Katikati ya Mvutano wa Nchi za Kikoloni juu ya Ushawishi nchini Yemen ni Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume Pekee ndiyo Itakayomaliza Mateso ya Watu wa Yemen
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo siku ya Jumatano, maandamano maarufu yalianza kwa siku ya pili mfululizo katika Jimbo la Aden. Waandamanaji walifunga barabara katika vitongoji vya Mansoura na Sheikh Othman. Maandamano hayo yalijumuisha majimbo jirani ya Lahj na Abyan, juu ya hali mbaya ya maisha na kuongezeka kwa bei za juu, pamoja na kukosekana kwa huduma msingi kama vile umeme, maji, na huduma za afya, ambazo zimeyasibu Majimbo hayo kusini mwa Yemen kwa miaka mingi.