Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tajikistan: Ndevu zina Maana ya Kisiasa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Aprili 26: Mkuu wa Kamati ya Mambo ya Vijana na Michezo ya Tajikistan Abdullo Rakhmonzoda, alikashifu wanablogu wenye ndevu katika mkutano mmoja wa ndani akisema kwamba "upigiaji upatu wa ndevu katika mitandao ya kijamii unatishia usalama wa taifa". "Harakati iliyopigwa marufuku ya Taliban, ambayo ilipindua serikali ya watu nchini Afghanistan, sasa inapigia debe ndevu kwa bidii. Na ikiwa raia kijana wa Tajik atafuga ndevu kama Taliban, basi hakika hii ni aina ya ishara ya mshikamano nao. Kwa kukuza ndevu, wao basi wanatoa ishara: wanasema, njoo, tunakubali maoni yako, una wafuasi hapa. Kwa hivyo, tunaunda tishio kwa serikali yetu. Ndevu pia zina umuhimu wa kisiasa. Tunahitaji kuzingatia mambo kama haya kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa kitaifa”, - afisa huyo alisema.

Maoni:

Kama tunavyoona, maafisa wa Tajik hawajaona haya kueleza hadharani uchokozi dhidi ya sifa za Uislamu kwa muda mrefu. Tayari tunasikia matusi kwa Uislamu, hijab na misikiti kutoka kwa viongozi wa eneo hilo, na kutoka kwa Rahmon mwenyewe. Vita dhidi ya Uislamu vya utawala wa Rahmon havidhoofiki, bali vinazidi. Kwa hivyo, kwa mfano, ikiwa mapema uungaji mkono wa serikali na wahubiri na maimamu uliwahakikishia usalama wa kiasi, sasa serikali inawafunga hata wale ambao bila shaka walishirikiana na mamlaka, lakini hawakufanya kwa uchangamfu wa kutosha.

Kumbuka kwamba Tajikistan kwa mara nyingine imekuwa miongoni mwa dola 17 "zinazo na wasiwasi sana" kuhusu uhuru wa kidini, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya kuzingatiwa kwa haki za kidini duniani na Tume ya Marekani ya Uhuru wa Kidini wa Kimataifa (USCIRF). Nchini Tajikistan, kwa mujibu wa waandishi wa ripoti hiyo, hali ya uhuru wa kuabudu bado inasikitisha: serikali ya nchi hiyo inaendelea kuwakandamiza Waislamu - watoto wa chini ya miaka 18 wamepigwa marufuku kuhudhuria misikiti; elimu ya dini haiwezekani, kuna ukomo wa umri wa kuhiji, wanawake wamekatazwa kuvaa nguo za kidini, na wanaume wamekatazwa kufuga ndevu, na tangu 2014, hotuba zilizokubaliwa na viongozi zimekuwa zikisomwa misikitini. Bila shaka, inapotajwa ripoti hii, mtu asisahau kwamba "maneno haya matupu ya kujali" ya wanaharakati wa haki za binadamu wa Magharibi hayazuii hata kidogo serikali za nchi za Magharibi kushirikiana na kuwaunga mkono madikteta katika ulimwengu wa Kiislamu, akiwemo Rahmon.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu