Jumatatu, 04 Safar 1442 | 2020/09/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa Vya Habari 08/05/2020

Vichwa vya Habari:

Mporomoko wa Sasa wa Kiuchumi wa Ulaya ndio Mbaya Zaidi Tangu Vita Vya Pili vya Dunia, Ripoti zinaonyesha

Imran Khan Auonya Ulimwengu kuhusu Operesheni Batili ya Bendera ya India dhidi ya Pakistan

Virusi vya Korona vya Tishia 'Vita Baridi' Vipya kati ya Amerika na China

Maelezo:

Mporomoko wa Sasa wa Kiuchumi wa Ulaya ndio Mbaya Zaidi Tangu Vita Vya Pili vya Dunia, Ripoti zinaonyesha

Ulaya ipo katikati ya mporomoko [mdororo wa uchumi] ambao haujawahi kuonekana tangu mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia, na hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi, afisa wa ngazi ya juu katika benki kuu ya Ulaya alisema siku ya Alhamisi akichora taswira kwamba hali hii itapima ni kwa kiasi gani viongozi wa kisisa wa bara hilo wapo tayari kuutunza muungano wao ulio paraganyika . “Eneo la ulaya linakabiliwa na kusinyaa kwa uchumi kwa kiwango na kasi ambayo haijawahi kuonekana wakati wa amani,” Christine Lagarde, Raisi wa Benki Kuu ya Ulaya, alisema huku akionya kwamba uchumi wa kanda ya ulaya huenda ukashuka kwa asilimia 12 kwa mwaka huu. Katika juhudi za kuzuia mgogoro mwengine wa kiuchumi ambao utazalisha miaka mingi ya uhasama wa kiuchumi, Baraza la Usimamizi la Benki hiyo liliamua mnamo Alhamisi kuzilipa benki barabara ili kukopesha pesa na kuapa kufanya kila juhudi kuhakikisha inazuia athari za kiuchumi zilizo sababishwa na janga la virusi Vya Korona. Lakini wataalamu wengi wa uchumi na vongozi wa serikali wamekubali kwamba ingawa benki kuu huo kuonyesha nguvu yake ya kifedha, itakayowezesha kupatikana kwa zaidi ya dolari trilioni 4 ndani ya uchumi, hazitatosha kudhamini uhai wa kanda ya kiuchumi ya Ulaya bila msaada kutoka katika serikali hizo. “Ulaya inaendelea kupata pigo la kiuchumi lisilokuwa na mfano katika zama hizi,” alisema Paolo Gentilo, Kamishna wa uchumi wa Ulaya na waziri mkuu wa zamani wa Italia. “Hii ndio sababu tunahitaji mpango mbadala ambao utakuwa mkubwa na fanisi mno, utakaolenga katika uchumi na sekta zilizo athirika zaidi, na kuingizwa katika utendaji kwa miezi ijayo.” “kama sio sasa, itakuwa lini?” aliongezea. Bi. Lagarde aliwasihi viongozi wa Ulaya kuzidisha viwango ya vile walivyo ahidi awali na “kufanya kazi kufikia kupata hazina ya uokozi yenye kujitolea kukabiliana na migogoro hii isiyo ya kawaida.” Tathmini yake ya kina ya athari ya kiuchumi ya virusi vya Korona ilijiri baada ya shirika la twakimu la Muungano wa Ulaya kukadiria kwamba uzalishaji wa kiuchumi katika kanda ya ulaya utashuka kwa asilimia 3.8 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ndio matokeo mabaya zaidi tangu sarafu ya pamoja kuzinduliwa mnamo 1999. [Chanzo: NY Times]

Kwa mara nyingine tena mgogoro wa kiuchumi unaonyesha wazi kwamba Muungano wa Ulaya umegawanyika pakubwa juu ya tatizo la kiuchumi na uwezekano wa Muungano wa Ulaya kugawanyika kwa misingi ya nchi tajiri na masikini. Hili linatoa wito wa kutilia shaka uwezo wa kudumu kwa mradi wa Muungano wa Ulaya.

Imran Khan Auonya Ulimwengu kuhusu Operesheni Batili ya Bendera ya India dhidi ya Pakistan

Mnamo Jumatano Mkurugenzi Mkuu wa ISI Luteni Jenerali Faiz Hamid alimtembelea Waziri Mkuu Imran Khan na kujadili mambo yanayo husiana na usalama wa taifa, ilisema taarifa iliyo thibitishwa na Afisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Habari. Mkutano kati ya kiongozi wa ISI na Waziri Mkuu ni muhimu sana kufuatia ukatili wa India dhidi ya Pakistan kwa kufanya uchokozi na kutumia njia za propaganda. Wakati huo huo, Msaidizi Maalumu wa Kitengo cha Usalama wa Taifa Dkt. Moeed Yusuf pia alimtembelea Waziri Mkuu Imran Khan katika ziara tofauti na wakajadiliana hali ya eneo ilivyo, haswa mashambulizi ya India katika masiku ya hivi karibuni, miongoni mwa mambo mengine. Mapema, Waziri Mkuu Imran Khan mnamo Jumatano, aliyataja madai ya India ya Pakistan kupenya Mpaka wa Udhibiti (LoC) kama “yasiyo na msingi wowote”, akisema hayo ni “muendelezo wa ajenda za hatari”. Waziri Mkuu kupitia katika mtandao wa Twitter alisema kwamba amekuwa “akiuonya ulimwengu kuhusu kuendelea kwa juhudi za India za kutafuta kisingizio cha operesheni batili ya bendera dhidi ya Pakistan”.

Maneno hayo ya Waziri Mkuu yanajiri baada ya mlipuko wa madai kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa India Rajnath Singh, Mkuu wa Majeshi Jenerali MM Naravane na maafisa wengine kuhusu kile wanachokiita “Eneo salama la kufanyia ugaidi” upande wa Pakistan wa mpaka wa LoC na kuwa ndio njia wanayotumia magaidi. Akizungumzia kuhusu Kashmir iliyo kaliwa, Imran Khan alisema “upinzani wa wenyeji wa Kashmiri dhidi ya uvamizi wa India ni natija ya moja kwa moja inayotokana na ukandamizaji na unyama wa India” kwa watu wa Kashmir. Alionya kwamba “sera za kiimla” za serikali ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ni za “taharuki na ni hatari mno”. Aliisihi jamii ya kiulimwengu kuchukua hatua kabla ya hatua "ovyo na zenye kuhatarisha amani na usalama" za India eneo hilo. Kiongozi wa upinzani na PML-N Rais Shehbaz Sharif pia alikemea madai hayo ya India. “kasumba ya kizalendo iliyo vuka mipaka umeenea katika damu ya Modi. Licha ya mapambano dhidi ya Korona, vitendo vya kihalifu vinavyo faywa na jeshi la India vimekithiri kiasi cha kurekodiwa matukio 940 kwa mwaka huu pekee,” alisema kupitia mtandao wa Twitter. “Madai ya ‘uwanja salama wa ugaidi’ kutoka India yanalenga kukuza propaganda dhidi ya Pakistan!” mapema kabisa, Mkurugenzi Mkuu wa ISPR Meja Jenerali Babar Iftikhar alikemea madai ya jeshi la India na kuyaita ‘yasiokuwa na mashiko’ na  ‘yakupuuzwa’. DG ISPR alisema vitendo vya kihalifu vinavyo fanywa na India katika eneo LoC vimekuwa vikiongezeka kila uchao. “Hali katika eneo la LoC imezidi kuwa mbaya,” alisema. “Uongozi wa India unatengeneza madai yasiyo kuwa na msingi dhidi ya Pakistan,”alisema. “India ina satelaiti zake yenyewe. Twambie, uko wapi ushahidi unao onyesha maeneo ya kufanyia ugaidi” aliuliza. Msemaji wa jeshi aliwaalika waangalizi wa kimataifa kufanya ziara katika eneo la LoC ili kushuhudia endapo madai ya India ni ya kweli au la. Alisema kwamba India ilikuwa inajaribu kuilaumu Pakistan kwa matatizo yake yenyewe ya ndani. Meja Jenerari Babar alisema kwamba tume ya Kiamerika iliangazia namna ambavyo India imekuwa ikitekeleza mauaji dhidi ya jamii zake za wachache . [Chanzo: The Nation].

Dunia imeshughulishwa mno na virusi vya Korona kiasi cha kushindwa kutulizia makini uvamizi wa India katika eneo la Kashmiri pamoja na LoC. Muda sasa umewadia kwa Pakistan kuchukua hatua mikononi mwake yenyewe na kuiunganisha Kashmir nayo milele.

Virusi vya Korona vya Tishia 'Vita Baridi' Vipya kati ya Amerika na China

Rais Donald Trump ameituhumu China kwa kuficha kuhusu virusi vya Korona, alieleza kwamba huenda serikali hiyo iliruhusu kusambaa kwa ugonjwa huo, na kutishia kuilipisha "thamani stahiki" Beijing. Maafisa wa China waliukasirisha utawala wa Trump kwa ujinga wa kimakusudi, utepetevu hatari wa kiusimamizi na hata kujaribu “kuisaliti.” Urushianaji wa kila siku wa mabomu kati ya Washington na Beijing umewashtua wataalamu wa usalama wa taifa wanao hofia kuwa “Vita Baridi” vinatokota kati ya dola mbili kubwa duniani katika wakati ambao ulimwengu upo katika ambapo kuna janga la kiulimwengu. "Hali hii ni hatari mno kwa ulimwengu," alisema Rachel Esplin Odell, mtaalamu kutoka China katika taasisi inayo jishughulisha na mambo ya kiutawala. “Serikali zote mbili zinajaribu kunufaika kindani kutokana na makosa ya mwenzake," alisema, kupigana moto kwa moto huku ulimwengu ukiungua.

Athari huenda zikawa kubwa mno – zikirefusha janga hili la maambukizi, na kuongeza kina katika mgogoro wa kiuchumi wa kiulimwengu, ikihatarisha mazungumzo tete ya kibiashara na kufungua mianya mipya ya kisiasa ya kimaeneo, Odell na wengine walisema. "Aina hii ya kadhia za kiasili ambazo ungetarajia kuwepo na ushirikiano dunia nzima – haswa miongoni na dola zinazo ongoza – kwa sababu mporomoko ni mkubwa mno huupati," alisema Jacob Stokes, mchambuzi mkuu wa sera za China kutoka Taasisi ya Amani ya Amerika, taasisi isiyokuwa ya mrengo wowote. Mpaka sasa, hakuna ishara kuwa uhasama mkali utapelekea makabiliano ya jeshi, japo jeshi la wanamaji la Amerika lilifanya "operesheni ya ubaharia huru " hivi majuzi wakati huu katika bahari ya kusini mwa China, sehemu ambayo Beijing inadai ni eneo lake. Lakini mahusiano kati Amerika na China ni "mbaya zaidi kuliko yalivyo kwa karibu miaka 50," alisema Stokes, mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa wa Makamu wa Rais Joe Biden. Mojawapo ya majeruhi wa kwanza huenda ikawa ni mkataba wa kibiashara uliopigiwa upatu mno ulio sainiwa kati ya Trump na Makamu wa Waziri Mkuu wa China Liu katika ikulu ya White House mnamo Januari  – "awamu ya kwanza" ya makubaliano ambayo maafisa wa ikulu ya White House walisema huenda ikafuatiwa na mkataba mpana zaidi. Haiko wazi iwapo China itakuwa tayari au kuweza kufuatilia ahadi zake katika awamu ya kwanza, inayo jumuisha ahadi ya kununua bidhaa na huduma za Amerika zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 200 kwa miaka miwili ijayo – kuanzia katika bidhaa za kilimo hadi magari mpaka vifaa vya kitabibu. [Chanzo: US Today]

Dunia ya leo inafanana na ile ya miaka ya thalathini. Wakati huo ikiwemo katikati ya unyogovu wa kiuchumi Ujerumani iliyo kuwa ikiinuka ilitishia mfumo wa kiulimwengu wa Uingereza, ambapo hatimaye ilipelekea Vita vya Pili vya Dunia. Leo, Dunia imetumbukia katika unyogovu mwingine tena mkubwa na kuinuka kwa China kunatishia ubwana wa Amerika.

#Covid19    #Korona       كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 14 Juni 2020 20:01

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu