Jumatatu, 04 Safar 1442 | 2020/09/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  12 Muharram 1442 Na: 06 / 1442
M.  Jumatatu, 31 Agosti 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Bajwa-Imran Inafanya Kazi kama Mwendeshaji Mteule wa Mazungumzo ya Ndani ya Afghanistan ili Kudhamini Ushindi wa Trump katika Uchaguzi

Ili kuhakikisha ushindi wa Trump katika uchaguzi, Imarati kwanza na bila aibu ilisawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, na serikali ya Bajwa / Imran sasa inafanya kazi kuhakikisha kuwa upinzani wa Afghanistan unashirikiana na serikali ya kibaraka wa Amerika nchini Afghanistan. Utawala wa Pakistani hutumia sera ya karoti na kijiti kuwa kati na kati katika njama hiyo, kwa kuweka vikwazo vipya vya kifedha dhidi ya wanachama wengine wa uongozi wa Taliban. Wakati huo huo, mkuu wa wajadilianaji wa Taliban, Mullah Abdul-Ghani Baradar Akhund, alialikwa Islamabad, na baada ya hapo Imran Khan alimtaka Abdullah Abdullah, ambaye ndiye mwenyekiti wa Baraza Kuu la Upatanishi wa Kitaifa, kusaidia kuanza tena kwa mazungumzo, baada ya miezi kadhaa kuyumba chini ya mwamvuli wa Amerika. Kwa hivyo, serikali ya Bajwa / Imran inataka kufanya mazungumzo kati ya Waafghan, ili damu ya mashahidi katika vita vya miongo kadhaa iuzwe na kusalitiwa ili Trump ashinde Novemba ijayo, katika upande wa kuhakikisha makubaliano ya amani ya Afghanistan ambayo yanahesabiwa kwake katika kampeni za uchaguzi.

Mujahideen waaminifu wa Afghanistan hawajazitoa roho zao na mali zao kafara kwa zaidi ya miongo minne ili kuachana na lengo lao nzuri la kusimamisha dola ya Kiisilamu, ili kugawanya mamlaka pamoja na vibaraka wa Amerika. Kuachana na hukmu za kisheria kwa kupendelea kutawala kwa sheria ya kisekula ya kiliberali chini ya pazia la Uislamu inamaanisha kukubali nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali inayotegemea riba na sarafu ya karatasi inayotegemea dolari, korti za kisekula pamoja na adhabu kadhaa za Kiislamu kuficha ufisadi wao wa kibinadamu, na nidhamu ya utawala ambayo Waislamu wenye ikhlasi nchini Afghanistan wanaachana nayo kutokana na hamu yao kwamba sheria ya Kiislamu ndiyo itakayo tabikishwa juu yao, na kujisalimisha kwa nidhamu ya kimataifa inayotawaliwa na Magharibi ... Kwa sababu hii, Waziri wa Kigeni wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi alitoa lakabu ya "waharibifu" kwa upinzani wa dhati wa Afghanistan ambao unakataa wazi mpango wa Kiamerika.

Enyi Waislamu katika vikosi vya wanajeshi vya Pakistan na upelelezi: Je! Ni kwa vipi mnautumikia mpango wa Amerika katika eneo hilo na kufanya kazi kama walinzi wa ruwaza ya wakoloni kwa kila njia?! Je! Vipi ruwaza ya kujisalimisha kwa maagizo ya Amerika na kuimakinisha Amerika nchini Afghanistan kwa upana wa misingi yake na ujasusi wake ilikuwa wakati wa enzi ya Musharraf? Ruwaza sahihi ilikuwaje?! Je! ni vipi ruwaza sasa imekuwa ni kuwashinikiza Waislamu wa Afghanistan kumaliza kusonga kwao mbele bila kuchoka kwenye uwanja wa vita dhidi ya majeshi waoga wa Amerika, kwa kuwalazimisha kukaa pamoja na wavamizi ambao mikono yao bado ingali inadondoka damu tukufu ya Waislamu?! Sasa imejulikana kwa kila mtu kuwa nguvu ya Amerika ni nguvu ya kindoto, na nguvu hiyo imetolewa kutoka kwenu. Basi kateni minyororo ya utumwa kwa kutoa Nusra ili kusimamisha dola ambayo nguvu za kikoloni zitaipigia magoti. Na tumieni nguvu mliokabidhiwa juu yake ili kuunusuru Uislamu na Waislamu na kuzilinda nchi za Waislamu. Na kataeni mpango wa udanganyifu wa kikoloni wa mazungumzo baina ya Waafghan. Na jueni kwamba kwa kurudisha Khilafah kwa Njia ya Utume, tunaweza kuunga mkono upinzani wa Afghanistan, kuwafukuza Makruseda wa Kiamerika kutoka eneo hilo na kuijumuisha Afghanistan na dola za Asia ya Kati, na ni Khilafa Rashida ya pili pekee ndio itakayokuwa ngome yenye nguvu kwa Waislamu, na ndiyo itakayofunga milango yote ya adui, na jueni kuwa Uislamu na Waislamu wanadai kusimamishwa kwa utiifu na nguvu kutoka kwa maafisa waaminifu katika vikosi vya jeshi la Pakistan ili kuurudisha Uislamu katika uwanja wa kiulimwengu, basi jitokezeni sasa, enyi ndugu, na muinusuru dini yenu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:  

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾.

"Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele." [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Pakistan 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-pakistan.com/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu