Alhamisi, 14 Safar 1442 | 2020/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  9 Rabi' I 1441 Na: 1441 H / 005
M.  Jumatano, 06 Novemba 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Majaribio ya Kukata Tamaa ya Kuwabandikiza Mukhlisina na Fikra zao kuwa ni Misimamo Mikali na Ugaidi hakutawazuia wao kufanya Kazi na haitakuwa ni Kizuizi baina yao na Watu
(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Fajr liliripoti mnamo Jumamosi, 2/11/2019, kile ilichokiita kuwa janga; uwepo wa tovuti 10 kubwa duniani chini ya udhibiti wa Qatar na Uturuki. Ilitaja taarifa iliyotolewa na Abdulghani Alhindi, mwanachama wa Chuo cha Utafiti wa Kiislamu kwamba watu wenye misimamo mikali wanaopigia debe ugaidi na ambao wanatoa fatwa wamejumuishwa katika orodha ya watu waliozindua fatwa: miongoni mwao ni Yousuf al-Makharza, Ahmad al-Qasas na Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut Tahrir pasina na kutuonyesha aina au mada za fatwa ambazo watu hawa wametoa na ni kipi kilichomo ndani ya fatwa zao kuwa ni “misimamo mikali na ugaidi”!


Inajulikana pakubwa kwamba kila shutuma ambazo haziambatanishwi na ushahidi au uthibitisho ni urongo na hatuko hapa kumtetea Amiri (kiongozi) wetu na wanachama wetu. Wako juu ya kiwango cha kushukiwa; Hizb ut Tahrir haifuati vitendo vya kutumia nguvu kama njia ya kusimamisha dola. Lakini inajifunga na njia ya Mtume (saw), inapambana na Magharibi, fikra zake katika mapambano ya kifikra na Magharibi inajua wazi kwamba katika ulingo huu wa vita vya kifikra haina nafasi na haiwezi kupambana na Hizb ut Tahrir. Na hata taasisi zake zimeelezea kuwa chama ndio mpiganaji mkuu katika vita vya kifikra. Amerika inafahamu nguvu na ukubwa wa fikra za chama. Na inafahamu kwamba chama kinakwenda juu zaidi ya kuta ilizoziweka kama kizuizi ili kulinda mfumo wa kirasilimali. Hii ndiyo iliyopelekea Magharibi kufanya majaribio ya kukata tamaa ili kuharibu sura ya Hizb ut Tahrir, kushambulia fikra zake na kubuni majeshi ya kifikra yaliyovutiwa na thaqafa yake.


Hata kutoka kwa wanaolingania Uislamu wako wale ambao wako katika upinzani ili kujaribu kupambana na chama na fikra zake na kuharibu sura ya watu wake, wabebaji Da’wah mukhlisina. Licha ya kwamba inajulikana kwamba Hizb ut Tahrir haijiwasilishi kama chama cha fatwa kwa Ummah, na hakitoi fatwa kamwe kwa kuwa chama sio Nyumba ya Fatwa kama tulivyosema. Majaribu yenu yanayoendelea ili kukishtumu chama na Amiri (viongozi) wake na wanachama kwa “ugaidi” hakutatuzuia sisi kutoendelea na kufanyakazi ya kurudisha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo Magharibi inaiogopa kwa kuwa inaihisi inakaribia. Majukumu ya majeshi yenu na zana nyinginezo zipo tu kusimama dhidi yake na kuwa kizuizi baina yake na watu ili kuwazuia watu kutoiunga mkono na kuinusuru.
Kinachobeba Hizb ut Tahrir ni fikra safi na iliyokita ya Uislamu, ambayo inapatikana katika vitabu vyote vya Kiislamu vya kisharia, Hadith, Seerah, simulizi na nyinginezo hata kutoka kwa wale munaosoma kwao ndani ya Al-Azhar. Muasisi wa chama na Amiri wa kwanza, Sheikh Taqi ud-Din An-Nabhani (rahimahu Allah) alihitimu kutoka Al-Azhar na alikuwa mmoja wa wanachuoni wake wakubwa. Vitabu ambavyo chama inajifunga navyo, vinaonyesha njia na fikra zake ambazo ni ushahidi kwake na kwenu. Vyote viko na viliwahi kuwasilishwa na utawala kwa kamati ya Al-Azhar katika kipindi cha kesi za baadhi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir mnamo 2002/2003. Uamuzi wa Kamati ni kwamba haviendi kinyume na Shariah ya Kiislamu. Na kwamba havina tatizo na hakuna madhara katika usambazaji wake, hili liliripotiwa rasmi na katika magazeti ya kimataifa, yakijumuisha Jarida la Misri la Al Gomhuria na gazeti la kimataifa la Al-Hayat mwishoni mwa Machi 2003.


Kinachotia wasiwasi Magharibi kuhusiana na ulinganizi wa Hizb ut Tahrir na kuifanya ni adui wake wa kwanza ni kwamba chama kinatafuta ukombozi wa Ummah kutoka katika fikra za Magharibi na kuwa huru kutokana na utumwa wake na kung’oa nidhamu yake ya kirasilimali ambayo inaiwezesha kudhibiti utajiri wa Ummah na rasilimali zake. Kile ambacho Magharibi na zana zake zinaogopa zaidi ni kwamba watu wataitikia fikra na kupenya katika macho yaliyowazi na mioyo tambuzi ya watoto mukhlisina wa Ummah ndani ya majeshi, na itakuwa ndio nusra yao waliyokuwa wakiitafuta na kuinusuru kama walivyofanya mababu zao ili kusimamisha dola iliyoogopwa na Magharibi. Dola ambayo itasitisha utegemezi wa nchi zetu na nidhamu za serikali kwa fikra na sera za Magharibi; na kusitisha usambazaji wa uporaji wa hazina za utajiri wa nchi zetu na kurudi ardhini mwao wakiwa wamekata tamaa lau kama bado watakuwa na ardhi.
Enyi Wanachuoni Wakubwa, Masheikh na Wakuu! Fikra hizi zinatokana na Uislamu, Dini yenu munayoiamini. Musiwe zana za utendaji katika mikono ya Magharibi na mishale inayofuma Dini yenu na wabebaji Da’wah. Jukumu lenu ni kuwanusuru na kubeba majukumu pamoja nao na kuwachochea vijana wa Misri kwa ujumla ili kukumbatia fikra zao mpaka pale Mwenyezi Mungu amri yake itakapotimia na Yeye (swt) hupeleka ushindi wake kwa Dini Yake na kuinyanyua Dola Yake.


Enyi Watu wa Misri (Kinana), Watu na Jeshi! Hizb ut Tahrir ni moja katika nyinyi, kiongozi ambaye hakudanganya na hatowadanganya, na ni mshauri wenu muaminifu anayefanyakazi pamoja nanyi ya kurudisha dola ambayo iliwapa utukufu na kutawala duniani kwa uadilifu wa Uislamu kwa zaidi ya karne kumi na tatu. Kwa shikaneni mikono pamoja nao na simamisheni pamoja nao dola ambayo itarudisha uadilifu wa Uislamu katika ardhi; ambayo katika kivuli chake miti, ndege, mawe na sio tu wanadamu watafurahia baraka zake nanyi mutapata utukufu katika dunia hii na hadhi Akhera. Ewe Mwenyezi Mungu, ilete karibu na tufanye sisi kuwa ni wanajeshi wake na mashahidi wake na ifanye Misri kuwa mji kuu wake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ] “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir


Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu