Jibu la Swali: Biashara ya Mtandaoni (E-Commerce)
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kifiqh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Je, biashara ya mtandaoni (e-commerce) na kampuni ya DXN ya Malaysia inaruhusiwa? Kampuni hii inategemea uuzaji wa virutubisho vya lishe, shampoo, krimu za ngozi...nk. Unapo nununua kutoka kwake kiasi fulani, inatoa punguzo (discount). Pindi pointi zako zikifika 100 inakupa punguzo la asilimia sita. Kadiri unavyopata pointi zaidi, ndivyo inavyokupa punguzo kubwa zaidi, na pointi hizi hubadilishwa kuwa kiasi cha pesa ambacho huhamishiwa kwako ama kwa njia ya bahasha au barua ambayo hutolewa kwako kila mwezi, au kuhamishiwa kwenye salio (balance) lako la benki.