Alhamisi, 05 Rajab 1447 | 2025/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir Mwalimu Ustadh Ahmad Muhammad Al-Saharin (Abu Khalid)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Jordan inaomboleza kifo cha mwalimu mtukufu, Ustadh Ahmad Muhammad Al-Saharin (Abu Khalid), mwanachama wa Hizb ut Tahrir, aliyefariki Jumatano, 10 Disemba 2025, akiwa na umri wa miaka 79. Alikuwa miongoni mwa wabebaji da’wah wa muda mrefu na anayejulikana sana huko Tafila.

Soma zaidi...

Bajeti za Jordan Ni Nakala Zinazorudiwa katika Ufisadi Wao na Kuzishughulikia Kupitia Madeni Kuna Wiana na Dori ya Kiutendaji ya Serikali na Haijali Uchungaji wa Mambo ya Watu

Serikali ilikadiria, katika Rasimu ya Sheria ya Bajeti Kuu ya mwaka 2026, mapato ya umma yangekuwa takriban dinari bilioni 10.931, 75% kati yake yakiwa ni kutokana na kodi, na dinari milioni 735 kutoka kwa ruzuku za kigeni. Waziri wa Fedha alisema kwamba kiasi cha matumizi ya sasa ni dinari milioni 11,456, huku matumizi makuu yakifikia dinari milioni 1,600 pekee. Kuhusu nakisi inayotarajiwa kwa mwaka 2026, inakadiriwa kufikia takriban 4.6% ya Pato la Taifa.

Soma zaidi...

Je, Vituo vya Mafuta Vina Thamani Zaidi na Hadhi Kubwa Zaidi kuliko Watu?!

Imeripotiwa katika habari kwamba Vikosi vya Ulinzi vya Wananchi wa Sudan Kusini vilianza kupeleka vikosi vyake kulinda Uwanja wa Mafuta wa Heglig kufuatia makubaliano ya pande tatu kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Uhuru la Utawala la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, na kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo. Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Sudan Kusini, Paul Nang, alielezea katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ndani ya uwanja wa mafuta wa Heglig kwamba makubaliano hayo yalibainisha kuondolewa kwa jeshi na kuondoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka kutoka eneo hilo, na alithibitisha kwamba lengo la makubaliano hayo lilikuwa kuhakikisha kwamba hakuna hujuma yoyote inayotokea kwenye vituo vya mafuta!!

Soma zaidi...

Vita vya Amerika dhidi ya Uislamu

Utawala wa Marekani na watoaji maamuzi ndani yake hawaachi kuonyesha uadui wao dhidi ya Uislamu na kufichua vita vyao vinavyoendelea na anuwai dhidi yake. Katika kila tukio na bila ya tukio, utamsikia afisa wa Marekani akipaza sauti yake kuushambulia Uislamu, akiuelezea kwa maelezo yanayofichua ukubwa wa chuki yao dhidi yake na kuashiria ukubwa wa utisho unaojaza nyoyo zao kutokana na Uislamu.

Soma zaidi...

Mamlaka ya Kihalifu ya Palestina, ikiwemo Wizara ya Masuala ya Wanawake, Yakimbilia Kutekeleza Miradi ya Maadui wa Uislamu ya Kuharibu Familia, Kuvunja Jamii, na Kumponda Mwanamke wa Kiislamu Anayezaa Mashujaa

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Masuala ya Wanawake ilifichua kwamba Wizara hiyo ilifanya warsha pamoja na Kamati ya Mpito ya Kuandika Katiba ili kujadili sifa za kuzifanyia kazi kwenye rasimu ya katiba na kuingiza masuala ya wanawake katika vifungu vyake. Kulingana na taarifa hiyo: “Kwa ushiriki mpana kutoka kwa taasisi rasmi na za kiserikali, taasisi za wanawake na haki za binadamu, na mashirika ya kiraia, na kwa uhudhuriaji mkubwa kutoka kwa viongozi wanawake wa Kipalestina walioko ughaibuni nchini Syria, Jordan, Lebanon, Misri, na Ulaya, Wizara ya Masuala ya Wanawake ilifanya warsha pana ya kitaifa kwa ushirikiano na Kamati ya Mpito ya Kuandika Katiba ya Palestina, kama sehemu ya kuimarisha mazungumzo ya kitaifa kuhusu kuandika katiba inayoakisi matarajio ya watu wa Palestina na kuhakikisha uwepo changamfu wa masuala ya wanawake katika maudhui yake.”

Soma zaidi...

Chuo Kikuu cha Al-Quds Kinafanya Kongamano kwa Ufadhili wa Magharibi na Programu Iliyoundwa na Magharibi Chini ya Kauli Mbiu “Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake”

Mnamo Jumanne, 2 Disemba 2025, Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Al-Quds – Abu Dis kilizindua kongamano la kimataifa lililopewa kichwa “Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake: Changamoto, Masuluhisho, na Mbinu Bora katika Eneo la Mediterania,” kwa ushirikiano na Wizara ya Masuala ya Wanawake ya Palestina, Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kupambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake, Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), na Chuo Kikuu cha Perugia, Italia, kwa usaidizi wa ushirikiano wa Italia.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kwa nyoyo zilizoridhika na amri ya Mwenyezi Mungu, macho yanayobubujika machozi, na huzuni kubwa, inaomboleza mmoja wa mashababu wake aliyebeba ulinganizi wa kuregesha maisha kamili ya Kiislamu; kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, Mwenyezi Mungu amsamehe: Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Soma zaidi...

Mapambano Dhahiri ya Kikoloni huko Hadramawt juu ya Mafuta Na Kuegemea Upande Wowote Ni Hasara Katika Dunia Hii na Akhera

Mnamo Jumamosi, 29/11/2025, vikosi vya jeshi vya Kikosi cha Ulinzi cha Hadramawt chenye uhusiano na Amr bin Habrish Al-Ali viliingia katika vituo vya mafuta vya Petro Masila katika Bonde la Hadramawt, vikinyanyua kauli mbiu ya kulinda vituo vya mafuta, huku vikiwaondoa wale waliokuwa hapo vikosi vya kawaida vya jeshi vilivyokuwa na uhusiano na Baraza la Octet.

Soma zaidi...

Mauaji ya Pilkhana Yalikuwa Njama ya India ya Kudhoofisha Jeshi la Nchi hii - Ripoti Hii ya Tume Huru ya Uchunguzi ya Kitaifa Imethibitisha Ukweli ambao Hizb ut Tahrir Iliuwasilisha kwa Taifa kwa Ujasiri Miaka Kumi na Sita Iliyopita. Tunatoa Wito Ten

Tume Huru ya Kitaifa ya Uchunguzi iliyoundwa na serikali ya mpito kuhusu mauaji ya Pilkhana, na kusababisha vifo vya maafisa 57 wenye sifa nzuri, yaliyotokea katika Makao Makuu ya BDR mnamo Februari 25 na 26, 2009, imetoa ripoti yake ya uchunguzi. Uchunguzi umethibitisha kuhusika kwa Hasina na washirika wake Tapas na wengineo katika kutekeleza njama ya India ya kudhoofisha jeshi la nchi hii. Tunataka sana adhabu ya haraka kwa wahalifu hawa waliohusika katika tukio hilo na kutangazwa kwa India kama dola adui. Lazima mukumbuke kwamba chama cha kisiasa chenye busara na ikhlasi, Hizb ut Tahrir, kilikuwa cha kwanza kuleta ukweli huu kwa ujasiri kwa taifa

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu