywa na vitendo kama hivyo, na lazima watambue kuwa vitendo hivyo vya kujifanya havitamaliza ufisadi kwa mizizi yake. Ufisadi sio tu ni jina la pili la jamhuri na demokrasia pekee, bali pia ni kiini cha msingi wa mfumo uliopo. Suluhisho ni kubadilisha mfumo. Ni Uislam pekee unaoweza kuchukua nafasi ya tawala hizi fisadi na dhalimu. Uislamu ni lazima utekelezwe kwa njia kamili ya kimapinduzi kupitia dola ya Khilafah, ili mifumo, viwango na kanuni hizi ziondolewe kutoka kwa uso wa dunia, pindi uadilifu wa Uislamu itakapo chukua nafasi ya ufisadi wa Urasilimali.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu