Jumapili, 17 Rabi' al-awwal 1448 | 2026/08/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Je, Erdogan Anasubiri Mayahudi Waipige Mabomu Ankara Kabla ya Kuhamasisha Jeshi Lake?!

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, katika hotuba aliyotoa wakati wa mkutano wa kundi la wabunge wa Chama cha Haki na Maendeleo katika Bunge la Uturuki, alisema: "Tunafahamu vyema lengo kuu la udanganyifu wa 'Ardhi iliyo Ahidiwa', na Mungu akipenda, hatutaruhusu kamwe." Alifafanua kwamba usalama wa Uturuki hauanzii katika mkoa wa Hatay kusini mwa Uturuki, bali Aleppo, Damascus, na Beirut. Aliendelea: "Ikiwa uonevu wa Israel hautasimamishwa, gharama haitalipwa na eneo hilo pekee, bali na wanadamu wote." Erdoğan alizisihi dola kuu duniani kuchukua msimamo wazi dhidi ya umbile hilo la Kizayuni, akisema: "Kuirudisha Israel katika kufuata sheria sio tena jukumu la baadhi ya nchi tu, bali ni jukumu la pamoja linalowaangukia wanadamu wote."

Soma zaidi...

Mtoto Aliyeuawa Shahidi, Kuhesabiwa kwa Waathiriwa Kutaisha Lini? Watu wa Damu hiyo Watainuka Lini Kuwalipiza Kisasi?

Wizara ya Afya ya Palestina ilisema kwamba vikosi vya uvamizi vilifyatua risasi kwenye gari moja lililokuwa limebeba raia wa Palestina katika mji wa Hebron katika Ukingo wa Magharibi wa kusini unaokaliwa kimabavu, na kusababisha kifo cha kishahidi cha mtoto mchanga wa miezi saba Sam Abu Hikal huku akiwa mikononi mwa mamake. Mamake na babake pia walijeruhiwa.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria na Kushiriki katika Kikao cha Kadhia za Umma

Tunafuraha, kama Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wote walio na hamu na masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika Kikao cha kila mwezi cha Kadhia za Umma, ambacho mwezi huu kitafanyika katika afisi ya Hizb jijini Khartoum baada ya kukatizwa kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na vita.

Soma zaidi...

Jibu kwa Mwandishi wa Makala (Usekula na Ugumu wa Historia ya Uislamu Iliyoghushiwa)

Uislamu ni itikadi ya kiroho na kisiasa ambayo ilikuja kushughulikia matatizo ya wanadamu, kwa kutambua kwamba wanadamu wana silika (ghariza) na mahitaji ya kimwili ambayo yanahitaji kushibishwa. Uislamu umebainisha jinsi mahitaji haya yanavyopaswa kukidhiwa bila ya ziada au upungufu, kupitia hukmu kutoka kwa Mwenye hekima, Mjuzi wa yote. Yeye aliyewaumba wanadamu anajua kipi kuna manufaa na kipi kina madhara kwao! Ukosefu wa elimu wa mwandishi juu ya hukmu hizi haumwondolei jukumu; badala yake, unasisitiza kutoujua kwake Uislamu.

Soma zaidi...

“KL Headline Msimu wa 2026”: Serikali ya Madani Haijali tena Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu!

Kuala Lumpur iko tayari kuibuka kama mahali mwanana pa ziara za matamasha ya kimataifa barani Asia kupitia “KL Headline Msimu wa 2026,” ambao unakutanisha maonyesho 25 ya wasanii wa kimataifa katika mwaka mzima wa 2026. Mji mkuu wa Malaysia umepangwa kuwa mwenyeji wa maonyesho 25 ya wasanii wa kimataifa katika maeneo sita, yakiwalenga zaidi ya mashabiki 500,000 kutoka pwani za ndani na nje ya nchi - kulingana na mratibu, Live Nation Malaysia.

Soma zaidi...

Enyi Ummah wa Kiislamu na Majeshi Yake: Ikiwa Hamkasirishwi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mambo Yake Matakatifu, Basi Mtakasirishwa na Kuchukua Hatua kwa ajili ya Nini?!

Mnamo Jumatano, 27/5/2026, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vilirusha picha zinazoonyesha vikosi vya umbile la Kiyahudi vikimshambulia kikatili mwanamke mchanga wa Kipalestina huko Bab Hutta, moja ya malango ya Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, vikimnyang'anya kitambaa chake cha kichwani kwa nguvu kabla ya kumkamata. Tukio hili linajiri huku kukiwa na ongezeko la ukiukwaji wa sheria na hatua za usalama ulioongezeka kutoka kwa vikosi vya uvamizi katika milango ya kuingia katika Jiji la Kale la Al-Quds na malango ya Msikiti wa Al-Aqsa, sanjari na Idd al-Adha. Waliweka vituo vya ukaguzi na kuchunguza vitambulisho vya wapita njia, wakizuia idadi kubwa ya watu kuingia msikitini.

Soma zaidi...

Vikosi vya Msaada wa Haraka Vinafanya Mauaji Dhidi ya Watu Wasio na Silaha, na Serikali Haiwezi Kuwalinda!

Mnamo Alhamisi na Ijumaa, Mei 28 na 29, 2026, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilizindua mashambulizi kwenye vijiji vilivyo magharibi mwa mji wa Bara katika Jimbo la Kordofan Kaskazini, na kusababisha vifo vya raia kadhaa wasio na silaha. Mtandao wa Madaktari wa Sudan ulithibitisha katika taarifa mnamo Ijumaa, Mei 29, 2026, kwamba RSF ilifanya mauaji makubwa katika mji wa Al-Marra na vijiji vinavyozunguka, na kuwaua raia 27. Katika ripoti yake ya hivi karibuni mnamo Jumamosi, Mei 30, 2026, Al-Arabiya TV ilisema: “Idadi ya vifo kutokana na mauaji ya Vikosi vya Msaada wa Haraka katika eneo la Al-Marra huko Kordofan Kaskazini imeongezeka hadi 58.” Wakati Vikosi vya Msaada wa Haraka vinafanya mauaji haya katika vijiji vya Kordofan, serikali inalaani tu na kuhesabu waliokufa, bila kuchukua hatua zozote kali kuzuia mauaji haya kutokea.

Soma zaidi...

Ulaya Yahangaika Siku Chache Tu Bila Mafuta na Gesi ya Waislamu: Vipi Basi Ikiwa Ummah Ungeamka?!

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Roland Lescure alisema kwamba serikali haziwezi kuamua kama zitoe akiba ya ziada ya mafuta ya kimkakati ili kupunguza usumbufu unaosababishwa na vita vya Iran hadi muda unaowezekana wa mzozo huo utakapokuwa wazi. Katika muktadha huo huo, mashambulizi ya awali ya makombora ya Iran kwenye kituo cha gesi cha Ras Laffan nchini Qatar, mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya gesi asilia vilivyoyeyushwa duniani, yalisababisha kupungua kwa kasi kwa akiba ya gesi ya Uingereza. Akiba ya gesi asilia nchini Uingereza ilishuka hadi viwango vya kutosha kukidhi matumizi ya ndani kwa muda usio zidi  masaa 48.

Soma zaidi...

Ufisadi wa Mfumo Huzalisha Ufisadi katika Masuluhisho Sera ya Ufukarishaji: Zawadi ya Idd al-Adha kutoka kwa Watawala kwa Watu wa Yemen

Serikali ya Shaea Al-Zandani mnamo Jumanne, 19/05/2026, ilianzisha hatua mpya ya kiuchumi ambapo ilipandisha bei ya dolari ya ushuru wa forodha kwa zaidi ya 100%, kutoka riyali 750 hadi riyali 1,550, na kuongeza bei ya chombo cha dizeli cha lita 20 kwa 24.5%, ikiruka kutoka riyali 29,500 hadi 36,000. Kisha ilijaribu kuwaziba macho watu wa Yemen kwa kuidhinisha posho ya gharama ya maisha ya 20% kwa wafanyikazi wa sekta ya umma, pamoja na kuwapa nyongeza yao ya kila mwaka inayostahili kwa miaka ya 2021-2024, na kufanya marekebisho ya viwango vya kazi ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa zaidi ya miaka 13.

Soma zaidi...

Salamu za Idd Idd ni Wakati Ambapo Furaha na Huzuni Zinaunganishwa!

Siku hizi Idd al-Adha inafika, ambapo furaha na huzuni zimechanganyika. Furaha katika mwitikio wa waumini kwa wito wa Mwenyezi Mungu wa Hijja, wakiitikia wito wake katika mkusanyiko unaowaunganisha kutoka pembe zote za dunia, pamoja na makabila na rangi zao mbalimbali, kwa kutii amri ya Mwenyezi Mungu na kupata radhi Zake. Na huzuni kubwa inawakumba nyoyo zao kwa masaibu yao tangu kupoteza nguvu yao na kuvunjwa kwa dola yao mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Ni Idd ya aina gani huku Gaza ikiendelea kutokwa na damu?! Idd ya aina gani huku kambi na meli za kivita za maadui wa Umma zikiwa katikati ya ardhi zake?! Idd ya aina gani huku wanawake huru wa Waislamu wakidhalilishwa huko Palestina, Turkestan Mashariki, Myanmar, na India?!

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu