Simama pamoja na Watu Wasioteteleka wa Gaza, Sio na Trump Mwenye Kiburi!
- Imepeperushwa katika Uturuki
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Miaka miwili imepita tangu mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi huko Gaza, ambalo liliyafanya ili kuficha kushindwa kukubwa lilikokupata mnamo Oktoba 7, 2023. Miaka miwili ambayo kila siku ilishuhudia mauaji mapya na ukatili usioelezeka, na dunia nzima imeshuhudia ukatili wa Mayahudi wanyakuzi ambao unakinzana na akili. Watoto, watoto wachanga, nyumba, shule, misikiti na hospitali zililengwa. Watawala wa nchi za Kiislamu walikutana mara kwa mara, wakazungumza, wakalaani, na kisha kutawanyika. Kila shutma iliwashajiisha Mayahudi kufanya uvamizi na mauaji makubwa zaidi. Umbile la Kiyahudi lilifikia hatua ya kuzuia kuingia kwa kipande cha mkate au tama la maji ndani ya Gaza kwa miezi mingi mirefu.