Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Majanga ya Kimaumbile yanazidi kuwa mabaya kwa kukosekana Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ripoti ya habari ya CNN siku 5 baada ya tetemeko la ardhi la Uturuki kuonya juu ya maafa makubwa zaidi nje ya kuporomoka kwa awali kwa miundombinu katika maeneo yanayopakana na Syria. Hali ya hewa ya baridi na mvua pamoja na uhaba wa chakula, vifaa vya matibabu na maji vinavyoingia katika eneo hilo inamaanisha wengi watakufa ovyo. Makaazi ni sababu kuu inayoathiri viwango vya manusura walio katika hatari ya kushuka kwa kiwango cha joto mwilini (hypothermia) katika hali ya baridi kali. Wasyria wako hatarini haswa kwani UN imeshikilia kura ya TURUFU juu ya msaada unaoingia katika maeneo yaliyoathirika. Urusi na China zimetumia nafasi zao kuziba vivuko 3 kati ya 4 vya kuingia katika mpaka wa Syria na kukwamisha kwa kiasi kikubwa misaada ambayo inaweza kutolewa kwa maelfu ya wanawake na watoto waliokosa makaazi na tayari rasilimali zinazopatikana kwao ni finyo.

Maoni:

Wazo la kwamba umbile lisilokuwa la Kiislamu ndilo linalosimamia iwapo Waislamu watapokea usaidizi wa kubadilisha maisha au la ni hali iliyoharamishwa na haikubaliwi na Mwenyezi Mungu (swt).

Idadi ya manusura tayari ni ya kimiujiza huku watu wengi zaidi wakiwa wamekufa kuliko wale waliotoka kwenye majengo yaliyoporomoka. Kufikiri kwamba baada ya yote ambayo wamevumilia kwa kweli wangekufa kutokana na kitu ambacho kilikuwa kinaweza kuzuiliwa kabisa ni jambo la kutisha zaidi kuliko tetemeko la ardhi lenyewe.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Geneva, meneja wa kukabiliana na matukio wa WHO Robert Holden alionya kuwa kuna "...watu wengi" wanaoishi "nje ya makaazi, katika hali mbaya na za kutisha. Tumepata mkatiko mkubwa wa usambazaji wa maji, tumepata mkatiko mkubwa wa mafuta, vifaa vya umeme, vifaa vya mawasiliano, mambo msingi ya maisha. Tuko katika hatari halisi ya kuona maafa ya pili ambayo huenda yakasababisha madhara kwa watu wengi zaidi kuliko maafa ya awali ikiwa hatutasonga kwa kasi na nguvu kama vile tunavyofanya katika upande wa utafutaji na uokoaji."

Ukubwa wa changamoto hiyo unazidishwa na ukweli kwamba maeneo yaliyoathiriwa nchini Uturuki na Syria yanakabiliwa na baridi zaidi kuliko joto la kawaida. Kwa mfano, mji wa Syria wa Aleppo unatabiriwa kuwa na viwango vya chini vya -3°C hadi -2°C (27°F hadi 28°F) mwishoni mwa wiki hii, ilhali viwango vya chini vya Februari kwa kawaida huwa joto zaidi.

Siku 4 baada ya tetemeko la ardhi, kivuko cha Bab al-Hawa - njia pekee ya misaada ya kibinadamu kati ya Uturuki na Syria kiliruhusiwa kufunguliwa. "Je, inakuwaje barabara ziko sawa kwa magari yanayobeba miili, lakini sio kwa msaada?" Mazen Alloush, msemaji aliyeghadhabishwa wa Bab al-Hawa alikuwa ameiuliza CNN. Abu Muhammad Sakhour, mfanyibiashara wa zamani, anajitolea kama muuguzi katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Idlib, akifunga majeraha kwa wahasiriwa wa tetemeko la ardhi na kuwafanyia uchunguzi majeruhi ambao wameruhusiwa kutoka katika hospitali zilizojaa watu.

"Hali ni mbaya kweli kweli," alisema. "Sasa tunaponya majeraha yetu wenyewe." Kwa walio hatarini kama vile wanawake wajawazito, wazee, watoto wachanga na wadogo, masaa yanayotumiwa katika hali kama hizi yanaweza kutosha kusababisha vifo kutokana na kuanikwa baridini na udhaifu.

Jambo hili la uhai na kifo ni jambo ambalo haliwezi kujadiliwa au kuachwa kwenye mikono ya kura zinazopigwa na maadui wa Uislamu. Kiukweli kile kinachotokea hapa ni uovu wa mataifa kupiga kura iwapo watu wataishi ili wafe. Khilafah na kiongozi wa Uislamu kamwe hangekubali ulisia kama huo kutokana na uwajibikaji wake wa kutuma msaada kwa watu wote katika eneo hilo, wakiwemo raia wasiokuwa Waislamu. Hakuna kisingizio kinachoweza kutolewa cha kutosimamisha tena Khilafah kama jambo la dharura la haraka kabla ya maafa mengine ya kimaumbile kutokea na Ummah wetu kuachwa na dua kwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu