Jumatatu, 03 Safar 1447 | 2025/07/28
Saa hii ni: 03:41:21 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mkataba wa Biashara na Unyenyekeaji wa Indonesia kwa Maslahi ya Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza makubaliano ya kibiashara na Indonesia, kupunguza ushuru unaotishiwa wa 32% kwa bidhaa za Indonesia hadi 19%. Kwa upande wake, Indonesia ilijitolea kununua nishati ya Marekani kwa dolari bilioni 15, bidhaa za kilimo kwa dolari bilioni 4.5, na ndege 50 za Boeing, ikiwa ni pamoja na aina ya 777. Trump alidai Marekani itapata ufikiaji kamili wa soko la Indonesia bila kulipa ushuru. Makubaliano hayo yalifuatia vitisho vya ushuru wa juu na yalikamilishwa baada ya mazungumzo na Rais wa Indonesia Prabowo Subianto. Bado haijulikani ni lini upunguzaji wa ushuru na ununuzi utaanza kutekelezeka. Biashara ya Indonesia na Marekani ilifikia karibu dolari bilioni 40 mwaka 2024, na nakisi ya biashara ya bidhaa za Marekani ya takriban dolari bilioni 18.

Soma zaidi...

Idhini ya Marekani sio Kipimo cha Uamuzi wa Kisiasa kwa Umma wa Kiislamu

Mnamo tarehe 17 Julai 2025, Dawn News ilinukuu kutoka Reuters, "Ikulu ya White House mnamo Alhamisi ilisema kwamba hakuna ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump iliyopangwa Pakistan "kwa wakati huu" baada ya kuenea kwa taarifa za safari hiyo. Mapema siku hiyo, baadhi ya vituo vya habari vya televisheni vya ndani viliripoti, vikinukuu vyanzo, kwamba Trump alitarajiwa kuzuru Pakistan mwezi Septemba. Chaneli za habari zilisema kwamba Trump pia angetembelea India baada ya kuwasili jijini Islamabad mwezi Septemba. Chaneli hizo baadaye ziliondoa ripoti zao.” [Dawn]

Soma zaidi...

Uislamu uko Mbali na Mazungumzo ya Dini Mseto

Mnamo tarehe 5 Julai 2025, jumba jipya la ibada katika Kanisa la Arise and Shine Tanzania lililopo Kawe, viungani mwa jiji la Dar es Salaam lilizinduliwa. Kanisa hilo linaongozwa na Mwinjilisti na anayejiita ‘mtume’ Boniface Mwamposa ambaye mahubiri yake mwaka 2020 yalileta msiba wa vifo vya waumini zaidi ya 20 kutokana na mkanyagano waliokuwa wakikimbia kupakwa mafuta yenye baraka.

Soma zaidi...

Mpango wa Mosaic: Kubadilisha Chapa Mkakati Uliofeli na Jaribio Jipya la Kuidhibiti Taliban

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilifanya kikao maalum kujadili hali ya Afghanistan. Katika mkutano huu, Roza Otunbayeva, mkuu wa Misheni ya Misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA), aliwasilisha mfumo mpya wa kina unaoitwa "Mpango wa Mosaic." Alisisitiza kuwa mpango huu haulengi "kusawazisha hali nchini Afghanistan," bali unalenga kuendeleza maslahi ya kweli ya watu wa Afghanistan.

Soma zaidi...

Marekani Yapanga Mpango Mpya baada ya Mpango wa Awali Kufichuliwa na Kutibuliwa na Umma

Makundi yenye silaha ya Rohingya yameanza kusajili kutoka kambi za wakimbizi za Cox's Bazar kusaidia katika mapigano dhidi ya Jeshi la Arakan huko Rakhine. Taarifa hiyo ilifichuliwa katika ripoti moja ya Shirika la Kimataifa la kutatua Migogoro yenye kichwa "Bangladesh/Myanmar: Hatari za Waasi wa Rohingya". Ripoti hiyo inabainisha kuwa, baada ya Jeshi la Arakan kupata ushindi dhidi ya jeshi la Myanmar huko Rakhine, makundi ya Rohingya yamezidi kuwa changamfu na yamekubali kufanya kazi kwa pamoja dhidi ya Jeshi la Arakan, kundi ambalo lenye Mabudha wengi wa Rakhine kuwa kambi yake. (The Business Standard, 18 Juni 2025)

Soma zaidi...

Erdoğan anapaswa Kuhutubia Umma wenye Ikhlasi na sio Walinzi wa Sykes-Picot kwa Umoja na Udugu wa Kiislamu!

Akihutubia Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu jijini Istanbul, Rais Recep Tayyip Erdoğan ametoa wito wa kuwepo umoja na udugu mkubwa zaidi miongoni mwa nchi za Kiislamu. Erdoğan pia alisema, "Hatutaruhusu kuanzishwa kwa agizo jipya la Sykes-Picot katika eneo letu mipaka kuchorwa kwa damu." Na alisisitiza kwa mara nyengine kwamba suluhisho liko katika "diplomasia na mazungumzo".

Soma zaidi...

Umebarikiwa kwa Nguvu, Umedhoofishwa na Mgawanyiko

"Pentagon yasema Marekani haitaki kuanzisha vita na Iran" - hii, baada ya kudondosha mabomu kumi na nne aina ya bunker-buster kwenye vituo vitatu vya nyuklia ndani ya ardhi ya Iran. Kauli kama hiyo si ya kinafiki tu - ni ya kuchukiza. Inaakisi mawazo ya kiburi, ya kikoloni. Mtu yeyote mwenye akili timamu anawezaje kuamini kwamba vita sio nia pindi taifa linapofanya mashambulizi yaliyoratibiwa kwa taifa jengine?

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu