Jumapili, 06 Ramadan 1442 | 2021/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa vya Habari 24/02/2021

Vichwa vya habari:

Amerika Yaigeukia Urusi

Familia ya Kifalme ya Uingereza Kuendeleza Ushawishi wa Kiingereza

Japan Yamteua ‘Waziri wa Upweke’

Maelezo:

Amerika Yaigeukia Urusi

Kulingana na taarifa kutoka Politico, utawala wa Biden unajiandaa kuigonga Urusi pigo kubwa kutokana na tukio la Urusi la  kumfunga na kumshambulia kwa sumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny. Vyanzo vya taarifa vimeiambia Politico kwamba Amerika inajipanga kuweka vikwazo kwa kushirikiana na nchi za Ulaya. Taarifa kuhusu aina zipi za vikwazo ambavyo Rais Biden anakusudia kuviweka dhidi ya Urusi bado hazijawekwa wazi. Taarifa inasema kwamba, utawala wa Trump ulikuwa umeshaandaa mapendekezo ya adhabu kwa Urusi, mapendekezo ambayo utawala mpya unayapitia. Maafisa wa Utawala wa Biden wametishia kuchukua hatua dhidi ya Urusi kupitia shutuma dhidi yake.

Shutuma nyingi, kama madai ya kuwa Urusi inailipa Taliban ili kuua wanajeshi wa Amerika nchini Afghanistan, bado hayajathibitishwa. Wakati huo huo Rais Biden kwa haraka amefikia makubaliano na  Putin katika kile kinachoitwa MWANZO Mpya, mkataba wa silaha za nyuklia, akidumisha  hali ya sintofahamu na Moscow. Mbali na maswali yasio hitajia majibu na vitisho vya vikwazo, Amerika pia imekuwa ikisogeza shughuli zake za kijeshi katika sehemu nyingi ili kuikabili Urusi. Amerika na NATO wote wanapanga kupanua na kuongeza uwepo wao katika eneo Bahari Nyeusi. Utawala wa Biden umepeleke manuari kubwa mbili za makombora katika eneo la Bahari Nyeusi kwa siku 17, ikiwa ni moja ya kati ya utumaji vikosi mkubwa katika kanda kwa miaka ya hivi karibuni.

Arctic ni eneo jingine ambalo Amerika inalitazama kwa ajili ya kupanua ushawishi wake dhidi ya Urusi. Kama sehemu ya juhudi hii, Washington imeweka aina ya ndege za kivita B-1 bombers katika nchi ya Norway, na kufanya kwa mara ya kwanza nchi ya Scandinavia kuwa na aina ya ndege hizo za kivita. Chini ya Trump uimarishaji wa Amerika ulishindwa kumfanya Rais kuweka umakini katika ushindani mkubwa na Urusi, haswa pale ambapo Trump alipokuwa akimsifu Putin na kuisifu Urusi. Mara chache Trump alipolazimika kuiwekea vikwazo Urusi ilikuwa ni kwa shinikizo la bunge la Congress. Kwa uzoefu mkubwa aliokuwa nao ikulu ya White House hivi sasa akiwa madarakani umakini umerejea upya dhidi ya China na Urusi.

Familia ya Kifalme ya Uingereza Kuendeleza Ushawishi wa Kiingereza

Wanachama wa familia ya kifalme ya Uingereza wamekutana na tawala za kiimla za mashariki ya kati zaidi ya mara 200 tangu kutokomezwa kwa mchepuo wa kiarabu ulioanza mwongo mmoja uliopita, taarifa iliweka wazi. Utafiti mpya uliofanywa katika tovuti iliyoiweka wazi Uingereza na kuonyesha kwamba kumekuwa na mchakato uliodumu kwa miaka 10. Familia ya kifalme ya Bahrain imekuwa na wahudhuriaji wengi mno, kulingana na habari ya tovuti hiyo, ikifuatiwa na nyumba ya Saud. Mtoto wa kiume wa mfalme wa Bahrain, Nasser bin Hamad Al Khalifa, kwa mfano, ambaye amehusishwa na kuwatesa wanaharakati, alikutana na wanachama wa familia ya kifalme ya Uingereza mara saba, ikiwa ni pamoja na nyumbani kwao, Kasri la Windsor. Maelezo kuhusu mazungumzo hayo hayajawekwa wazi: taarifa kuhusu familia ya kifalme ya Uingereza imebaki kuwa ni siri mafaili ya serikali yenye taarifa hizo yameondolewa katika sehemu maalumu za taifa za kuhifadhia taarifa. Kitengo cha diplomasia cha Amerika kimeweka wazi kupitia mtandao wa WikiLeaks kikiangazia umuhimu wa familia ya kifalme kama zana ya Uingereza na sera za kigeni za mashariki ya kati. Wakati huo huo Uingereza imeendelea kuimarisha ujenzi mashariki ya kati kitu ambacho kimetengeneza njia kwa Amerika ambayo tangu Vita vya Pili vya Dunia imejitahidi kuyaondoa mataifa ya Ulaya katika ukanda huo. Uingereza imeweza kudumisha ushawishi wake kupitia watawala wa Ghuba katika ukanda huo na familia za kifalme, ambao ndio ufunguo kwa Uingereza ni mikono iliyozeeka katika kuimarisha ushawishi wa Uingereza katika dunia.

Japan Yamteua ‘Waziri wa Upweke’

Japan imemteua “waziri wa upweke” kujaribu kupunguza upweke na kutengwa kijamii miongoni mwa wakazi wake. Maamuzi hayo yamechukuliwa na serikali kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watu wanaojiua. Waziri Mkuu Yoshihide Suga, mapema mwezi huu, alimteua Tetsushi Sakamoto kama waziri wa upweke kwa ajili ya kudhibiti idadi kubwa ya wanaojiua inayoongezeka kwa kasi kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 11. Sakamoto ameshawahi kuwa waziri anayeshughulikia kupunguza idadi ya watoto kuzaliwa, na hivi sasa anapambana na tatizo la upweke na kujitenga. “Wanawake wanapata tabu zaidi katika kutengwa zaidi ya wanaume, na idadi ya wanaojiua inazidi kuongezeka,” Suga alimwambia Sakamoto mnamo tarehe 12 mwezi Februari katika mkutano wa wanahabari akitangaza majukumu mapya, kulingana na Japan Times.  Mwezi Oktoba, watu wengi zaidi wamekufa kwa kujiua zaidi ya walivyo kufa kwa Virusi Vya Korona mwaka mzima wa 2020.

Kulikuwa na vifo vya kujiua 2,153 mwezi huo na jumla ya vifo vya Virusi Vya Korona 1,765 mwishoni mwa mwezi wa Oktoba 2020 nchini Japan. Nchi kama Japan imekuwa na utajiri wa nyenzo baada ya kuukumbatia ubepari, lakini bado inahangaika na matatizo ya kijamii yanayopelekea kupunguza idadi ya watu na baki ya mambo mengine ya kijamii  ambayo haijui hata namna ya kuyatatua.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu