Alhamisi, 19 Rajab 1444 | 2023/02/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chazindua Kampeni ya Kimataifa: “Mabadiliko Halisi ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah PEKEE”

Ulimwengu uko katika machafuko na giza, karibu na mbali. Mateso na taabu za wanadamu zinaongezeka siku hadi siku huku mataifa yakiingia kwenye mgogoro mmoja hadi mwingine. Umaskini, utovu wa usalama wa kifedha, njaa, mauaji ya halaiki, uvamizi wa kikatili, udikteta, vita vya kinyama, kuvunjika kwa familia, maisha yenye uharibifu, milipuko ya uhalifu, unyanyasaji dhidi ya wanawake, matatizo ya afya na elimu na matatizo mengine yanayolemaza yanakumba nchi kote ulimwenguni

Soma zaidi...

Afya ya Watoto wa Umma iko Hatarini bila ya Khilafah

Mnamo tarehe 20 Oktoba 2022, BBC iliripoti kwamba Indonesia imepiga marufuku uuzaji wa dawa zote za kikohozi za watoto baada ya watoto 99 kufariki kutokana na kufeli kwa figo. Iligunduliwa kuwa viwango vya juu vya sumu haramu vilikuwepo ndani ya dawa zilizochafuliwa. Maafisa wanahofia kwamba idadi kamili ya vifo haijajulikana kwani dawa hizo zilikuwa na mzunguko mkubwa.

Soma zaidi...

Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wanakumbwa na Njaa Hadi Kufa Nchini Somalia huku Watawala wa Waislamu Wakiunga Mkono Ukandamizaji Ulimwenguni

Mnamo tarehe 5 Oktoba 2022, BBC iliripoti kuwa Somalia inakabiliwa na baa la njaa inayotokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Hadithi ya dada mmoja Muislamu inayofichuliwa na waandishi wa habari, ni ile ya Fatima Omar ambaye alimzika mtoto mmoja wa kiume kutokana na njaa na tayari alikuwa ameshamzika bintiye wa miaka 3 ambaye alifariki huku akitembea kwa siku 10 kutafuta msaada. Anawaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa na nguvu za kumzika mtoto wake na alilazimika kuuacha mwili wake kando ya barabara huku akijua kuwa Fisi walikuwa wanakaribia kuingia ndani.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu