Kauli za Uhalalishaji Mahusiano ni Tangazo la Wazi la Kuoanishwa na Adui na Kujitenga na Ummah
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Siku za hivi karibuni zimeshuhudia msururu wa kauli zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty wakati wa ushiriki wake katika makongamano ya kimataifa. Maarufu zaidi kati ya kauli hizi ni msisitizo wake juu ya “umuhimu wa 'Israel' kuishi kwa amani na kuoanishwa ndani ya eneo hili,” na “utayari kamili wa kuhalalisha mahusiano na ‘Israel’" pamoja na Saudi Arabia na nchi zengine, na kauli yake kwamba “suluhisho pekee kwa mustakbali ni kuanzishwa kwa dola ya Palestina isiyo na kijeshi inayoishi kwa amani na ‘Israel’.” Kauli hizi waziwazi zinaakisi mwelekeo unaofuatwa na tawala zilizoko katika nchi za Kiislamu: njia iliyojaa uhalalishaji mahusiano na umbile nyakuzi, na hata juhudi za kulilinda na kulioanisha ndani ya eneo hili, kuhudumia mradi wa kikoloni wa Magharibi.