Jumatano, 15 Safar 1443 | 2021/09/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Vichwa Vya Habari 06/06/2020

Habari:

Unyanyasaji wa Trump wa Waandamanaji Wanaopinga Ubaguzi wa Rangi Inaonyesha Mgawanyiko Demokrasia Huru

India Yatuliza Mahusiano na China; Lengo Halisi la India ni Waislamu wa Kashmir

Amerika Inafanya Kazi ili Uamuzi wa Libya uwe kwa ya Maslahi Yake

Maelezo:

Unyanyasaji wa Trump wa Waandamanaji Wanaopinga Ubaguzi wa Rangi Inaonyesha Mgawanyiko Demokrasia Huru

Wakati maandamano na machafuko yakiendelea kote nchini Amerika, Raisi Donald Trump na timu yake wameanza kuchukua hatua. Lakini sio kwa ajili ya kulitatua tatizo au kutangaza mageuzi yanayo tarajiwa. Badala yake, Trump ametumia fursa hiyo kwa manufaa yake ya kisiasa.

Maandamano hayo yalisababishwa na tukio la kuuwawa bwana George Floyd, mmarekani mweusi aliye fariki mikononi mwa polisi baada ya polisi kukita goti lake kwenye shingo kwa muda wa dakika 9. Wakati kama huu, kunahitaji busara na kiongozi anayeweza kuwatuliza watu lakini hili ni gumu kwa Trump ambaye ameendelea kutoa matamshi ya kibaguzi.

Haya yalifanyika siku ya Jumatatu, wakati Trump alipotishia kulituma jeshi kuzima maandamano, na kitendo cha kuwatumia polisi kuwatawanya wandamanaji karibu na ikulu ya White House. Ili kupisha msafara wa raisi kuelekea kanisa jirani la St. John’s Episcopal. Muda mfupi tu baada ya polisi kuwatawanya wandamanaji kwa vitoa mchozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji baridi, Trump alisikika akisema, "ni mshirika wa wandamanaji wa amani."

Mwanzoni mwa siku hiyo, kwa hasira Trump aliwaamrisha magavana kuwazuia wandamanaji katika majimbo yao. Alisema wanapaswa "kuwadhibiti" waandamanaji ili kuzima machafuko.

Ni umbile la nidhamu ya kidemokrasia kusababisha migawanyiko baina ya watu. Ili kufanikiwa, wanasiasa ni lazima, katika muda wote wa taaluma yao, hudumisha ngome imara za wafuasi miongoni mwa watu.  Upandikizaji migawanyiko na chuki ndio njia rahisi mno ya kufanya haya. Hii ni kinyume na nidhamu ya utawala wa Kiislamu ambapo Khalifah huchaguliwa na hudumu kwa kipindi chote cha uhai wake. Kwa hivyo khalifa hana haja ya kuwagawanya watu na kupandikiza chuki ili apate kudumisha uungwaji mkono. Mbali na hayo katika uchaguzi wa Kiislamu, misingi na fikra zisizo za Kiislamu ni Haramu, fikra hizo ni kama vile umadhehebu, ubaguzi wa Rangi, dini, umajimbo n.k Matokeo chanya ya hili ni kuyeyuka kwa watu na kuwa ummah mmoja usio gawanyika ambao ni  kinyume na  kile kinachofanyika  leo Magharibi na kwengineko chini ya nidhamu za kidemokrasia ambazo zimewatenga na kuwagawanya watu.

India Yatuliza Mahusiano na China; Lengo Halisi la India ni Waislamu wa Kashmir

Baada ya kushtushwa na hatua za China katika eneo la Ladakh, India imeamua kutuliza hali. Kwa mujibu wa Al-Jazeera:

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya India, India na China zimekubaliana kutatua mgogoro wao wa mpaka wa Ladakh kwa njia ya "amani"

Taarifa hiyo ya Ijumaa imekuja kabla ya majenerali wakuu wa pande zote mbili kupanga kukutana mpakani hapo ili kumaliza kabisa mzozo huo ambao ulianza baada ya India kudai kwamba vikosi vya kijeshi vya China vimevuka mpakani wake mara tatu mnamo Mei.

Maafisa wa India wanasema pande zote mbili zitalenga kwanza kukubaliana juu ya pande zote kurudisha jeshi nyuma na kusalia katika eneo la awali.

Wanajeshi wa pande zote wameweka kambi katika bonde la Galwan eneo la nyanda za juu la Ladakh, na wakituhumiana kukoleza mzozo huo wa mpaka. Ambao mwaka wa 1962 ulisababisha umwagikaji wa damu.

China inadai kiasi cha kilomita 90,000 mraba (maili 34,750 mraba) za mpaka wa kaskazini mashariki mwa India. India nayo  inasema kwamba China imechukua kimabavu kilomita 38,000 mraba (maili 1,467 mraba) za mpaka wake katika eneo la Askai chin mashariki mwa milima ya Himalaya ikijumuisha eneo la ukanda wa Ladakh.

Maafisa wa ngazi za juu wa nchi zote mbili walizungumza kupitia njia ya video na kukubaliana kwamba “pande zote mbili zitatue mzozo huo kwa njia ya amani” na kutoruhusu kuzozana, ripoti ya wizara ya mambo ya nje ilisema.

Vitendo vya India katika eneo la Ladakh havikulenga kuijaribu China, bali vililenga kuhalalisha ukaliaji wa kimabavu wa eneo la Kashmir. Suala muhimu sio kwa nini China iliirudisha nyuma India, suala muhimu ni kwa nini Pakistan haikufanya hivyo. Ni dhahiri kwamba nafasi ya Pakistan ni zaidi ya swali lisilo na jibu. Waziri Mkuu wa India Nerandra Modi anaendeleza vizuri mpango makhsusi ili Kashmir iwe sehemu ya India. Na Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan anafuta kikamilifu mpango huo huo kwa kuiruhusu India kufanikisha mpango wake. Mchunguzi makini atagundua kwamba ni Amerika ndiyo iliyo nyuma ya wote wawili na pia ndiyo inayo panga mipango hii. Ni muhimu mno kufichua uongo wa siasa za Pakistan na utawala wa jeshi hilo kwa kushirikiana katika mpango huu mchafu.

Amerika Inafanya Kazi ili Uamuzi wa Libya uwe kwa ya Maslahi Yake

Kutokana na kufeli kwa kamanda wa mashariki Khalifah Haftar kuidhibiti kikamilifu Libya, inaonekana wazi Amerika inamtelekeza na kupanga mpango mwingine wa makaazi ya pamoja kati ya mashariki na magharibi kwa pamoja jambo ambalo litainufaisha zaidi Amerika. Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post:

Wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wamedhibiti ngome ya mwisho ya mashariki ya kamanda wa wanamgambo Khalifa Haftar mnamo Ijumaa, kitu ambacho kimerudisha nyuma malengo yake ya kudhibiti nchi.

Wapiganaji wa upande wa serikali wanaoungwa mkono na Uturuki walifika katikati ya Tarhun, takriban maili 40 kusini mashariki mwa mji mkuu, Tripoli mnamo Ijumaa asubuhii baada ya majeshi ya Haftar kurudi nyuma, haya ni kulingana na makamanda wa kijeshi na wachambuzi wa mambo ya ulinzi. Video zilorushwa mtandaoni zilionyesha magari aina ya pick-up yakiwa na silaha za kivita na wapiganaji wakionyesha alama za ushindi.

Mohammed Gnounou, ambye ni msemaji wa kijeshi wa serikali ya Tripoli, alisema katika taarifa moja kwamba ni wapiganaji walioingia mjini humo kupitia sehemu nne na kumfunza Haftar "somo ambalo hatalisahau". Afisi ya jeshi ya Haftar haikujibu chochote baada ya kuombwa maoni juu ya hili...

Haftar,  ambaye ana uraia wa Amerika na Libya na pia aliitumikia CIA wakati akiishi Virginia kaskazini, alipata ufadhili wa silaha nzito na msaada mwingine wa kijeshi kutoka Imarati, Misri, na kutoka katika nchi nyingine zenye nguvu kinyume na azimio la udhibiti wa silaha la Umoja wa Mataifa...

Lakini, kubadilika huku kwa matukio kumetokana na muungano kati ya Uturuki na Urusi kama vile makala haya yatakavyo eleza baadaye:

Hadi kufika mwezi uliopita, wanamgambo wanaoegemea upande wa GNA wakisaidiwa na ndege zisizo na rubani za Uturuki na mifumo ya ulinzi ya Uturuki, wameweza kumshinda Haftar na kuchukua mji. Ikiwa ni pamoja na kuukamata uwanja wa kijeshi wa kimkakati. Jambo ambalo lililazimisha Urusi kuzituma ndege zake kumi na nne za kivita hadi Libya mashariki. Pentagon ilisema haya katika juhudi za kumsaidia Haftar na kutuma onyo kwa Uturuki.

Lakini wakati huo huo mamluki wa Urusi walijiondoa kutoka katika safu za mbele katika uwanja wa mapambano na kuelekea kwenye ngome ya Haftar iliyopo mashariki, huku wakiviacha vikosi vya jeshi la Haftar katika hatari mbaya katika mji wa Tripoli.  Na kupelekea GNA kuitumia fursa hiyo.

Uturuki na Urusi wanafanya kazi kulingana na mpango mkakati wa Amerika juu ya Libya. Kama vile ambavyo wamekuwa wakishirikiana katika mipango ya Amerika juu ya Syria.

Waislamu hawatafurahia amani, utulivu, haki na heshima hadi pale tutakapoisimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itawatoa makafiri mabepari wa kigeni katika ardhi za Waislamu na kuwaondoa vibaraka watawala ambao wameusaliti ummah kila mara.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 14 Julai 2020 12:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu