Ijumaa, 10 Safar 1443 | 2021/09/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  22 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 1441 H / 032
M.  Jumatano, 12 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kina Mama Wanauwawa… Watoto Wanafanywa Mayatima… Na Serikali Zilizojisalimisha na Kujidhalilisha!!
(Imetafsiriwa)

Mwanamke mmoja wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 23 aliuwawa shahidi na risasi za majeshi ya uvamizi ya Kizayuni wakati wa ghasia katika mji wa Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi katika Ardhi Iliyo Barikiwa – Palestina, baada ya kupigwa na risasi alfajiri zilizopenya katika nyumba ya familia yake…

Umbile la Kiyahudi linaendela kwa kiburi chake, maonevu, na umwagaji wake wa damu tukufu ya watu wasio na hatia ambao hawajafanya uhalifu wowote; bila ya uwajibikaji wowote wala kuhesabiwa… mwathiriwa mpya zaidi wala hatakuwa wa mwisho (wa waathiriwa wake) ni mama mchanga aliyeamka alfajiri kumtayarishia mmoja wa watoto wake wawili wadogo maziwa, ambaye alimuogopea gesi ya kutoa machozi, hivyo akaenda kufunga dirisha. Mmoja wa wanajeshi hao katili akampiga risasi moja kwa moja kifuani mwake. Hawakutosheka na hili bali pia wakaizuia ambulensi kutomfikia kumuokoa.

Ni upi uhalifu na kosa lililofanywa na mwanamke huyu?! Alikuwa tu anataka kuwalinda watoto wake na 'akalipwa' kwa kuuwawa kinyama. Tukio hili na matukio mengine yote (yametokea), na hatujasikia sauti ya kulaani yaliyojiri, si kwa utawala wa Dayton wala kwa wengine… utawala wa Dayton umeshughulishwa na kukusanya kodi na sio kuchunga watu; hatua zake zinaongezea uzito juu ya watu katika mateso yao. Serikali vikaragosi katika nchi za Waislamu zimezama ndani ya udhalilifu na utumwa. Hili limesababisha umbile la Kiyahudi kuzurura kwa uhuru na furaha katika Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina, ikiuwa watu wake, na kuchafua matukufu yake. Utukufu wa Msikiti wa Al-Aqsa unakiukwa kila leo, na wanajeshi katili wa kikafiri wa umbile la Kiyahudi na makundi ya walowezi wao, huku umbile la Kiyahudi likiweka vikwazo vikali juu ya kuingia kwa Waislamu (katika msikiti huo). Sasa inasonga mbele kuupa Msikiti wa Ibrahimi mjini Al-Khalil kitambulisho cha Kiyahudi, huku ikiwakataza watu wake kuingia humo, hivyo hakuna adhan inayosikika wala swala inayo swaliwa humo.

Ni upi uhalifu uliofanywa na watoto wake wawili? Mkubwa kati yao ana umri wa miaka mitatu pekee. Alikuwa akimuita mamake lakini hakusikia na hakujibu wito wake?! Na mtoto huyo angali anasubiri maziwa?! Hatujasikia sauti za watetezi wa haki za wanawake, watoto na familia, na hatujawaona wakilaani dhidi ya uhalifu huu. Pia hatujawaona wakipinga dhidi ya uhalifu huu kama vile wanavyopinga dhidi ya sheria za Uislamu chini ya kisingizio cha uhuru na misimamo yao kwa haki za wanawake na watoto!! 

Ni haki, serikali na watawala duni walioje hawa? Mko wapi Enyi majeshi ya Waislamu kumlipizia kisasi mama huyu na waathiriwa wengine wa Mayahudi na serikali za kitumwa? Je, wakati haujawadia kwa damu inayochemka katika mishipa yenu kwa uhalifu unaofanywa dhidi yetu, na udhalilifu na utumwa tunaoishi ndani yake?! Kumbukeni ayah hii tukufu:

 (وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ * بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَت)

“Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa * Kwa kosa gani aliuliwa?” [At-Takwir: 8-9]

Wameyazika matarajio yake, ndoto, furaha na usalama wake, na ni Imam pekee ndiye anayemhami shahidi kama huyu na watoto wake watamuokoa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kuileta Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume. La Hawla Wa La Quwata Ila Billah, hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu