Kutoka Uingereza hadi Australia: Utambuzi wa Uongo Unafungua Njia ya Uhalalishaji Mpana zaidi wa Mahusiano
- Imepeperushwa katika Australia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Miaka miwili baada ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na umbile la Kizayuni katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, likiungwa mkono kikamilifu na Marekani, NATO, na washirika wao makruseda, Umoja wa Mataifa na dola zenye nguvu duniani wamejibu kwa kulituza umbile hilo. Utambuzi wa “Dola ya Palestina” unakuja huku Gaza ikivuja damu, na baada ya dola 150+ tayari kutoa utambuzi sawia.