Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  17 Jumada II 1442 Na: 1442 / 02
M.  Jumamosi, 30 Januari 2021

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Hatua za Kisaniisanii

Tangu serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar chini ya Raisi Hussein Mwinyi kuingia madarakani imeonekana kana kwamba ina dhamira ya kweli kurejesha uwajibikaji, kukabiliana na ufisadi, rushwa na vitendo vya ubadhirifu wa mali za Umma vilivyotendwa na baadhi ya maafisa wa serikali iliyotangulia.

Licha ya hatua hizo kuwa zenye tija hafifu kwa kiasi fulani, Sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunasema kwamba bado kuna mapungufu makubwa  yanayodhihirika  katika hali zifuatazo:

  1. Kampeni hii inajihusisha na baadhi tu ya maafisa wa serikali iliyopita huku ikiwa kimya juu ya maafisa wa juu zaidi wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu wa wizara waliotangulia, na pia iko kimya hata kwa raisi aliyepita ambaye karibuni kapewa majukumu mengine ya Umma akiendelea kujifaragua kwa kinga ya kikatiba. Kama kweli Serikali ya Umoja wa Kitaifa ina dhamira ya kweli ya kupambana na rushwa na ufisadi ilipaswa iwe imewahusisha maafisa wote wa juu (waliohusika) na pia kuondoa kifungu cha kinga (ya raisi) ili kutoa nafasi kwa mchakato wa kisheria kuchukua mkondo wake. Lakini wapi! kubwa tumekuwa tukisikia kauli isemayo serikali haina haja ya kufukua makaburi yaliyopita, ilhali inayafukua lakini kwa baadhi tu ya watu.
  2. Serikali zinazoshikilia mfumo wa Kibepari (ikiwemo serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar), mfumo uliojengwa juu ya kipimo cha maslahi katika msingi wake, suala la ufisadi na rushwa ni la kimaumbile na ni saratani isiyotibika. Hivyo, vita vya kupambana navyo havitarajiwi kuzaa matunda yenye tija.
  3. Wakati Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikijidhihirisha kana kwamba ni ngao ya kuhami na kulinda ustawi wa raia, kwanini ipo kimya juu ya ukatili uliotendwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 ukihusisha mauaji ya wasio na hatia, mateso, udhalilishaji wa kingono na uporaji wa mali za watu bila ya uchunguzi wala hatua za kisheria? Pia kwanini Serikali ya Umoja wa Kitaifa inajifanya kana kwamba haijui kinachoendelea juu ya dhulma dhidi ya masheikh na maustadh (wa Uamsho) na wengine ambao wamekuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka 8 bila ya baadhi ya kesi zao kusikilizwa, kupewa dhamana au kuachiwa huru kwa kisingizio cha kutokamilika ushahidi? Vipi serikali inayodai kutetea ustawi wa raia iwe kando na mambo haya?

Ni serikali ya Khilafah pekee ndio inayoweza kuwatumikia raia kwa mambo yote na kwa upana wake na sio kiusanii, kuanzia kulinda fedha za Umma, kuhifadhi damu na heshima kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu.  Pia kulinda usalama, amani na kuleta uadilifu kwa wote.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu