Ijumaa, 14 Shawwal 1441 | 2020/06/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Nigeria Yakabiliana na Mustakbali Usiothabiti

Tangu uhuru mwaka wa 1960, historia ya kisiasa ya Nigeria imekuwa ya kuzongwa na matatizo kadhaa - vita vya kikabila, vita vya kidini, vita vya mafuta, mapinduzi ya kijeshi nk. Takribani asilimia 75 ya miaka baada ya uhuru ilitumiwa chini ya utawala wa kijeshi na udikteta. Hata hivyo, ghasia za Nigeria hazijawahi kufikia kiwango cha wenzao wa Afrika kama Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Nigeria ilikuwa kwenye rada ya wakoloni wa Ulaya kwa karne nyingi. Ilikuwa ni sehemu ya 'Pwani ya Wafungwa' na iliyo barikiwa na rasilimali za madini. Waingereza waliweka waliiteka na kufanya biashara ya utumwa na kusafirisha mafuta ya nazi nje.

Japo, ilipata upinzani kutoka kwa watawala kama wa Sokoto na Mfalme Koko, meli zao za 'Wamisheni' zilichukua udhibiti wa moja kwa moja katika baadhi ya sehemu na njia isiyo ya moja kwa moja katika sehemu nyinginezo. Waingereza walikuja Nigeria na ujumbe wa kueneza Ukristo kwa njia ya Wamishenari. Lakini ukweli nyuma ya 'Umisheni' wake ilikuwa ni ukoloni.

Makubaliano ya dola kuu za kiulimwengu katika kongamano la Berlin (1889-1890) yalianzisha Kinyang’anyiro cha Afrika. Hili liliifanya Afrika kuwa mali ya kibinafsi ya mataifa ya kikoloni. Mfalme Leopold wa Ubelgiji alitangaza makoloni yake kama falme zake za kibinafsi.

Nigeria iligundua mafuta mwaka wa 1956. Hii iliifanya Nigeria kuwa 'Hifadhi' au 'Mamlaka' muhimu na yenye thamani zaidi. Hili pia lilikuja wakati ambapo mizani ya utawala ya kimataifa ilikuwa inagura na mivutano ya kudhibiti maeneo ya mafuta ilikuwa kwa kasi duniani kote. Afrika bado haikuwa sehemu ya uwanja wa siasa za kiulimwengu hadi 1960.

Kwa hivyo, maslahi ya Uingereza hayakukabiliwa na tishio lolote nchini Nigeria mpaka kuibuka kwa Marekani kuwa dola kuu duniani baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Ulaya yote ilitingishwa na vita hivi, kufuatia kumalizwa kwa rasilimali zake na Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na Mporomoko Mkuu wa kiuchumi wa 1929. Hili liliifanya kuyakamata kwa nguvu zaidi makoloni yake.

Marekani iliibuka yenye nguvu kubwa na jeshi lake baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Ilijitokeza kudhibiti ulimwengu baada ya kugundua na kuonja kiasi ‘kikubwa’ cha mafuta duniani. Kisha ilianza kusaidia harakati za uhuru katika ‘Ulimwengu wa Tatu' – Mataifa yaliyo koloniwa. Kwa hiyo, ilifunga mkataba na Nikita Khrushchev, Waziri Mkuu wa Soviet mwaka 1961, ili kugawanya ulimwengu kati ya Marekani na Umoja wa Kisovieti. Hii ndiyo iliyokuwa sababu ya Marekani kuwaruhusu Wakomunisti kuingia sehemu za Afrika na Asia. 

Ilhali, 'Uingereza Kuu' ilikuwa inageuka kuwa 'Uingereza Ndogo', Marekani iligundua kwamba ilistahili kuinyang’anya Ulaya makoloni yake ili kuimarisha nafasi yake ya kimataifa. Baada ya kutoa 'uhuru' kwa Makoloni haya, Wakoloni waliwaachia mamlaka vibaraka wao ili kuhifadhi maslahi yao; hii ndiyo iliyokuwa sababu ya mapinduzi na mapinduzi dhidi.

Uingereza iligundua kwamba ilikuwa dhaifu sana kukabiliana na Marekani moja kwa moja, kwa hiyo ilipitisha sera ya Kujihifadhi Kibinafsi (Self-Preservation), ambayo ilifanywa kwa njia mbili: kushirikiana na Marekani na kutibua mipango yake wakati mwingine; ikitaraji kushawishi matokeo ya kisiasa kwa manufaa yake katika hali zote mbili. Kama alivyosema katika nukuu yake maarufu mno; Bwana Henry John Temple, 3rd Viscount Palmerston – Waziri Mkuu wa Uingereza wa wakati huo katika karne ya 19 –'Hatuna washirika wa milele, na hatuna maadui wa kudumu. Maslahi yetu ndiyo ya milele na ya kudumu, na maslahi hayo ni wajibu wetu kuyafuata'. Hii ni taarifa inayo heshimiwa na dola zote za kikoloni.

Licha ya udhaifu wake, Uingereza ni nzuri katika ujanja wa kisiasa. Katika kitabu chake, ‘The Post American World’, Fareed Zakaria alitoa ufupisho wa Sera ya Kigeni ya Uingereza baada ya Vita vya Pili vya Dunia: 'Picha za Roosevelt, Stalin na Churchill katika kongamano la Yalta mnamo Februari 1945 kwa kiasi fulani zinapotosha. Hakukuwa na 'wakubwa watatu ' huko Yalta. Kulikuwa na 'wakubwa wawili ' pamoja na mjanja mmoja mahiri mfanyi biashara wa kisiasa aliyeweza kujiweka yeye na nchi yake katika mchezo huo, ili Uingereza idumishe vyema mambo mengi ya ufalme mkuu hadi mwishoni mwa karne ya 20.’

Baada ya miaka ya kupanda na kushuka kwa watawala wa kiraia na kijeshi, Marekani hatimaye ilipata mshiko thabiti juu ya Nigeria wakati Olusegun Obasanjo alipochukua utawala mwaka 1999. Marekani ili hakikisha kuwa kibaraka wake alichaguliwa baada ya Obasanjo mpaka uchaguzi wa 2015 wakati kibaraka wa Uingereza kwa muda mrefu, Muhammadu Buhari, alijitokeza huku akitabasamu kutokana na bahati ya kushinda uchaguzi baada ya kugombea kwa miaka mingi. Marekani haikuwa na chaguo kwa sababu ilikosa mtu muaminifu wa kumuunga mkono – kwani Goodluck Jonathan alikuwa ameharibu mipango yake. Kuyachakachua matokeo ya uchaguzi na kumkabidhi ushindi mgombea wake kungechochea ghasia, hasa eneo la Kaskazini – ambalo ni ngome ya Buhari. Marekani kwa hakika hakutaka hilo. Buhari alichukua utawala kwa niaba ya Waingereza. Alikuwa, hata hivyo, akizungukwa na viabaraka wa Marekani; mfano wa Saraki na Kwankwaso.

Marekani inafanya jitihada kubwa za kupata mgombea wa kuaminika. Lakini 2019 hauonekani kama mwaka wa yeye kuitia mikononi tena Nigeria. Mgombea anayetarajiwa zaidi, Atiku Abubakar, ana hadhi duni machoni mwa watu wa Nigeria – hasa eneo la Kaskazini lenye wakaazi wengi ambapo Buhari anaungwa mkono kiupofu. Gavana wa zamani wa Kano, Kwankwaso, huenda akawa chaguo bora zaidi.

Tatizo la Nigeria lilisababishwa na ulafi wa Ukoloni wa Kimagharibi. Historia ya kisiasa ya Nigeria daima imekuwa ni hadithi ya mapambano ya kikoloni.

Kwa hiyo, uchaguzi wa 2019 ni mapambano kati ya dola za Kikoloni – nchini Nigeria, ni Marekani na Uingereza. Nigeria ni lazima ijikomboe kutokana na minyororo ya Ukoloni na inapaswa kubeba fikra safi yenye natija kwa binadamu ili kupata maendeleo ya kikweli.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Umar Abu Ammar Bin Ahmad

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu