Jumatano, 22 Dhu al-Hijjah 1441 | 2020/08/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika Inateketea na huku Ubepari Ukianguka

Habari:

Raisi wa Amerika Trump ametangaza kwamba amesambaza maelfu ya majeshi na vikosi vya usalama vilivyo jihami sawasawa ili kupambana na hali ya vurugu nchini. Kumetangazwa amri ya kutotoka nje usiku kwa muda wa siku mbili ndani ya jiji kuu la Amerika, Washington DC, baada ya maandamano mazito yaliyo tikisa jiji hilo dhidi ya mauaji yaliyofanywa na polisi kwa Mwamerika mwenye asili ya Kiafrika George Floyd. Tim Walz, Gavana wa jimbo la Minnesota, alitangaza kwamba mazishi ya Floyd yatafanyika siku ya Alhamisi. Trump alieleza kwamba vikosi vya usalama na vikosi vya walinzi wa kitaifa vitapekekwa kote nchini kutokana na hali ya ongezeko la maandamano na vurugu. (https://www.milliyet.com.tr/galeri/son-dakika-haberi-ve-abdde-kiyamet-koptu-trump-askerlere-emir-verdi-6224711)

Maoni:

Amerika inapambana na wimbi la waandamanaji ambalo haijawahi kuliona katika miaka ya karibuni. Machafuko yako kila mahala. Mitaani kumechafuka. Kuna matukio ya uporaji takriban kila pahala nchini. Kwa hali yoyote iwayo Amerika haijawahi kuwa hivi, vikosi vya kijeshi vimesambaa nchini kuingilia kati hali hiyo.

Kwa kweli, Waamerika wamezoea haswa mashambulizi ya kiubaguzi wa rangi na vitendo vya ghasia vya polisi dhidi ya watu weusi. Kumekuwa na matukio mengi nchini yanayofanana na tukio la Georg Floyd, lakini katika matukio hayo ya kihalifu halikuwepo hata tukio moja lililo weza kupelekea mripuko mkubwa wa maandamano kama ilivyo kuwa kwa tukio la George Floyd. Basi, ni kwa nini majibu ya Waamerika yamekuwa ya vurugu mno kwa tukio la kuuwawa George Floyd?

Ni hali isiyo na shaka kabisa kwamba watu wanafungamana kuwa kitu kimoja kwa sababu  ya dini zao, rangi zao au itikadi zao za kimfumo. Fungamano pekee linalo wafungamanisha watu wanaoishi ndani ya Amerika pamoja na Dola yao ni maslahi, yanayo tokamana na itikadi ya mfumo wa kirasilimali. Na uraia wa Mwamerika ni makubaliano yaliyofanywa juu ya maslahi haya.

Kwa kuenea mripuko wa virusi vya korona hadi Amerika, upande wa ulafi wa Urasilimali umedhihirika kwa mara nyengine tena. Maelfu ya watu hakuweza kunufaika na huduma za afya kwa sababu ya kukosa pesa. Kuwa mtu asiye na ajira ndani ya Amerika inamaanisha kwamba umehukumiwa kuishi mtaani. Kwa mazingira haya, Waamerika wameona kwamba nidhamu ya kirasilimali haichukulii uzito wowote dhidi ya maisha yao. Na badala yake, wameona kwamba wanadharauliwa kama bidhaa iliyokosa thamani. Na kama ilivyo kwa tukio la video lililo sambaa kwenye mitandao ya kijamii ambalo Floyd anauawa kikatili kwa kukandamizwa shingoni mpaka kufa tukio lililo fanywa na mhalifu kwa kuiwakilisha dola, raia wa Amerika ambao wanashutumiwa kufanya kazi katika mazingira mazito na kujitolea mhanga, wamejionea picha yao wenyewe kwa tukio la George Floyd. Floyd hakuwa ndio wa mwanzo kuuawa kwa kifo cha namna hii. Mamilioni ya Waamarika waliguswa na tukio la kukandamizwa shingoni na kufa kwa Floyd, na kichobakia kinajulikana. Makubaliano ya uraia yamevunjika. Maandamano hayo yaliyo ambatana na uporaji. Karibia maduka makubwa yote yaliporwa.

Kijana wa kike ambaye aliwaongoza waandamanaji alipiga kelele mbele ya kamera “Usizungumze na sisi kuhusiana na uporaji. Nyinyi nyote ni waporaji! Amerika imewapora watu weusi. Amerika imewapora Waamerika wanati. Hivyo, uporaji ni kazi yenu. Tumejifunza hili kutoka kwenu!’’

Picha za maandamano na uporaji kutoka takriban kila jiji imepelekea kuwa na hali ya kujiuliza dhidi ya mamlaka iliyonayo ulimwenguni. Inawezekana vipi kwa taifa ambalo haliwezi hata kusimamia utawala hata katika nchi yake yenyewe liweze kuwa maridadi katika kusimamia ulimwengu mzima? Wanaweza vipi watawala wa Waislamu kukubali kuwa watumwa wa dola ambayo haiwezi hata kusikilizwa na watu wake wenyewe?

Bila shaka yoyote, jibu la swali hili linafichika kwenye usaliti wa watawala wa Waislamu. Watawala hawa hawafahamu uwezo wa nguvu walionayo watu wao wenyewe, na ambao huisi viti vyao vya utawala kuwa salama wakati wanapo egemea Wamagharibi, hasa Amerika, ni watawala ambao wametengana na Ummah wa Kiislamu na ambao hawaonyeshi tabia za Ummah wa Kiislamu. Kwa sababu Ummah wa Kiislamu hauifungi nguvu yake kwa ukubwa wa kiidadi au ukubwa wa kiuchumi. Kama ingekuwa hivyo, basi wasingekuwepo kwenye bandari za Himaya ya Sasania, ambayo ilikuwa mojawapo kati ya dola kubwa katika kipindi chake ambacho ni miaka michache baada ya kusimama dola ya Khilafah, na ambayo ilikuwa na ukubwa zaidi wa kiidadi na kiuchumi.

Kwa hakika, Urasilimali bado unaendelea kutikiswa. Unachirizika damu kwa kadri siku zinavyo pita. Jamii zinaugeuka, kwa sababu muda wake wa kuanguka umeshakaribia. Wanadamu wapo kati ya machaguo mawili. Imma Urasilimali ukarabatiwe upya na kuwa nidhamu ya kijamii kwa kufanya mabadiliko ya maadili yake msingi. Au nidhamu nyengine itakuja kuondosha Urasilimali kama mbadala wake .

Wakati tunapozingatia ukweli kwamba mawazo yanayotokamana na mawazo ya kirasilimali, tutaweza kuona kwamba chaguo la kwanza haliwezekani. Haiwezekani kuonekana kwamba Urasilimali utakuwa wenye kugeuka kuwa nidhamu baina ya hizi mbili. Hivyo chaguo la pekee ni nidhamu mpya.

Kwa kuwa hakuna mfumo mwengine zaidi ya hizi mifumo hii mitatu, kwa kuwa mwisho wa Urasilimali umeshafika, kwa kuwa Ujamaa umeshajaribiwa  na kukataliwa, hivyo basi ni mfumo wa Kiislamu na nidhamu ya Kiislamu pekee, ambayo umevuliwa kutoka katika mfumo huu, iliyobaki. Huo ndio mfumo haswa ambao wanadamu wanauhitaji .

Nidhamu kipekee ya kiuchumi ambayo haishawishi wala haikandamizi tamaa ya kupata mali kwa asili yake kama Mwanadamu, kuweka mizani baina ya haya mawili, kuzingatia ugavi adilifu wa mali, sio uzalishaji wa mali, ni nidhamu ya kiuchumi wa Kiislamu.

Mlango pekee ambao angeweza kugonga mwanadamu, ambaye anatafuta amani na furaha, ni mlango wa mfumo wa Kiislamu. Huu ni ukweli usiokanushika. Ni swala lenye kusubiria wakati tu... Na muda ni wenye kukimbia kiasi mno kwa njia ambayo hakuna anaye weza kudhibiti.

Muda unakaribia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Süleyman Uğurlu

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 31 Julai 2020 07:05

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu