Jumanne, 05 Safar 1442 | 2020/09/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  13 Shawwal 1441 Na: 1441/39
M.  Alhamisi, 04 Juni 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kufuatia Kuchapishwa kwa Taarifa kwa Vyombo vya Habari: “Kupeleka Majeshi  ya Amerika Nchini Tunisia ni Shari Iliyo Enea” Idara ya Facebook Imeufunga Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
(Imetafsiriwa)

Idara ya Facebook mnamo asubuhi ya 4 Juni iliufunga ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, na ingawa ufungaji huu sio wa kwanza, na wala hautakuwa wa mwisho, ni muhimu kutaja kwamba ufungaji huu ulifanywa kufuatia taarifa kwa vyombo vya habari kwa anwani “Kupeleka Majeshi  ya Amerika Nchini Tunisia ni Shari Iliyo Enea” ambayo kwayo Hizb ilionya dhidi ya kuingia kwa jeshi la Msalaba la Kiamerika nchini Tunisia, ambapo imefichua upande ambao idara ya Facebook inatangaza vita vyake viovu dhidi ya kurasa za Hizb ut Tahrir katika Facebook.

Taarifa ya hivi juzi kwa vyombo vya habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ilifichua dori ya uongozi wa Kijeshi wa Amerika barani Afrika (AFRICOM) ambao uliundwa ili kuitawala Afrika, kuifuja utajiri wake na kuwakoloni watu wake, zaidi ya hayo kupambana na Uislamu chini ya kisingizio cha kupambana na "ugaidi" kwa sababu unauona Uislamu kama tishio halisi la maslahi yake ya kiuchumi ulimwenguni, ikiwemo Afrika, ambayo wengi wa watu wake ni Waislamu. Vilevile, taarifa hiyo iliwaonya watu wa Tunisia dhidi ya kuruhusu kuingia kwa jeshi la Kiamerika nchini Tunisia, kwani pindi majeshi hayo ya Kiamerika yanapoingia katika nchini, huiangamiza na kuufanya utukufu wa watu kuwa wake udhalilifu, na hivyo ndivyo wafanyavyo. Taarifa hiyo ilitamatisha kuwa hakuna kitakachouzuia ulafi wa kikoloni wa Amerika na nchi zilizo salia za kikoloni za kikafiri za Kimagharibi na ufujaji wao wa mali ulimwengu mzima ikiwemo Afrika isipokuwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, na pasi kwayo wanadamu wote wataendelea kuteseka kutokana na ulafi wa kikoloni na dhulma ya Urasilimali. 

Idara ya Facebook kwa mara nyengine tena imethibitisha kwamba inazipendelea dola za kikoloni na ala zake za kieneo, na imethibitisha pasi na shaka yoyote kwamba hadhara ya Kimagharibi imeshindwa kukabiliana na Uislamu kifikra na kisiasa, hivyo daima hutumia mbinu za kuzuia na kufunga kama vile serikali za kiimla na huduma zake za kijasusi na licha ya kuzuia huku, Hizb ut Tahrir inaendelea kufikia lengo lake, haitazuiwa na dhulma za wenye kudhulumu wala mbinu za walio cheshewa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ]

“Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua.” [Al-Anbiya: 18].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu