Wakenya Amkeni
- Imepeperushwa katika Siasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kenya, shamba la kikoloni, kwa mara nyingine imo katika mchafuko na mtikisiko kwa kuwa mchezo wa bahati nasibu wa kidemokrasia umezunguka nyuzi 360! Walioko madarakani na walioko barabarani wakiandamana wanalaumiana, huku madai yakielekezwa kwa Mswada wa Kifedha wa 2024 ulioandaliwa kwa maelekezo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) (Business Daily, 28 Juni 2024)! Mswada huo unapendekeza mikakati ya kuzidisha ukusanyaji wa ushuru ambao unatajwa kuwa ni wenye kukandamiza na kuwadidimiza raia katika umasikini zaidi!