Mpango wa Trump ni Uvamizi wa Kikatili wa Kijeshi Ambao Unahitaji Haraka Kubadilishwa kwa Watawala Wanaokubaliana na Mpango Wake
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katikati ya miaka miwili ya vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea mjini Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mpango wa kina unaolenga kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza na kufikia “amani ya kudumu” katika Mashariki ya Kati. Mpango huu ulitangazwa wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari uliofanyika mnamo Jumatatu, 29/9/2025, na mhalifu aliyelaaniwa Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House. Alisema, “Leo tunalifanyia kazi suluhisho la kina kwa kadhia ya Palestina, sio Gaza pekee.” Miongoni mwa mambo muhimu zaidi katika mpango wake ni mpango wa “kuanzisha chombo kipya cha kimataifa cha uangalizi wa Ukanda wa Gaza kinachoitwa Baraza la Amani.” Aliongeza, “Mimi binafsi nitakuwa mwenyekiti wa baraza hili huko Gaza, kwa ushiriki wa Tony Blair.” Alisisitiza kwamba “washirika wetu wa Kiarabu na Waislamu wako tayari kuchukua majukumu yao kwa Gaza,” na kwamba “ufadhili ni muhimu ili kuruhusu mafanikio mjini Gaza, na tutajenga mustakabali salama zaidi kwa wote.”