Kwa Maongezi Matamu, Yenye Sumu kuhusu Mustakabali wa Lebanon na Kanda! Mjumbe wa Marekani Tom Barrack yuko nchini Lebanon Kuimarisha Kukamilishwa kwa Makubaliano ya Amani na Uhalalishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi!
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Julai 7, 2025, katika mkutano na waandishi wa habari katika Kasri la Rais, Mjumbe wa Marekani Tom Barrack alitoa taarifa akisema kwamba "Lebanon na kanda hii wana fursa nzuri ambayo lazima ichukuliwe," kwamba "wakati umefika wa kubadilisha kanda hii," na kwamba "kila mtu amechoshwa na kile kilichotokea," kama alivyoweka. Pia alisema kwamba "usalama utavutia uwekezaji kwa Lebanon," kwamba "Rais wa Marekani alithibitisha dhamira yake ya kuchangia kujenga amani na ustawi nchini Lebanon," na kwamba "fursa inapatikana kwa Walebanoni kuifanya nchi yao kuwa Lulu ya Mashariki kwa mara nyingine tena."