Jumamosi, 03 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuufahamu Udhaifu Wetu Hutufanya Tuwe Imara Katika Dini Yetu

Funzo moja muhimu ambalo virusi vya Korona vimeifunza dunia, ni kuwa mmoja ya mkaazi wake mdogo kabisa ameweza kuvuruga maisha kama tunavyo yafahamu. Kirusi kikiwa na wastani wa kipenyo cha takriban nanomita 120 hakikutenganisha baina ya mataifa yaliyo endelea kidogo na yaliyo endelea sana au ima mtu ni tajiri, aliye elimika au mzuri. Kile ilicho kifanya, kinatusukuma kuchukua hatua moja nyuma kutoka katika maisha tuliokuwa nayo na kutathmini malengo ya kimaisha ya muda mfupi na muda mrefu tuliyoweza kuyaweka, kwa kuwa maisha tunayoishi ghafla yamevurugika.

Namna ambavyo mtu anashughulikia matatizo katika maisha hutegemea imani na maadili ambayo ndio huathiri fikra na matendo yao. Tukiwa Waislamu tumebarikiwa na muongozo wa Aliye Mkuu, Muumba wa vyote vilivyo tuzunguka, ikiwemo virusi vya Korona.

Hivyo sisi kama Waislamu wakati tukitafakari juu ya kuvunjika kwa maisha, na namna tunavyo hitajia kuiunganisha fikra hii kwa usahihi, wakati tukiunda maisha yetu wenyewe. Tutaregea kwenye Quran na Sunnah ili kupata muongozo sahihi na kutusaidia kufanya maamuzi ya sawa.

Kwa mfano Mwenyezi Mungu (swt) ametuumba, anajuwa kuwa malengo yetu mengi ya kimaisha yanahusiana na hamu ya kukusanya mali. Hivyo Yeye (swt) ametuonya kwa hilo katika Quran:

[الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا]

Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini” [Surah Al-Kahf 18:46]

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[يَوْمَ لا يَنْفَعُ مَالٌ وَلا بَنُونَ * إِلاَّ مَنْ أَتَى اللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيم]

“Siku ambayo kwamba mali hayatofaa kitu wala wana. Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi” [Surah Ash-Shu’araa 26:88-89].

Aya hizi zinatukumbusha na kuunda fikra zetu na matendo yetu ili tusichukue nafasi ya masuala muhimu zaidi kama jitihada katika kufanya matendo mema badala ya kushughulikia matamanio yetu au kutafuta malengo ya kidunia, kama kukusanya mali.

Kila tunapokumbushwa kuwa uhalisia uliopo ni tepetepe ndipo tutapojifunga zaidi kuwekeza katika “kile kisichomalizika” kinachofuatia. Kwa maneno mengine, tunapoishi katika maisha ambayo tunafahamu kuwa ni ya muda na mtihani kwa kile kinachokuja, hatutojawa na tamaa za starehe na kutozingatia mipaka ya Mwenyezi Mungu (swt) aliyoiweka.

Abu Huraira (ra) amesimulia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

«إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلَى صُوَرِكُمْ وَأَمْوَالِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وَأَعْمَالِكُمْ»

“Hakika Mwenyezi Mungu haangalii sura zenu na mali zenu lakini anaangalia nyoyo zenu na matendo yenu.” (Muslim)

Na ufahamu sahihi wa udhaifu wa maisha haya unatusaidia kushughulikia majanga yanapotukumba kama wakati sahaba mtukufu Sa’ad ibn Muadh (ra) alipokufa na mama yake akilia, Mtume (saw) alimwambia,

«أَلَا يَرْقَأُ (ينقطع) دَمْعُكِ، وَيَذْهَبُ حُزْنُكِ، فَإِنَّ ابْنَكِ أَوَّلُ مَنْ ضَحِكَ اللَّهُ لَهُ، وَاهْتَزَّ لَهُ الْعَرْشُ»

“Basi chozi lako na likatike na huzuni yako iondoke kwani mwanao ni wa mwanzo ambaye Mwenyezi Mungu atatabasamu kwake na Arshi Yake kutetemeka.” (At-Tabarani).

Kufikiria kuhusu udhaifu wa maisha utufanye tutake kusahihisha maisha yetu, kwa kufahamu lengo letu katika maisha. Itushajiishe kuisoma Dini ili tuweze kufahamu malengo yetu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa upana, na kufanya kila kitu kilicho kwenye uwezo wetu kuyakimbia makatazo Yake. Itufanye tuitamani siku ambayo tutashuhudia kila hukmu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameiweka kuwa imetekelezwa na itufanye tuwepo mahala ambapo tutakuwa ni sehemu ya harakati ambayo inalingania kuregea kwa Uislamu kuwa ni ajenda yetu kuu. 

[أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ]

“Je mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache”. [Al-Taubah: 38]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Yasmin Malik

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 #Covid19    #Korona     كورونا#

#FromAffliction2Success          #MihnettenKurtuluşa             محن_ومنح#

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu