Alhamisi, 16 Dhu al-Hijjah 1441 | 2020/08/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  22 Dhu al-Qi'dah 1441 Na: 1441 / 03
M.  Jumatatu, 13 Julai 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

TUNASIMAMA IMARA NA FAMILIA ZA MAHABUSU

Kufuatia mkutano wa waandishi habari wa wawakilishi wa familia tatu za mahabusu: Omar Salum Bumbo, Ramadhan Moshi Kakoso, na Waziri Suleiman Mkaliaganda mnamo 09 Julai 2020 huko Magomeni Makuti, Dar es Salaam, Tanzania ili kuelezea huzuni na uchungu wao juu ya jamaa zao watatu ambao wanazuiliwa pasi na mashtaka kwa takriban miaka mitatu, sisi katika  Hizb ut Tahrir / Tanzania  tunasimama imara kwa mshikamano na familia hizi (za mahabusu) ambao ni wanachama wa Hizb ut Tahrir / Tanzania ili kudai haki kwao.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania kwa mara nyengine tena tunavitaka vyombo vyote vinavyo husika na utoaji haki nchini Tanzania kuzingatia mchakato sahihi wa mahakama kwa kufikisha ushahidi mahakamani tayari kwa mashtaka ya mahabusu, endapo watakuwa na ushahidi wowote, waachilieni mahabusu hao watatu kwa dhamana, au waachilieni huru mara moja.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

 

Alama Ishara

#StopOppressiveLawsAndAbduction (English)

#KomeshaUkandamizajiWaKisheriaNaUtekaji (Swahili)

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu