Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali:

Kazi ya Hizb Itakuwa ni ipi Baada ya Kusimamisha Dola ya Khilafah Rashidah ya Pili?

Kwa Abu Muso.

Swali:

Assalam Alaikum Ewe Amiri wetu, vipi hali yako? Wakati dola ya Kiislamu itakaposimamishwa, Hizb ut Tahrir itaenda kwenye marhala (hatua) gani? Baadhi ya watu wanasema: itaendelea kama ilivyo katika marhala ya tatu na wengine wasema: itakapohamia kwenye utawala basi marhala ya tatu itakuwa imeisha, na Hizb itaanza kazi nyengine kabisa, nayo ni kuwahisabu watawala na kuisimamia jamii… kauli ipi ndio sahihi na yenye nguvu zaidi?

Jibu:

Wa Alaikum Salaam wa Rahmatullahi wa Barakaatuh.

Tulitaja katika kitabu cha utambulisho haya yafuatayo:

[8- Njia ya hizb ut tahrir:

njia ya kubeba daawa ni hukmu za kisheria, huchukuliwa kutoka kwenye njia ya Mtume (saw) katika ubebaji wake wa daawa, kwa sababu yeye ni wajib kufuatwa. kwa neno lake Mwenyezi Mungu (swt):

(لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا)

"Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana." [Al-Ahzab: 21]

Na neno lake:

(قُلْ إِنْ كُنْتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ)

"Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu." [Aali-Imran: 31]

Na kwa neno lake:

(وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا)

"Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu." [Al-Hashr: 7] Na aya zengine nyingi zinazojulisha ulazima wa kumfuata Mtume (saw) na kumuiga na kuchukua hukmu kutoka kwake.

Kwa kuwa Waislamu leo wanaishi ndani ya daarul kufr, kwa sababu wanahukumiwa na sheria zisizokuwa za Mwenyezi Mungu (swt), hivyo basi ardhi zao zafanana na Makkah wakati akitumilizwa Mtume (saw), kwa hiyo yalazimu kipindi cha Makkah kufanywa ndio mahala pa kufuatwa.

Na mtu yeyote anapofuatilia mwenendo wa Mtume (saw) alipokuwa Makkah hadi aliposimamisha serikali madina, atabainikiwa kwamba Mtume alipitia hatua zenye alama za wazi. Alikuwa katika hatua hizo akifanya matendo maalumu ya wazi. Kwa hiyo Hizb ikachukua njia na mwendo wake hapo, na matendo ambayo ni lazima yafuate, kwa ajili ya kuiga matendo ya Mtume (saw) ambayo alikuwa akifanya katika hatua za mwendo wake.

Ni kutokana na hayo, ndio maana Hizb ikaweka njia ya mwendo wake kwa hatua (marhala) tatu:

Hatua ya Kwanza: hatua ya kuelimisha kwa lengo la kutengeza watu wanaoamini fikra ya Hizb na njia yake, ili kuunda kundi (chama)

Hatua ya Pili: hatua ya maingiliano na Ummah, kwa lengo la kuubebesha Uislamu, ili uufanye Uislamu ndio kadhia yake, ili ufanye kazi ya kuutabikisha katika maisha.

Hatua ya Tatu: hatua ya kuchukua utawala na kutekeleza Uislamu, utekelezaji kamili na jumla, na kuubeba kama ujumbe kwa ulimwengu.

Ama Hatua ya Kwanza: Hizb iliianza huko Al Qudsi mwaka wa 1372 H - 1953 M mkononi mwa muasisi wake, mwanachuoni mtukufu, na mwanafikra mkubwa, na mwanasiasa mwenye cheo, na kadhi katika mahkama ya rufaa quds: Ustadh Taqiyyudin An-Nabahani Mwenyezi Mungu amrahamu. Na Hizb ilikuwa ikifanya kazi ya kuwasiliana na watu mmoja mmoja katika Ummah, ikiwapa fikra na njia yake kila mmoja kivyake. Na waliokuwa wakiikubali Hizb huwaweka kwenye vikao vya masomo endelevu, hadi watakapo yeyuka kwa fikra za Uislamu na hukm zake ambazo Hizb imetabanni, na hatimaye kuwa na utambulisho wa Kiislamu, awe akitekeleza Uislamu na kuwa na aqliyya na nafsiyyah ya Kiislamu, na kuanza kubeba ulinganizi kuwafikishia watu. Mtu anapofikia kiwango hiki hujilazimisha kwa Hizb, na Hizb humuunga na wanachama wake, kama alivyokuwa akifanya Mtume (saw) katika marhala yake ya kwanza ya ulinganizi ambayo iliendelea kwa miaka mitatu akiwalingania watu mmoja mmoja, akiwaonyesha yale ambayo Mwenyezi Mungu alimtuma nayo. Na aliomuamini alikuwa akimuunga kisiri juu ya msingi wa hii dini, na hufanya pupa ya kumfunza Uislamu na kumsomesha aliyoteremshiwa katika Quran, mpaka alipowayeyusha kwa Uislamu. Na alikuwa akikutana nao kwa siri, na kuwafundisha kwa siri, kwenye maeneo yasiyokuwa wazi. Na walikuwa wakitekeleza ibada zao kisirisiri. Kisha utajo wa Uislamu ukaenea hapo Makkah na watu wakauzungumza, na wakaingia mmoja mmoja.

Na baada ya Hizb kuweza kuunda chama, na jamii kuihisi na kuijua na kutambua fikra zake na yanayolingania, hapo Hizb ikahamia:

Hatua ya Pili: nayo ni atua ya kuingiliana na Ummah ili kuwabebesha Uislamu, na kutengeneza uelewa na rai jumla kwao juu ya fikra za Kiislamu na hukmu zake ambazo Hizb imetabanni, mpaka wazifanye ni fikra zao, ambazo watazifanyia kazi ili zipatikane katika maisha. Na ili waende pamoja na Hizb katika kusimamisha serikali ya Khilafah na kumuweka khalifah ili kuanzisha upya maisha ya Kiislamu, na kubeba ujumbe wa Uislamu kuwapelekea walimwengu. Na ni katika hatua hii ndipo Hizb ilihamia kuwazungumzia watu mazungumzo ya pamoja. Na ikawa katika hatua hii ikitekeleza matendo yafuatayo:

  1. Utoaji endelevu wa thaqafa kwenye halaqat kwa watu mmoja mmoja, ili kukuza mwili wa Hizb na kukithirisha wafuasi wake, na kuunda wenye utambulisho wa Kiislamu watakaoweza kubeba ulinganizi, na kuingia kwenye nyanja za mivutano ya kifikra na mapambano ya kisiasa.
  2. Utoaji wa thaqafa ya pamoja kwa mikusanyiko ya Ummah, na kuwapa fikra za Kiislamu na hukmu zake ambazo Hizb imezitabanni, kwenye darsa za miskitini na mbarazani, mihadhara na katika maeneo ya mikusanyiko jumla, na kupitia magazeti, vitabu, na vipeperushi ili kujenga uelewa jumla kwa Ummah na kuingiliana nao.
  3. Mivutano ya kifikra dhidi ya imani za kikafiri, serikali zake na fikra zake, na imani mbovu, fikra za makosa, na dhidi ya fahamu zilizoharibiwa. Kwa kubainisha makosa yake na zinavyogongana na Uislamu. Kwa lengo la kuunasua Ummah kutokana nazo na kutokana na athari zake.
  4. Mapambano ya kisiasa …

Na pindi jamii ilipoganda mbele ya Hizb, kutokana na Ummah kukosa imani na viongozi wao ambao ndio waliokuwa tumaini lao, na kutokana na mazingira magumu ambayo yamewekwa katika maeneo haya ili kupitisha mikakati ya njama fiche na kwa sababu ya ukandamizaji wa watawala dhidi ya raia wao, na kwa sababu ya maudhi makali yanayofanywa na watawala dhidi Hizb na mashababu wake, kwa huo mgando na kwa sababu zote hizo ndipo Hizb ikaanza kuomba nusra kutoka kwa wenye uwezo

Na pamoja na Hizb kutekeleza hizo kazi za kuomba nusra, pia iliendelea kufanya matendo yote ambayo ilikuwa ikifanya kabla, kama vile: masomo ya umakinifu ndani ya halaqa, utoaji thaqafa ya pamoja, na kumakinikisha Ummah ili kuubebesha Uislamu na kutengeza rai jumla kwao, pia kuendelea kupambana na dola za kikoloni za kikafiri na kufichua mikakati yao, na kufedhehi njama zao, pamoja na kugongana na watawala, na kubeba maslahi ya Ummah na kuchunga mambo yao.

Hizb ni yenye kuendelea na yote hayo, huku ikitarajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwatimizia wao pamoja na Ummah wa Kiislamu mafanikio na ushindi, ili ifikie:

Hatua ya Tatu: ambapo itasimama Khilafah Rashidah na hapo watafurahi waumini kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu ]. (mwisho wa nukuu kutoka kwenye kitabu cha utambulisho).

Kwa hiyo: hizo hatua tatu ni pale ambapo dola haipo, hivyo kazi ya Hizb huwa ni kutekeleza faradhi ya hizo hatua tatu… ama wakati dola inaposimama, basi yale yote ambayo yalikuwa na uhusiano na usimamishaji wa dola hayatokuwa tena katika kazi za Hizb. Kwa mfano: uombaji nusra mwishoni mwa hatua ya pili ili kusimamisha dola, hilo halitakuwepo tena. Vivyo hivyo, hatua ya tatu yaani, usimamishaji dola, yote hayo hayatokuwepo tena, kwa sababu itakuwa dola ishasimama tayari. Bali badili ya hayo yote itakuwa ni kumhesabu mtawala kwa mujibu wa dalili za kisheria… ama marhala zengine zilizobakia, hizo zitaendelea kwa nguvu zaidi na uchangamfu mkubwa. Kwa sababu, baada ya kusimama dola uadilifu utachukua nafasi ya dhulma zilizotangulia, na itaandaa mazingira bora ya kazi za Hizb, badala ya kule Hizb kuandamwa kwa ukali. Na naam kweli wakati huo waumini watafurahi kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu.

Na tumeshabainisha katika vitabu vyetu, na hasa kwenye kitabu cha “Kurrasah” namna ya kuhesabu watawala kwa mujibu wa hukmu za kisheria…Haya yanatosha, Na Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mjuzi na Mwenye Hekima zaidi.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

 01 Dhu al-Hijjah 1442 H

11/07/2021 M

Link ya Jibu hili katika ukurasa wa Amiri (Mwenyezi Mungu amhifadhi) wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu