Ijumaa, 10 Safar 1443 | 2021/09/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Jukwaa la Kadhia za Umma

"Kadhia ya Bwawa la An-Nadha... Fikra, Utekelezaji na Matarajio ya Mustakbali!"

(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumamosi, 28 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na tarehe 07/08/2021 M, Jukwaa la Kadhia za Umma la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan lilifanyika katika ukumbi wa afisi ya hizb jijini Khartoum, kwa anwani: "Kadhia ya Bwawa la An-Nadha... Fikra, Utekelezaji na Matarajio ya Mustakbali!", ambapo Mhandisi Haider Youssef - Mkurugenzi wa Idara ya Maji ya Nile na mtaalam wa rasilimali za maji, Bwana Hatem Jaafar, wakili - mwanachama wa Baraza la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na Bwana Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan.

Mhandisi Haider Youssef alizungumza katika muhadhara wa kwanza, akionyesha kwamba ukoloni ulizichochea nchi za Bonde la Nile kudai hisa zao katika maji ya Nile, tangu miaka ya tisiini, na matokeo yake tafiti zilianza kuanzisha vituo vya ufuatiliaji ili kujua kiwango cha maji katika Bonde la Nile ili kutekeleza miradi ya Mpango wa Bonde la Mto Nile, na kwa hivyo ni Makubaliano ya Entebbe, ambayo Sudan na Misri zilikataa kuyatia saini, kwa sababu yanatoa maamuzi yaliyoidhinishwa na wengi, sio kwa pamoja, pamoja na kufutilia mbali mgao wa kihistoria wa Misri na Sudan katika maji ya Nile. Alizungumzia pia juu ya uharibifu na hatari zilizosababishwa na Bwawa la An-Nahdha. Alidokeza kuwa serikali ya Misri inaunga mkono ujenzi wa bwawa hilo kwa ukamilifu, na kulegea inakokufanya ni kurusha vumbi machoni kwa kuogopa hasira ya watu wa Misri.

Kisha Wakili Bwana Hatem Jaafar alizungumza katika waraka wenye anwani: "Bwawa la An-Nahdha ... Zaidi ya Mawimbi," ambapo alianza hotuba yake kwamba kadhia ya Bwawa la An-Nahdha ni kadhia nyeti ambayo haina nafasi ya mjadala, wala makubaliano na maridhiano, kama alivyoonyesha kuwa eneo ambalo bwawa limejengwa, matetemeko ya ardhi zaidi ya elfu kumi yalitokea katika kipindi cha 1970 hadi 2013, yenye nguvu ya zaidi ya digrii nne kwa kiwango cha Richter, na Ethiopia ina historia ndefu ya kuanguka kwa mabwawa, ambayo ilihitaji tafiti juu ya usalama wa bwawa hili, ambao haukufanyika, kama alivyogusia taarifa za maafisa wa Ethiopia na wengineo ambao walisisitiza kuwa bwawa hili sio kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, bali ni mradi wa kikoloni kwa dhati yake.

Na alionyesha kuwa hatua nzito za suala la Bwawa la An-Nahdha zinahitaji yafuatayo:

• Kushughulikia Bwawa la An-Nahdha kama mradi wa zamani wa kikoloni wa kudhibiti maji ya Mto Nile unaotekelezwa na Ethiopia.

• Bwawa la An-Nahdha ni kadhia nyeti na muhimu mno kwa Sudan na Misri, na haipaswi kuvumiliwa au kupuuzwa.

• Bwawa la An-Nahdha ni suala la kisiasa linalohusiana na usalama, na sio suala la kisheria linalotatuliwa katika faili za taasisi za sheria za kimataifa.

• Watawala wa Misri na Sudan wamejizatiti kupuuza maslahi ya watu wa Bonde la Nile, kwa kupunguza suala hilo kutoka kwa kiwango cha kadhia nyeti ambayo tishio lake linaweza kujibiwa tu na nguvu ya kijeshi, hadi kwa kiwango cha kuwa ni suala la ziada!

• Kutambua dori chafu ya watawala waliowagawanya watu kati ya wafuasi na wapinzani katika kadhia ya bwawa, na kuwapotosha, na bado wangali wanaendelea kwenye njia ile ile.

• Usaliti wa watawala wa Sudan katika mahitaji yao tu kwa makubaliano ya lazima juu ya ujazaji na uendeshaji, bila ya kutaja kufanya tafiti zinazohusiana na usalama, athari na hatari za bwawa hili!!

Kisha Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, alizungumza katika waraka kwa anwani: "Je! Ni hatua gani za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa kwa Bwawa la An-Nahdha", ambapo alielezea mukhtasari wa hukmu ya kisheria (Hukm Shari ') kuhusiana na suala hili, akiorodhesha hukmu za kisheria zilizowekwa na Sharia katika kushughulikia mito. Alitaja pia kwamba watawala wa Misri na Sudan walikiuka vifungu vya Sharia kwa kuruhusu ujenzi wa bwawa hili, ikionyesha kwamba haki za Ummah hazingepotea lau Ummah huu ungekuwa na dola yenye misingi ya Uislamu. Alimalizia hotuba yake kwa kuwaalika wanasiasa, wataalamu wa vyombo vya habari, wanafikra, na waundaji rai jumla kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Halafu Bwana Mohamed Mabrouk - mwandishi mashuhuri na mchambuzi mzuri wa kisiasa - alitoa maoni juu ya nyaraka, kama vile Bwana Hassan Abdel Hamid - Naibu Mdhibiti Mkuu wa Ikhwaan al-Muslimin.

Kisha fursa kwa hadhira kushiriki,

1- Dkt. Mubarak Awad Al-Jayed - daktari wa wanyama.

2- Profesa Qureshi Al-Hajj – mtafiti katika sayansi za kisiasa.

3- Profesa Al-Tijani Mustafa - Chama cha Arab Socialist Ba'ath.

4- Bw. Mortada Muhammad Ali - vuguvugu la kuunga mkono Sharia na utawala wa sheria.

5- Profesa Abdullah Abu Imam - mtafiti.

Hatimaye jukwaa lilimalizika kwa taarifa hitimishi. Jukwa hili liliendeshwa vyema na Dkt. Muhammad Abdul Rahman - mwanachama wa Hizb ut Tahrir.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah ya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu