Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari mnamo Jumamosi, 22 Safar 1447 H sawia na 16/08/2025 M, yenye kichwa: “Wito kwa Watu wa Sudan... Ikamateni Darfur Ili Isiungane na Kusini”
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Jumamosi, 26/7/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilitangaza kuundwa kwa serikali sambamba na serikali iliyopo nchini Sudan, katika mji mkuu wa Darfur Kusini (Nyala). Hatua hii ya RSF ni hatua ya juu katika kutenganisha eneo la Darfur, ambalo inalidhibiti, isipokuwa sehemu za mji wa El Fasher, ambao mzingiro wa kukandamiza umewekwa juu yake kwa zaidi ya mwaka mmoja, na kuanzisha mashambulizi mfululizo dhidi yake ili kuuangusha, ili eneo zima la Darfur liwe chini ya udhibiti wake.