Jumamosi, 13 Dhu al-Qi'dah 1441 | 2020/07/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Majibu kwa Uzushi wa Dar al-Ifta ya Misri

Uislamu umelitambua jambo la ijtihad, ambapo Mujtahid anatia juhudi yake kuvua hukumu ya kifiqhi ya kivitendo kutoka kwa dalili zake fafanuzi katika machimbuko ya sheria na kuipachika juu ya uhalisia wa mada (Manat) ya hukumu hiyo. Ni dhahiri, Ijtihad haifanywi katika mambo yaliokatikiwa (Qati’), bali katika mambo yasio na mkato (Dhanni), na hivyo basi Mujtahid hupokea ujira mara mbili anapofanya Ijtihad na akapata, na hupokea ujira mmoja endapo atakosea katika Ijtihad hiyo. Ijtihad haikufungwa kwa mtu au chama, bali ni kwa wale wote walio na uwezo wa kufanya Ijtihad.

Soma zaidi...

Uzushi wa Gazeti la Al-Sharq Al-Awsat Dhidi ya Hizb ut Tahrir

Gazeti hili haliku nukuu tu pekee Taarifa ya Afisi ya Hudumu ya Usalama ya Kifederali ya Urusi (FSB) juu ya ukamatwaji wa mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika eneo la Waislamu la Tatarstan, (katika toleo lake Na. 14563, Ijumaa 2/Safar 1440H – 12/Oktoba 2018M), bali liliongeza tuhuma zaidi dhidi ya chama hiki, na kuchapisha uzushi kuwa “kinatumia vitendo vya kigaidi kufikia lengo lake”, likiongeza, “Ni wazi kuwa Hizb ut Tahrir mbali na juhudi zake za kusajili Waislamu zaidi nchini Urusi na kuandaa halaqaat zilizounganishwa na miundo ya ngazi za uongozi, imekuwa ikiyasaidia mashirika na makundi haramu ya kigaidi eneo la Mashariki ya Kati kwa watu wenye kujitolea muhanga baada ya kuwakinaisha kutekeleza vitendo vya kigaidi”.

Soma zaidi...

Raisi wa Mauritania Anajiunga na Vita vya Msalaba Kuupiga Vita Uislamu

Inajulikana kuwa mwanajeshi Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye hakupokea shahada ya “Bakaloriasi” ya shule ya upili lakini “waundaji wake” walimsaidia na kumfanya apate usajili katika chuo cha kijeshi, licha ya yeye kuhitimu na elimu ya wastani shuleni, alimpindua, katika mapinduzi ya kijeshi ya mnamo 6 Agosti 2008, raisi wa kwanza aliye chaguliwa nchini Mauritania (Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallah), baada ya Sidi kutoa uamuzi wa uraisi wa kumuondoa yeye kutoka katika uongozi wa walinzi wa raisi. Na ingawa Ould Cheikh alikuwa amempandisha madaraka ya cheo cha Jenerali, cheo kikubwa zaidi ya vyeo vya jeshi la Mauritania, na kumteua kushikilia wadhifa wa mkuu wa majeshi ya Raisi wa Jamhuri, lakini kiu ya mamlaka na utawala juu ya nchi hiyo na watu wake ilimsukuma kumng’oa Ould Cheikh. 

Soma zaidi...

Nyuma ya Shambulizi la Bomu la Nuklia Jijini Nagasaki Magharibi ni Adui wa Waislamu na Wanadamu

Mnamo 9/8/2018, Japan iliadhimisha miaka 73 ya waathiriwa wa bomu la atomiki lililoangushwa na Amerika juu ya Nagasaki wakati wa siku za mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Takriban watu 74,000 walifariki kutokana na athari ya bomu hilo, huku bomu lililolipiga jiji la Hiroshima mnamo 6/8/1945 likisababisha vifo vya watu 140,000 ambao walikadiriwa na Kanali wa Amerika Cunningham kuwa shabaha halali.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu