Jumapili, 04 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  13 Rajab 1445 Na: 1445 H / 03
M.  Alhamisi, 25 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Unafiki wa Mashirika ya Kimataifa na Ukandamizaji wa Serikali
(Imetafsiriwa)

Katika wiki moja iliyopita, waandishi wa habari 11 wamekamatwa nchini Kyrgyzstan, na mashtaka ya jinai yameletwa dhidi ya wakuu wa baadhi ya majukwaa ya mtandaoni. Kwa sababu hii, mashirika ya kimataifa na nchi za Magharibi zimetoa maombi ya mara kwa mara kwa mamlaka ya Kyrgyz. Kwa mfano, uwakilishi wa Muungano wa Ulaya nchini Kyrgyzstan na balozi za Uingereza, Austria, Ubelgiji, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Latvia, Lithuania, Uholanzi, Ureno, Uhispania na Uswidi kwa pamoja zilitoa taarifa mnamo Januari 19 wakieleza wasiwasi wao kuhusu kukamatwa kwa waandishi wa habari nchini Kyrgyzstan. Katika taarifa hiyo ya pamoja, wameitaka serikali ya Kyrgyzstan kutimiza ahadi za kimataifa kuhusu haki za binadamu, kulinda haki za waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari, na kufanya uchunguzi ndani ya mfumo wa kisheria kwa kushirikisha mawakili.

Mamlaka za Marekani pia zimeelezea wasiwasi wao kuhusu kukamatwa kwa waandishi wa habari. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, alitoa taarifa ifuatayo mnamo Januari 18 kuhusu hali ya Kyrgyzstan: “Marekani inasikitishwa sana na ripoti za hatua za hivi majuzi zilizochukuliwa na serikali ya Jamhuri ya Kyrgyzstan dhidi ya vyombo huru vya habari na waandishi wa habari. Vitendo hivi vinachangia muundo wa shughuli za serikali unaoonekana kulenga kuzima mijadala ya umma na uhuru wa kujieleza. Tunahimiza mamlaka ya Kyrgyzstan kuhakikisha wanahabari wanaweza kufanya kazi bila shinikizo au unyanyasaji usiofaa. Vyombo huru vya habari ni muhimu kwa ajili ya kulinda haki za binadamu, kudumisha taasisi zenye ufanisi za kidemokrasia, na kukuza amani na usalama.”

Taasisi ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari (IPI), yenye makao yake makuu jijini Vienna, Austria, ilitoa wito wa kuachiliwa huru mara moja kwa waandishi hao 11 mnamo Januari 17. Zaidi ya hayo, shirika la Amnesty International lilitoa taarifa likisema kwamba “serikali ya Kyrgyzstan lazima iache kuwashinikiza raia walio na fikra tofauti, iwaachilie huru waandishi wa habari waliozuiliwa, na kuwaachilia huru wale waliofungwa kwa kueleza maoni yao.”

Siku hiyo hiyo, kura ilipigwa juu ya azimio kuhusiana na Asia ya Kati na kupitishwa katika Bunge la Ulaya huko Strasbourg. Azimio hilo liliungwa mkono na wabunge 543 kati ya 629 wa bunge hilo. Azimio hilo linasema kwamba “tawala za kimabavu zilizo madarakani katika Asia ya Kati lazima ziheshimu ahadi zao za kimataifa katika uwanja wa haki za binadamu.”

Rais Sadyr Japarov alisema katika mahojiano na shirika la Khabar kwamba waandishi hao walikamatwa kwa tuhuma za “kuitisha machafuko jumla.” Kulingana naye, wanahabari wa kujitegemea na wanablogu hutumia fedha zinazopokelewa kutoka kwa taasisi na mashirika mbalimbali kwa malengo tofauti. Alisema, “Kwa ujumla, mashirika ya habari kama kloop.media, Mediahab, kaktus.media, PolitKlinika, factcheck.kg, na T-Media hupokea zaidi ya $600,000 Dolari kila mwaka kama ruzuku kutoka kwa wafadhili wa kigeni. Fedha hizi za ruzuku zinakusudiwa kwa uhuru wa kujieleza, kusaidia jumuiya ya wanahabari, na miradi ya maendeleo ya uandishi huru wa habari. Hata hivyo, kiuhalisia fedha za ruzuku zinatumika katika sera ya kushutumu na kukashifu serikali, kuvuruga amani ya umma, kuwasilisha rufaa kinyume na katiba na kueneza taarifa za uongo zinazotishia usalama wa taifa.”

Je, rufaa za mashirika haya ya kimataifa zinahusiana kikweli na kukamatwa kwa waandishi wa habari na ukiukaji wa haki za binadamu, hasa uhuru wa kujieleza? Au kuna maslahi mengine nyuma ya rufaa zao? Au ni hatua ya kuanzisha utawala wa kidikteta nchini?

Inafahamika kuwa tangu serikali ya sasa iingie madarakani, imefungua mashtaka ya jinai dhidi ya mamia ya Waislamu kwa kutoa maoni yao au kusambaza habari za kidini kwenye mitandao ya kijamii. Hadi leo hii, makumi ya ndugu na dada zetu wenye mafungamano na Hizb ut Tahrir wanaendelea kuzuiliwa gerezani kwa mashtaka ya msimamo mkali, wakikabiliwa na hali ngumu, ikwemo mateso makali na yasiyo ya kawaida, kupigwa, kupigwa shoti za umeme, na kufungiwa peke yao katika vyumba vilivyofungwa. Hata hivyo, mashirika ya kimataifa yaliyotajwa na nchi za Magharibi hayajatamka neno lolote kuhusu vitendo hivyo dhidi ya Waislamu, achilia mbali kuibua wasiwasi kuhusu “uhuru wa kujieleza” na “haki za binadamu.

Kwa hakika, Waislamu wenye ikhlasi wanapotuhumiwa kuwa na msimamo mkali na kukabiliwa na adhabu kali, “masekula” hao hupiga makofi na kushangilia. Inafurahisha kuona kwamba mashirika haya yalianza kuzua mabishano tu baada ya wapinzani wa serikali kufungwa chini ya lebo za “itikadi kali” na “dhidi ya mfumo wa serikali.” Kwa hivyo, kauli mbiu za “uhuru wa kujieleza” na “haki za binadamu” si lolote bali ni mbinu za kinafiki zinazotumiwa na nchi za Magharibi na jumuiya za kimataifa kufikia malengo yao. Hii inaashiria kuwa makafiri wakoloni wanashindwa katika mapambano ya kimfumo dhidi ya Uislamu na watetezi wake.

Katika uhalisia, inajulikana pia kwamba “uhuru wa kujieleza” unaopigiwa upatu na nchi za Magharibi unapingana kabisa na Uislamu. Kwa sababu uhuru wa kujieleza hauishii tu katika kuwakosoa wanasiasa; kinyume chake, unajumuisha msemo wa kikafiri, kukuza mitazamo kinyume na imani ya Kiislamu, kuunga mkono riba na uzinzi, pamoja na kuonyesha aina mbalimbali za uasherati kupitia vipindi vya televisheni na mengineyo. Tumeshuhudia haya kwa uwazi katika matukio yasiyo ya kimaadili kama vile uchapishaji wa picha za utovu wa heshima za Mtume Muhammad (saw) na kudhalilishwa kwa Quran Tukufu. Kwa hiyo, uhuru wa kujieleza kwa makafiri unatumika tu linapokuja suala la kupiga vita Uislamu.

Vile vile kuwahisabu watawala katika Uislamu sio suala la uhuru wa kujieleza; bali inaangukia kwenye fahamu ya “kuamrisha mema na kukataza maovu,” ambayo ni wajibu juu ya Waislamu. Ikiwa kuwahisabu watawala kungekuwa ni sehemu ya uhuru wa kujieleza, basi “kuamrisha mema na kukataza maovu” kungeruhusiwa kwa Waislamu. Hata hivyo, Mtume Muhammad (saw) amesema: «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَفَلِعْ فَفْسْتَفَ فِي َدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِمْ فَفْسِفَ فَعَلَى تَعْمِينَ فَعَلَى يَسْتَطِعْ فَبِلِي. عْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ» “Mwenye kuona uovu miongoni mwenu, na aubadilishe kwa mkono wake; na ikiwa hawezi, basi [abadilishe] kwa ulimi wake; na ikiwa hawezi kufanya hivyo, basi kwa moyo wake - na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi.” [Muslim]

Na Hadith hii inajumuisha kuwahisabu watawala vilevile.

Hatuna nia kwa maneno haya ya kutetea au kuhalalisha ukandamizaji wa serikali ya sasa katika harakati za kuanzisha udikteta. Badala yake, tunataka kusisitiza unafiki wa nchi za Magharibi katika kukuza na kutekeleza maadili ya kidemokrasia. Kuwatuhumu Waislamu na waandishi wa habari kwa itikadi kali, na kukamatwa kwao baadaye, si chochote ila ukandamizaji na jaribio la kudumisha udhibiti. Hatimaye, serikali ya Kyrgyzstan imetumikia Urusi kwa uaminifu tangu miaka ya uhuru, ingawa sasa mara kwa mara inajaribu kuanzisha mahusiano na Magharibi na kujiweka mbali na Urusi. Majaribio ya awali ya mamlaka ya kuanzisha udikteta yamefeli, na serikali ya sasa ya Rais Sadyr Japarov inashikilia msimamo wa tahadhari katika uhusiano wake na Magharibi, unaoonekana katika kufungia mikataba ya kimkakati. Sera ya mambo ya nje ya serikali ya sasa inaelekezwa kwa China, ikiashiria kuhama kutoka Magharibi. Kwa hivyo, inajitahidi kuweka udhibiti wa kidikteta, na kusababisha kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusiana na Magharibi.

Kwa ajili ya kuanzishwa kwa udikteta, ni muhimu kwanza kuhodhi habari, mchakato unaotekelezwa katika tawala za kimataifa na hatua za kihistoria za mifumo anuwai. Kyrgyzstan, hata hivyo, imejitambulisha kama “Kisiwa cha Kidemokrasia” miongoni mwa dola za kiimla katika Jumuiya ya Madola Huru, ikipata mikopo yenye thamani ya mamilioni ya dolari kutoka nchi za Magharibi na mashirika ya kimataifa. Kwa hiyo, mashirika ya kimataifa yanatoa wito kwa mamlaka za Kyrgyz kushikamana na maadili na makubaliano ya kimataifa. Zaidi ya hayo, athari za kithaqafa kwa serikali ya kidikteta nchini Kyrgyzstan ni ndogo, na kuunda rai jumla katika mwelekeo huu kunahitaji muda mwingi.

Kwa kumalizia, jamii ya Kyrgyzstan lazima ipinge majaribio ya serikali ya kuanzisha udikteta na kuimarisha ujasiri wa watu wake dhidi ya ukandamizaji. Wakati huo huo, tusidanganywe na sera haribifu na za kinafiki za nchi za Magharibi. Badala yake, tunapaswa kusoma thaqafa ya Kiislamu na kutumia uwezo wetu kuiinua hadi viwango vya juu zaidi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu