Jumanne, 07 Sha'aban 1441 | 2020/03/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Namna gani Waislamu Walizishughulikia Bishara za Mtume (saw)?

Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara mbalimbali kwa Waislamu zilizowahamasisha kutenda kazi na kuwa na hakika ya kupata ushindi; baadhi yake zimetimizwa na baadhi bado hazijatimizwa. Miongoni mwa bishara zilizo fanikishwa: Kutoka kwa Al-Bara’ Bin Athib (ra), alisema:

«لَمَّا كَانَ حِينُ أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِحَفْرِ الْخَنْدَقِ عَرَضَتْ لَنَا فِي بَعْضِ الْخَنْدَقِ صَخْرَةٌ لَا تَأْخُذُ فِيهَا الْمَعَاوِلُ، فَاشْتَكَيْنَا ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم، فَجَاءَ فَأَخَذَ الْمِعْوَلَ فَقَالَ: بِسْمِ اللَّهِ. فَضَرَبَ ضَرْبَةً فَكَسَرَ ثُلُثَهَا، وَقَالَ: اللَّهُ أَكْبَرُ أُعْطِيتُ مَفَاتِيحَ الشَّامِ، وَاللَّهِ إِنِّي لَأُبْصِرُ قُصُورَهَا الْحُمْرَ السَّاعَةَ. ثُمَّ ضَرَبَ الثَّانِيَةَ فَقَطَعَ الثُّلُثَ الْآخَرَ فَقَالَ: اللَّهُ أَكْبَرُ، أُعْطِيتُ مَفَاتِيحَ فَارِسٍ، وَاللَّهِ إِنِّي لَأُبْصِرُ قَصْرَ الْمَدَائِنِ أَبْيَضَ. ثُمَّ ضَرَبَ الثَّالِثَةَ وَقَالَ: بِسْمِ اللَّهِ، فَقَطَعَ بَقِيَّةَ الْحَجَرِ فَقَالَ: اللَّهُ أَكْبَرُ أُعْطِيتُ مَفَاتِيحَ الْيَمَنِ، وَاللَّهِ إِنِّي لَأُبْصِرُ أَبْوَابَ صَنْعَاءَ مِنْ مَكَانِي هَذَا السَّاعَةَ»

 “Wakati Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) alipotuamrisha tuchimbe handaki, kukawa na mwamba katika handaki ambao hatukuuweza kuuvunja kwa sururu zetu, tukatoa taarifa kwa Mtume (saw), Mtume (saw) akachukua sururu na kutamka: Kwa jina la Mwenyezi Mungu akapiga na kuvunja thuluthi moja ya mwamba, na akasema: Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa), Nimekabidhiwa funguo za Ash-Sham; naapa kwa Mwenyezi Munbu nayaona makasri mekundu hivi sasa. Kisha akapiga mara ya pili, na kuvunja thuluthi ya pili, na akasema: Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa), nimepewa funguo za Fursi; naapa kwa Mwenyezi Mungu nayaona makasri yake meupe ya Mada’in. Kisha akapiga mara ya tatu na akasema: Kwa jina la Mwenyezi Mungu na akavunja sehemu iliyobaki ya jiwe, na akasema: Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) nimepewa funguo za Yemen, naapa kwa Mwenyezi Mungu naiona milango ya Sanaa, kutokea hapa nilipo hivi sasa” (Fath al-Bari kutoka kwa Ibn Hajar).  

Bishara hii inayoelezea juu ya ueneaji wa ushindi wa Uislamu, uliofanikishwa katika kipindi cha Khilafah Rashidah ya kwanza kwa njia ya Utume, bishara iliyotajwa wakati Waislamu wamezingirwa katika mji huku wakikumbana na dhiki, hofu, njaa na baridi kali. Baada ya Mtume (saw) kufariki, Waislamu waliendelea kufuata njia waliyochorewa na Mtume (saw). Khalifah wa Waislamu alikuwa ndio Imamu wao, akiwatawala kwa sheria za Mwenyezi Mungu na akiwaongoza katika Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), hivyo majeshi yake ya kikatiza ardhi kame na mashua zao zikisafiri baharini kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kueneza uadilifu ulimwenguni kote, kuzitimiza bishara moja baada ya nyingine.

Na katika masiku haya, kumbukumbu za kukombolewa Kostantinopoli zinatupitia. Imetajwa katika hadithi:

Kutoka kwa Abdullah ibn Amr ibn Al-As, alisema: “Tulipokuwa pamoja na Mtume (saw) tunaandika, Mtume (saw) akaulizwa, ni upi kati ya miji miwili utakombolewa mwanzo, Konstantinopoli au Roma? Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلاً، يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ»

  “Mji wa Heraclius utakombolewa mwanzo, yaani Kostantinopoli”

Ahmad ameisimulia hii katika mapokezi yake na Al Hakm katika Al-Mustadrak aliisemea: “Hadithi hii ni sahih juu ya masharti ya Mashekh wawili (Bukhari na Muslim)”. Pia katika hadith iliyopokewa na Abdullah ibn Bishr Al-Khathaami kutoka kwa Baba yake kuwa alimsikia Mtume (saw) akisema:

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Mtaifungua Kostantinopoli, Amiri bora ni Amiri huyo na jeshi bora ni jeshi hilo” [Imepokewa na Ahmad na Al-Bazzar]

Hebu tusite kwenye bishara ya kukombolewa Kostantinopoli na jinsi Waislamu walivyo shindana juu ya kutimiza bishara hii, basi jaribio la kwanza la kuikomboa Kostantinopoli lilikuwa mwaka wa 49 Hijiria, sawa na mwaka 669 Miladia, wakati wa Khilafah ya Muawiyah ibn Abi Sufyan. Alituma jeshi kubwa la ardhini ili kuuzingira mji, lililoongozwa na Fadhala bin Ubayd Allah al-Ansari, ambaye alipenya na Jeshi ndani ya ardhi ya Baizantino hadi kufika kwa Chalcedonia karibu na mji mkuu wa Roma. Alibakia huko katika kipindi cha baridi kali cha mwaka huo katika maeneo ya himaya yao na Muawiyah aliwapatia mahitaji na msaada. Mahitaji haya yakiongozwa na Sufyan bin Auf aliyetekeleza mzingiro wa mji wa Baizantaino [Ibn al-Athir al-Jazari, Abu al-Hasan Ali bin Abi al-Karam al-Shaibani. The Complete History (2nd ed.). Beirut - Lebanon: Lebanese Book House. Ukurasa 227.] Hata hivyo Waislamu hawakuweza kupata ushindi wa wazi, na wakalazimika kuvunja mzingiro na kurudi Damascus. Sahaba Abu Ayub al-Ansari, aliyekuwemo kwenye jeshi la Fadhala, alifariki katika vita hivi na kuzikwa katika kuta za mji wa Kostantinopoli. [Ibn Khayyat Al-Leithi, Abu Amr bin Abi Hurairah Khalifa. Uchunguzi wa Akram Dhia Al-Omari, mchapishaji. Historia ya Khalifa Bin Khayat (1st ed.). Najaf Al Ashraf-Iraq ukur. 197]

Baadaye Waislamu walirejelea jaribio la kuiteka Kostantinopoli kipindi cha utawala wa Khalifah Sulayman ibn Abd al-Malik mwaka wa 98 Hijiria sawia na mwaka 717 Miladia.

Kwa kuongezea majaribio yaliyotajwa, kulifanyika majaribio kadhaa ambayo hayakufikia kwenye mji wenyewe bali yaliishia katika vitongoji vyake. Baadhi ya wanahistoria wameiweka kuwa ni miongoni mwa majaribio ya Waislamu kufungua mji wa Kostantinopoli, ni pamoja na kampeni ya Khalifah wa Abbasiyah Harun al-Rashid kutoa adhabu kwa Mfalme wa Roma, Naqfour wa kwanza, ambapo aliweza kuifungua Hergla kitongoji cha Kostantinopoli. Kisha kulifanyika majaribio mengine ya Dola ya Uthmaniya kabla ya utawala wa Muhammad al-Fatih, lakini hayakuweza kutimiza bishara hiyo.

Katika masiku hayo al-Fatih alianza kuivamia na kuizingira Kostantinopoli kutokea tarehe ishirini na sita ya mwezi wa Rabi’al-Awwal hadi ilipofunguliwa muda wa mapambazuko ya tarehe ishirini ya Jumanne ya mwezi huu, Jumada al-Awwal 857 Hijria; hivyo ndivyo ilivyokuwa, mzingiro ulidumu kwa miezi miwili. Wakati Muhammad al-Fatih alipoingia mjini hali ya kuwa ni mshindi, alishuka katika farasi wake na kusujudu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi na mafanikio, na hivyo bishara hii ilitimia chini ya mikono ya kijana huyu mdogo, Muhammad al-Fatih aliyekuwa na umri usiozidi miaka ishirini na moja, lakini alitayarishwa kwa malezi mazuri tokea utotoni mwake; baba yake Sultan Murad II alimlea, na kusomeshwa na wanachuoni wazuri wa kipindi hicho, kama vile Ahmed bin Ismail al-Kurani, ambaye alitajwa na al-Suyuti kuwa ndiye mwalimu wa kwanza wa al-Fatih, na kumuelezea kuwa “Alikuwa mwanachuoni wa fiqhi, ambapo wanachuoni wa wakati wake walishuhudia ukubwa na umahiri wake, hadi kumuita kuwa ni: Abu Hanifa wa kipindi chake.” Pia, Sheikh Akshamsuddin Sunqar, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpandikiza akilini mwake hadithi ya Mtume (saw) tokea utotoni mwake juu ya “kufunguliwa kwa Mji wa Kostantinopoli.” Kijana huyu alikulia akiwa na lengo la kufanikisha ukombozi huo kwa mikono yake.

Hao ndio walikuwa Waislamu wa kwanza wakiwa na Khalifah wao na majeshi yao. Walikuwa wakishindana kwa dhamira ya dhati na jitihada ya kutimiza bishara ya Mtume (saw), na huo ndio utukufu wa Uislamu na Waislamu pale Uislamu unapotekelezwa kivitendo katika dola na jamii. Leo hii, ni nani atakayeshinda heshima ya kujiunga na msururu huu na kukamilisha bishara zilizobakia za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw); kusimamisha Khilafah ya Uislamu, kupigana na Mayahudi, na kuifungua Roma? Je (bishara hii) itafikiwa na mtawala anayeomba ridhaa na upendo kutoka Amerika? Au kwa mtawala anayeshindania mapenzi ya Mayahudi? Au mtawala dikteta, dhalimu na asiye na maadili anayetawala kwa sheria zisizokuwa za Kiislamu? Au mtawala anayehiyarisha sheria za kikafiri (kitwaghuti) na kijahiliya dhidi ya sheria za Mwenyezi Mungu, Bwana wa Ulimwengu? Au mtawala kibaraka aliye na umiliki juu ya watu, asiye heshimu udugu wala mkataba baina yao?

Baada ya kuangushwa kwa utawala wa Khilafah Uthmaniya mnamo Machi 03, 1924 Miladia, nchi za Waislamu zikawa ni shabaha rahisi ya makafiri wakoloni, wakaleta maangamizi makubwa duniani, na kuharibu nchi na vizazi. Wakazigawa ardhi za Waislamu na kuwa vijinchi dhaifu, vyenye maumbo yasiyokuwa na mamlaka ya kiukweli, na kwenye kila umbo wamechagua genge la watu miongoni mwetu wanaozungumza kwa lugha yetu. Wanaburuza nchi kwa ajili ya mabwana zao, hupiga nyuso za watu kwa viboko kama mikia ya ng’ombe, huajiri askari kwa kulinda nyadhifa zao, huuaa roho nyingi, hufungua magereza mengi na makubwa, wanaharibu akili za watu kwa fikra zao mbaya zilizopitwa na wakati, na kutengeneza kizazi kisichojua chochote isipokuwa utiifu kwa familia ya watawala, chama tawala, au anayetawala.

Hii ndio hali ya watawala katika nchi za Waislamu hivi leo, na tunaapa kwa Mwenyezi Mungu tumekuwa na mashaka juu ya ujanadume wa wanajeshi wetu, na tumekuwa na shaka ya imani zao na uchamungu, na tumekuwa ni wenye shaka juu ya ushujaa na wema wao. Kwa nini hawajachukua hatua baada ya yote wanayoyaona na kuyasikia? Nini kinacho washughulisha na kuwazuia kutokana na kutekeleza majukumu yao yanayowawajibikia, na riziki zao zikipatikana kutokana na damu na pesa za Waislamu? Masikitiko makubwa kwao, wanawachukiza Waislamu wakati wakiwasubiri kuingiliakati kwao katika matukio ili kuyarekebisha, na wakiongoza kwenye kuganda damu, kiharusi, wasiwasi, kurudi nyuma kisaikolojia na maradhi yote ya mfadhaiko na huzuni; yakiwasubiri maasi yatakayoondoa viti vya enzi vya watawala vibaraka!  Masikitiko makubwa kwao, kumetokea nini kwenu, enyi maafisa na wanajeshi? Nini kimetokea kwenu, enyi vijukuu vya Omar na Salahuddin? Kanusheni shaka zetu juu ya ujanadume wenu na wema, na msituangushe, panguseni vumbi la udhalili na kujishusha hadhi, na futeni aibu ya udhalilifu kwa Ummah, udhaifu na ufidhuli, na jifungeni kuzifikia bishara za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa kuiunga mkono Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itapigana na Mayahudi na kuikomboa Roma.                                                            

Kusimamishwa kwa Khilafah na kukombolewa Al-Quds kutatuweka katika orodha ya wenye kuabudu wateule Wake, ambao Mwenyezi Mungu ametutunuku ubora huu, ambapo hakuna anayelingana nasi na kushindana nasi katika wema huu. Basi hilo litakuwa ni jeshi lenye baraka tele. Watarudia kwa ajili ya Uislamu masiku ya Al Qadisiyah, vita vya Yarmouk, vita vya upanga vya Khaybar, mashambulizi ya Khalid na Ukombozi wa Salahudin na Ukombozi wa majeshi ya Uthumaniya. Hongera kwa Jeshi litakalo fungua Al-Quds siku za mwishoni kwa mara nyingine, na wanajeshi wakiwa na mizinga, ndege za kivita na vifaru vya Khilafah huku wakinyanyua bendera za Iman na bendera ya Al ’Uqab, ili Mwenyezi Mungu (saw) afungue miji zaidi na mataifa kupitia mikono yao kama vile miji ya Roma, London na Washington, na pongezi kwa watu wa kijani kibichi ni zaidi ya pongezi kwa watu wa vumbini. Baraka kwao kwa kutimiza bishara ya al-Habib al-Mustafa kwa kufungua Roma, kutokana na mapokezi ya Ahmad na wengineo kutoka kwa Abi Qabeel, alisema: Tulipokuwa pamoja na Abdullah Ibn Amr Ibn Al-As, aliulizwa; Upi kati ya Miji miwili utafunguliwa kwanza, ni Konstantinopoli au Roma? Abdullah akaomba sanduku, akatoa kitabu na akasema, Abdullah akasema: “Tulipokuwa pamoja na Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) tukiandika, Nabii wa Mwenyezi Mungu aliulizwa, ni upi kati ya miji miwili utafunguliwa mwanzo, Kostantinopoli au Roma?” Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلاً، يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ»

“Mji wa Heraclius utafunguliwa mwanzo, akimaanisha Kostantinopoli”

Watabarikiwa wakati bishara ya Mtume (saw) itakapo fanikishwa kwa kuenea Uislamu katika kila pembe ya dunia, hakuna nyumba ya tofali wala manyoya itakayosazwa, isipokuwa Mwenyezi Mungu ataingiza Dini yake humo, ambapo mwenye heshima atatukuzwa na mwenye udhalili atadhalilishwa. Kutoka kwa Tamim Ad-Dary, alisema, nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema:

«لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزّاً يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلّاً يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ»                                    

“Jambo hili (Uislamu) litafika kila mahali ambapo panafikiwa na usiku na mchana. Na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba yoyote iwe ya manyoya au tofali, isipokuwa Mwenyezi Mungu ataingiza Dini yake humo, ambapo mwenye heshima atatukuzwa na mwenye udhalili atadhalilishwa. Mwenyezi Mungu atawatukuza wenye heshima kwa Uislamu na atawadhalilisha wenye udhalili kwa ukafiri.”

Baraka ni za kwao wakati dunia yote itakapokuwa chini ya hukmu ya Uislamu, na imethibitishwa katika Hadithi sahihi ya Mtume (saw) aliposema:

«إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِي الْأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا»           

“Mwenyezi Mungu ameisogeza ardhi kwangu nikaona mashariki yake na magharibi yake, na kuwa Ummah wangu utafikia utawala wake kule nilikosogezewa”

Bishara kubwa iliyoje hii na utabiri ulio wa kweli kama huu, na shani ya kiasi gani hii kwa Waislamu hivi leo kujishughulisha katika kazi itakayofanikisha bishara hii kupitia mikono yao. Ewe Mwenyenzi Mungu tujaalie tuwe miongoni mwao ambao wataisimamisha Khilafah, kuikomboa Al Quds (Jerusalem), na kuikomboa Roma na miji yote ya kikafiri. Ewe Mola wan’goee wakandamizaji, Waamerika, Mayahudi, na watawala wa Waislamu wanaowafuata wao.

                     Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na                                    Ustadh Sulaiman Al-Muhajiry- Yemen

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Machi 2020 21:26

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu