Marekani Inatafuta Ushindi Madhubuti nchini Afghanistan
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Serikali ya Marekani, kupitia taasisi za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, inalenga kupata ushindi madhubuti. Ni ushindi ambao haikuweza kuupata, licha ya zaidi ya miaka ishirini ya vita dhidi ya Uislamu na Mujahidina nchini Afghanistan. Utafutaji ushindi huu ulianza pale Marekani ilipoiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa vuguvugu la Taliban, na kufungua afisi kwa ajili ya vuguvugu hilo huko Doha mwaka 2013. Kupitia afisi hii, Marekani ilijihusisha kisiasa na harakati hiyo, na kusababisha duru kadhaa za mazungumzo yaliyohusisha Marekani na waamuzi, ukiwemo ujasusi wa Pakistan.